Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Mtu ukiwa unalima shamba huhitaji press. Vikao vya Kamati za Bunge na vikao vya Bunge ni vikao serious vya kikazi. Wananchi wanachohitaji kujua ni matokeo ya kile walichojadili sio zile porojo za sijui mbunge huyu akachekesha, huyu akatukana. Wananchi wanachohitaji ni final result za kikao.
Ukiweka live Wabunge wengi wanageuza vikao vya Bunge au Kamati za Bunge kuwa sehemu ya kuuza sura kwenye vyombo vya habari badala ku-concentrate kwenye kazi.
Nakumbuka kuna Mbunge mmoja alishawahi mkunja mtangazaji wa radio ya Kenya, KBC, akifoka kwa Kiingereza kibovu akisema ''You KBC why not announce my voice?'' Alimaanisha kwa nini huwa hawamtoi hewani akiongea bungeni.
Wabunge wetu kuwa serious na kazi za bunge hawahitaji kuwa live. Utafiti niliofanya binafsi nimegundua wachangiaji bungeni wamepungua toka bunge lilipoacha kuonyeshwa live. Lilipokuwa liko live spika alikuwa na kazi ya ziada ya kuamua ampe nafasi nani aongee kila mbunge alikuwa anataka kuuza sura hewani na asikike hewani.
Sasa hivi wachangiaji ni wachache walio serious tu. Wabunge wengi wameingia mitini bunge live lilipoondolewa. Spika kwenye mijadala Hana kazi kubwa.
Una hoja za hapa na pale, lakini ukweli wabunge wengi kuacha kuchangia kumesababishwa na jiwe kupora mamlaka ya bunge, na kuligeuza kikundi cha wala hela za wananchi kisheria. Unachangia jambo gani la maana kama maamuzi yote anafanya rais? Mfano mzuri juzi Makonda anaomba hela ya ujenzi wa hospitali wakati ilishaombwa huko bungeni, na rais kashindwa kuweka rekodi sawa akaishia naye kwenye siasa za majitaka. Kwa sasa hakuna bunge bali kuna genge la wahuni wa ccm wanaomsifia rais kwenye jengo la bunge.