Kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Vikao vya Bunge au Kamati za Bunge zikiwa kazini hakufai


Una hoja za hapa na pale, lakini ukweli wabunge wengi kuacha kuchangia kumesababishwa na jiwe kupora mamlaka ya bunge, na kuligeuza kikundi cha wala hela za wananchi kisheria. Unachangia jambo gani la maana kama maamuzi yote anafanya rais? Mfano mzuri juzi Makonda anaomba hela ya ujenzi wa hospitali wakati ilishaombwa huko bungeni, na rais kashindwa kuweka rekodi sawa akaishia naye kwenye siasa za majitaka. Kwa sasa hakuna bunge bali kuna genge la wahuni wa ccm wanaomsifia rais kwenye jengo la bunge.
 
Sasa hivi wachangiaji ni wachache walio serious tu. Wabunge wengi wameingia mitini bunge live lilipoondolewa. Spika kwenye mijadala Hana kazi kubwa.
Mkuu, kuna namna nyingi za kujipendekeza. Wewe umechagua hii. Tumekuelewa.

Kumbuka tatizo la kuogopa Bunge live ni watu kuficha upuuzi wao ambao wananchi mwishowe watauona wazi, sio kuzuia kuuza sura. Kuna mbunge wapiga kura wake wakiona upuuzi anaoongea hawawezi kumchagua tena, na wengi wao ni wabunge wa CCM, sio upinzani.
 

Kama ni hivyo ukikata issue unasikika tu Magufuli anavyolazimisha live kila tukio ana maana gani? Kwa taarifa yako kuona ni kuamini. Ingekuwa watu wanalazimishwa kuacha kazi waangalie bunge live kungekuwa na hoja, lakini kumbe kuangalia ni uamuzi wako. Hapo inaonekana nia ya kuzima bunge ilikuwa ni nia ovu.
 
Kuzindua ni sherehe ndio maaana huitwa sherehe ya uzinduzi huwezi linganisha na kikao Cha bunge

Vile vikao na wafanyabishara nk navyo vinaangukia kwenye huu utetezi wako? Bora ukae kimya tu maana hapa ni kama unasonga kwa mafuta taa.
 
Ujinga mwengine bhana,yaani unaacha kumlisha mwanao kisa akishiba anaenda chooni,kisha unajisifu baada ya kuacha kumlisha mwanao kwenda chooni nako kumepungua wakati kula ni haki ya mtoto,akili za kipunguani utazijua tu.
 
Bunge huwa linatoa yaliyofikiwa kwa vyombo vya habari baada ya Vikao vya bunge na kamati
Wananchi kufuatilia mijadala ya bunge huelewa zaidi basis ya maamuzi kuliko kuhadithiwa kupitia vyombo vya habari. Kaman TBC1 inaona kurusha Bunge Live ni ghali kwa sababu za kibajeti, serikali iruhusu TVs za kampuni binafsi ziwahabarishe wananchi. Tunaamini TVs binafsi zipo willing na zinamudu jukumu Hilo.
 
Mbumbumbu mna kazi kweikwei!
 
Wewe umejuaje kuwa wachangiaji wameingia mitini na bunge halionyeshwi live? Kwa hiyo bunge live lilifutwa ili kumpunguzia spika kazi?

Kama wananchi wanataka mrejesho wa mwisho, mbona sasa mzee Meko yuko live kila siku? Kwa nini sasa mambo yake asiwe anatafanya live mwisho wa siku tupate mrejesho tu?

Spika juzi kawapongeza kenya kurusha vikao vya bunge live, kwa hiyo na yeye ni punguani? Au wewe ndie punguani? Au wewe ni mke wa spika?
 
Sherehe ya kula sambusa ikulu ina manufaa gani kwa taifa?
Inamwingiza kipato muuza sambusa na sambusa si unajua zinatumia nyama na vitunguu na ngano? Muuza bucha anapata chake na muuza ngano na vitunguu anapata chake na muuza mafuta ya kukaangia anapata chake na TRA inapata chake .Pato la taifa linaongezeka kwa Mtu mmoja mmoja na kwa taifa pia kupitia TRA.Na Pato la TRA likiongezeka huduma za jamii zinaongezeka
 
Watu wengi wanaotaka bunge live nnauhakika hawajui wanachokihitaji, mfano rahisi muulize ,unataka maendeleo jimboni kwako au kuona wabunge wakiwa dodoma?

Nazaidi wengi wao hushinda kuangalia bunge tuu bila kufanya shughuli zozote za maendeleo halafu mwishoni wanasema nchi ni masikini kume chanzo cha umaskini ni wao NAMBA MOJA full stop!!!!!!!
 
Mrejesho unaupataje wakati mjadala hauonekani? Kwa njia ya TV habari au magazeti?

Wabunge wao wanakazi gani wakienda kwenye majimbo yao?, halafu si kweli kwamba mrejesho wa yanayotokea bungeni hautangazwi ACHA KUPOTOSHA WATU MKUU
 
Aisee ,....hii Hali mwalimu wangu Prof.Chachage aliita kupumbaishwa kwa halaiki!Kingereza chake nimesahau...Mungu turehemu!
 
Wabunge wao wanakazi gani wakienda kwenye majimbo yao?, halafu si kweli kwamba mrejesho wa yanayotokea bungeni hautangazwi ACHA KUPOTOSHA WATU MKUU
Hebu sema ukweli wewe unadetails gani juu ya mienendo ya nchi na maendeleo yake kupitia bunge na mbunge wako? Weka ushabiki pembeni sema ukweli. Isingekuwa Rais Magufuli kuwa live events mbalimbali na kujaribu kutoa mwelekeo wa serikali yake wewe ungejua nini kuhusu nchi yako? Lakini kumbuka Rais si chombo cha wananchi, chombo cha wananchi kinachofanya maamuzi kwa niaba yao ni Bunge. Rais partly ni mtendaji wa nchi ambaye anahitaji balance ya Bunge.
 
Ila kuona kinachorushwa kutoka ikulu na ziara za raisi magufuli ndio sahihi. Si ndiyo?
 
Hii ni tofauti kabisa kwa sababu inakuwa ni baada ya kazi. ni events baada ya maamuz ( yaan ni matikeo ya kazi) ni sawa na wewe uwe ofisini kila kitu unachofanya kiwe live badala tupate mrejesho wa kaz mwisho wa siku (report)
Huu ni ujinga wa kiwango cha standard gauge? Hivi unakumbuka Bunge lilizuliwa kwa sababu zipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…