Kusafiri umekaa siti moja na mtu anayependa kula hovyo.

tang'ana

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2015
Posts
11,931
Reaction score
15,849
Habari wakuu,

Siku mbili nyuma nilikua safarini kutoka mkoa x kuja mkoa y. Safari yangu niliianza majira ya saa 1 jioni kwa usafiri wa bus.

Sasa kuna mtu tena mmama nilikua nimekaa nae siti moja nikashindwa kumuelewa alikua na appetite ya namna gani.

Kila bus likipiga break yeye lazima anunue kitu cha kula, mara mahindi ya kuchoma, mara yoghurt, soda, juice, korosho, machungwa, biscuits vyote vyake, uzuri hakua mchoyo kila alichokua ananunua alikua ananikaribisha ila bahati mbaya me sio mlaji safarini.

Nilishangaa tumefika sehemu ya kula ilikua ni around saa 8 usiku ila nikamuona kaja na wali kuku hapo ndio nikachoka hivi mtu unawezaje kupata hamu ya kula saa 8 za usiku?

Wasukuma nimewanyooshea mikono kwa kweli.
 
Hicho kibwagizo cha "wasukuma"ukome kututaja...oyaga gete!!hata na ivo maisha ni mafupi sana so ukipata wasaa wa kufanya jambo fanya kwa ufanisi!obheja
 
Aaaah umenikumbusha way back 2020 msimu wa COVID

Nilikuwa na mwanangu tunaenda mkoa, safari ya zaidi ya kilometa 700.

Tumetua tu Moro jamaa akaanza kujikoki kuagiza mazaga mi namcheki tu.

Akaniambia we vipi mbona huagizi nikamjibu mi kwenye safari huwa sili chochote njiani.

Akacheka akasema una tumbo bovu kama la mtoto wa kike..

Na ukumbuke kuwa huo ni usafiri wa umma na pembeni yetu kulikuwa na warembo wakali.

Basi jamaa akatwanga ule msosi wake mara kaagiza juisi, mchizi hakuwa hata na muda wa kuangalia imetengenezwa kwa matunda gani ye alichosema imradi tu iwe ya baridi.

Safari ikaanza.....

Katikati ya safari mara jamaa akaniambia hajiskii vizuri anahisi tumbo lina koroga... namimii nikamtania nikamwambia kama linakoroga jaribu kutia unga.

Basi ile gari kadri lilivyozidi kutembea ndio nilipomuona jamaa hali ikimbadilikia. Nikabaini kuwa ishu imekuwa serious.

Mwisho uzalendo ukamshinda si akaenda hadi mbele kwa suka....suka akamuelewa akasimamisha gari ili jamaa akajisaidie.

Jamaa akaja kuniomba maji yangu yale ambayo nilipewa na wahudumu wa basi kwakua mimi nilijiwekea mazingira ya kutokula njiani kwenye safari so yale maji nilikuwa nayaangalia tu.

Mchizi akachukua maji akashuka kuelekea vichakani. Baada ya muda akarudi na safari ikaendelea.

Tumeenda kama dakika 20 mbele jamaa akamfuata suka tena... Round hii wale masista duu wakasikika wakisema "mweeeh kaka wawatu polee jamani"

Mwana alipofunguliwa tu mlango akatoka nduki....nikajiuliza huyu bwege kaondokaje bila maji??

Aliporudi nikamuambia "we mjinga maji umeishiwa umetumia nini huko?" Akaniambia "nimetumia tiketi kama toilet paper"

Aaah nikishindwa kujiuzia nikacheka...

Tena mbeleni huko hata safari haijachanganya akaomba tena poo gari isimame.

Aliporudi kutoka vichakani nikamumuuliza "na saizi umetumia nini?" Akasema "barakoa"

Safari ikaendelea....tena jamaa kama kawaida yakabipu akashuka.

Aliporudi kabla hata sijamuuliza ametumia nini, yeye mwenyewe akaniambia "nimetumia boxer"

Nikacheka huku nikijikuta namuuliza "kwa hiyo hapo mwanamgu hauna boxer?" Naye kwa hasira akajibu "unauliza ny€ge kwa mfungwa"

Mchizi alifika akiwa hoi na kuanzia hapo anakuambia hata iwe kwenye daladala root ya Buguruni kwa Kariakoo hali chochote njiani.
 
Wengine hucheua na kutafuna
Ww jamaa n fala 😂

Kula mbele za watu ni kitu kinanishinda Sana sijui kwanini
Upo kama Mm, tena mm siwezi kula mbele za watu ambao wao hawali, na kwenye safari mwanzo mpaka mwisho hua sili chochote labla soda tuu tena soda yenyewe nitaanza kunywa mwanzo wa safari na itaisha mwisho wa safari.
 
Hicho kibwagizo cha "wasukuma"ukome kututaja...oyaga gete!!hata na ivo maisha ni mafupi sana so ukipata wasaa wa kufanya jambo fanya kwa ufanisi!obheja
Enyi watu weusi, Kuna mambo mengi ya kufanya maishani zaidi ya kushindilia vyakula masaa 24
 
Habari wakuu,

Siku mbili nyuma nilikua safarini kutoka mkoa x kuja mkoa y. Safari yangu niliianza majira ya saa 1 jioni kwa usafiri wa bus.

Sasa kuna mtu tena mmama nilikua nimekaa nae siti moja nikashindwa kumuelewa alikua na appetite ya namna gani.

Kila bus likipiga break yeye lazima anunue kitu cha kula, mara mahindi ya kuchoma, mara yoghurt, soda, juice, korosho, machungwa, biscuits vyote vyake, uzuri hakua mchoyo kila alichokua ananunua alikua ananikaribisha ila bahati mbaya me sio mlaji safarini.

Nilishangaa tumefika sehemu ya kula ilikua ni around saa 8 usiku ila nikamuona kaja na wali kuku hapo ndio nikachoka hivi mtu unawezaje kupata hamu ya kula saa 8 za usiku?

Wasukuma nimewanyooshea mikono kwa kweli.
Ukishazaliwa Msukuma unazaliwa na matumbo matatu
 
Unampangiaje kula wakati ana appetite iliyokomaa. Halafu ananunua Kwa pesa yake. Wewe ambaye huwezi kula safarini ni huenda huna pesa ya kula au una appetite mbovu
 
Kuna mambo mengi ya kufanya maishani zaidi ya kushindilia vyakula masaa 24
wengine hatukukulia misosi ya kwenye hotpot,vipaumbele vinatofautiana pia kwa hiyo si mbaya kila mtu akitumia uhuru wake ipasavyo!
 
Aaaah umenikumbusha way back 2020 msimu wa COVID

Nilikuwa na mwanangu tunaenda mkoa, safari ya zaidi ya kilometa 700.

Tumetua tu Moro jamaa akaanza kujikoko kuagiza mazaga mi namcheki tu.

Akaniambia we vipi mbona huagizi nikamjibu mi kwenye safari huwa sili chochote njiani.

Akacheka akasema una tumbo bovu kama la mtoto wa kike..

Na ukumbuke kuwa huo ni usafiri wa umma na pembeni yetu kulikuwa na warembo wakali.

Basi jamaa akatwanga ule msosi wake mara kaagiza juisi, mchizi hakuwa hata na muda wa kuangalia imetengenezwa kwa matunda gani ye alichosema imradi tu iwe ya baridi.

Safari ikaanza.....

Katikati ya safari mara jamaa akaniambia hajiskii vizuri anahisi tumbo lina koroga... namimii nikamtania nikamwambia kama linakoroga jaribu kutia unga.

Basi ile gari kadri lilivyozidi kutembea ndio nilipomuona jamaa hali ikimbadilikia. Nikabaini kuwa ishu imekuwa serious.

Mwisho uzalendo ukamshinda si akaenda hadi mbele kwa suka....suka akamuelewa akasimamisha gari ili jamaa akajisaidie.

Jamaa akaja kuniomba maji yangu yale ambayo nilipewa na wahudumu wa basi kwakua mimi nilijiwekea mazingira ya kutokula njiani kwenye safari so yale maji nilikuwa nayaangalia tu.

Mchizi akachukua maji akashuka kuelekea vichakani. Baada ya muda akarudi na safari ikaendelea.

Tumeenda kama dakika 20 mbele jamaa akamfuata suka tena... Round hii wale masista duu wakasikika wakisema "mweeeh kaka wawatu polee jamani"

Mwana alipofunguliwa tu mlango akatoka nduki....nikajiuliza huyu bwege kaondokaje bila maji??

Aliporudi nikamuambia "we mjinga maji umeishiwa umetumia nini huko?" Akaniambia "nimetumia tiketi kama toilet paper"

Aaah nikishindwa kujiuzia nikacheka...

Tena mbeleni huko hata safari haijachanganya akaomba tena poo gari isimame.

Aliporudi kutoka vichakani nikamumuuliza "na saizi umetumia nini?" Akasema "barakoa"

Safari ikaendelea....tena jamaa kama kawaida yakabipu akashuka.

Aliporudi kabla hata sijamuuliza ametumia nini, yeye mwenyewe akaniambia "nimetumia boxer"

Nikacheka huku nikijikuta namuuliza "kwa hiyo hapo mwanamgu hauna boxer?" Naye kwa hasira akajibu "unauliza ny€ge kwa mfungwa"

Mchizi alifika akiwa hoi na kuanzia hapo anakuambia hata iwe kwenye daladala root ya Buguruni kwa Kariakoo hali chochote njiani.
Hata Mimi nilikiwepo siku Ile. Wewe uliposhuka jamaa alisimamisha gari akaenda kujisaidia aliporudi nikamwuliza alichotimia kujifutia alisema bukta nikacheka kimoyomoyo. Akasimamimisha basi tena baada ya kubanwa na haja, safari hii alirudi huku amefunga sweta kiunoni nikamwuliza kwa nini amefanya vile akaniambia kuwa ametumia suruali yake kujichambia.

Nilichoka!
 
Back
Top Bottom