secretarybird
JF-Expert Member
- Aug 22, 2024
- 2,998
- 4,948
Ningeua
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Acha upuuzi, wewe kabila gani ili tujue kabila msilokuka safarini.Habari wak
Wasukuma nimewanyooshea mikono kwa kweli.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Aaaah umenikumbusha way back 2020 msimu wa COVID
Nilikuwa na mwanangu tunaenda mkoa, safari ya zaidi ya kilometa 700.
Tumetua tu Moro jamaa akaanza kujikoki kuagiza mazaga mi namcheki tu.
Akaniambia we vipi mbona huagizi nikamjibu mi kwenye safari huwa sili chochote njiani.
Akacheka akasema una tumbo bovu kama la mtoto wa kike..
Na ukumbuke kuwa huo ni usafiri wa umma na pembeni yetu kulikuwa na warembo wakali.
Basi jamaa akatwanga ule msosi wake mara kaagiza juisi, mchizi hakuwa hata na muda wa kuangalia imetengenezwa kwa matunda gani ye alichosema imradi tu iwe ya baridi.
Safari ikaanza.....
Katikati ya safari mara jamaa akaniambia hajiskii vizuri anahisi tumbo lina koroga... namimii nikamtania nikamwambia kama linakoroga jaribu kutia unga.
Basi ile gari kadri lilivyozidi kutembea ndio nilipomuona jamaa hali ikimbadilikia. Nikabaini kuwa ishu imekuwa serious.
Mwisho uzalendo ukamshinda si akaenda hadi mbele kwa suka....suka akamuelewa akasimamisha gari ili jamaa akajisaidie.
Jamaa akaja kuniomba maji yangu yale ambayo nilipewa na wahudumu wa basi kwakua mimi nilijiwekea mazingira ya kutokula njiani kwenye safari so yale maji nilikuwa nayaangalia tu.
Mchizi akachukua maji akashuka kuelekea vichakani. Baada ya muda akarudi na safari ikaendelea.
Tumeenda kama dakika 20 mbele jamaa akamfuata suka tena... Round hii wale masista duu wakasikika wakisema "mweeeh kaka wawatu polee jamani"
Mwana alipofunguliwa tu mlango akatoka nduki....nikajiuliza huyu bwege kaondokaje bila maji??
Aliporudi nikamuambia "we mjinga maji umeishiwa umetumia nini huko?" Akaniambia "nimetumia tiketi kama toilet paper"
Aaah nikishindwa kujiuzia nikacheka...
Tena mbeleni huko hata safari haijachanganya akaomba tena poo gari isimame.
Aliporudi kutoka vichakani nikamumuuliza "na saizi umetumia nini?" Akasema "barakoa"
Safari ikaendelea....tena jamaa kama kawaida yakabipu akashuka.
Aliporudi kabla hata sijamuuliza ametumia nini, yeye mwenyewe akaniambia "nimetumia boxer"
Nikacheka huku nikijikuta namuuliza "kwa hiyo hapo mwanamgu hauna boxer?" Naye kwa hasira akajibu "unauliza ny€ge kwa mfungwa"
Mchizi alifika akiwa hoi na kuanzia hapo anakuambia hata iwe kwenye daladala root ya Buguruni kwa Kariakoo hali chochote njiani.