kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Wanafunzi wetu nchini ni kundi kubwa la wananchi wenye mahitaji maalumu.
Hapa nchini daladala tu ndizo zilizopewa jukumu la kuwasafirisha kwa bei pungufu ya sh. 200. Hii Ni tofauti na biashara nyingine kama ya stationery, uniforms, bodaboda, chips, soda, nk ambao wao huwa wanawauzia wanafunzi kwa bei kamili. Hawana Bei pungufu kwa wanafunzi.
Daladala zinanunua mafuta, spea na kufanya matengenezo kwa bei kamili. Tena huwa zinalimwa faini kwa makosa ya barabarani kila siku bila huruma Wala kujali kazi wanayofanya ya kuwahudumia wanafunzi kwa bei pungufu.
Je, daladala zinapewa motisha gani ili zipende kuwasafirisha wanafunzi wetu kwa bei hiyo bila kinyongo?
Inauma Sana traffic anakotoza faini ya sh. 30,000 wakati ndani umebeba wanafunzi 10 wanaolipa sh 200. Hivi sh. 30000 za traffic utazipata kwa kubeba wanafunzi wangapi? Labda ndiyo maana makondakta wa madaladala hawataki wanafunzi kwenye magari yao.
Itafutwe motisha kwa madaladala itakayowavutia kuwabeba wanafunzi kwa furaha, la sivyo wanafunzi walipe pia Bei kamili Kama wanavyolipa kwenye stationery, uniforms, chips, bodaboda na kwingineko au watafutiwe namna yao ya kusafiri.