Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa mkuu kwanini watoto tuwafanye wawe ni wakuwaonea huruma ndoo wafike shule? Je kama wote madereva wakiona na makonda wakiona hakuna haja ya kuwaonea huruma kwa kuwa wanapata hasara watoto wataendaje shule?
Mtoa mada yupo sahihi kabisaa,serikali hilo ni jukumu lao kwa kushirikiana na wazazi.Mbona kila huduma wanayoitaka popote hakuna punguzo wala huruma ya mtoa service mpaka kwa mwenye daladala ndoo limuangukie yeye wakati nae anafanya biashara kama wengne.
Unataka kusema mwanafunzi anapoingia kwenye mgahawa atengewe sahani, viti, meza na chakula chao kwa bai pungufu?hii 200 siyo sheria,na wamiliki wa daladala walishaurina wakakubaliana hivi,ndio maana waliambiwa wawe na ile siti yao ya moto juu ya engine...halafu hata ukigoma kuwapakia siyo umevunja sheria,hakuna kesi hapo ni uungwana wako mwenyewe kama hutaki kuwapakia wewe acha...ila kama ukiamua kuwapakia usiwatumie kama excuse ya wewe kuvunja sheria za barabarani
ile ajali ya lucky vicent dereva akijitetea kwamba alikua anawahisha wanafunzi wanakoenda nao utamuelewa?!
Kwani mtu akikosa siti huwa analipa nauli pungufu? Mbona hapo aliposimama mtoto wa shule angepata 600 Kama angesimama mtu mzima? Kwahiyo ukienda bar ukakosa kiti Cha kukaa na ukasimama Bei ya bia inapungua?Mkuu hao wanafunzi wenyewe unaowajungua humu mbona kwenye hizo daladala hawakalii siti zako...wanajisimamia zao na ndio maana wanalipa 200.
Usibadilishe mada Mkuu, hoja hapa Ni Nani awasafirishe wanafunzi kwenda shuleni?.hata hakuna hasara
ndio maana wanasafirishwa kila siku
hoja hapa siyo hasara,ni kutaka kutumia wanafunzi kama kigezo cha kuvunja sheria za barabarani