Kusafirisha wanafunzi ni kazi ya nani?

Mkuu hao wanafunzi wenyewe unaowajungua humu mbona kwenye hizo daladala hawakalii siti zako...wanajisimamia zao na ndio maana wanalipa 200.
 

hata hakuna hasara

ndio maana wanasafirishwa kila siku

hoja hapa siyo hasara,ni kutaka kutumia wanafunzi kama kigezo cha kuvunja sheria za barabarani
 
Unataka kusema mwanafunzi anapoingia kwenye mgahawa atengewe sahani, viti, meza na chakula chao kwa bai pungufu?

Bro, daladala hawana jukumu la kisheria la kugharamia Usafiri wa wanafunzi, walimu na Askari. Bila kupepesa macho Wala kumung'unya maneno Huku ni kuwakandamiza Hawa wafanyabiashara, hii ndio inayosababisha madaladala wavunje sheria ili kufidia hasara za aina hii.
 
Mkuu hao wanafunzi wenyewe unaowajungua humu mbona kwenye hizo daladala hawakalii siti zako...wanajisimamia zao na ndio maana wanalipa 200.
Kwani mtu akikosa siti huwa analipa nauli pungufu? Mbona hapo aliposimama mtoto wa shule angepata 600 Kama angesimama mtu mzima? Kwahiyo ukienda bar ukakosa kiti Cha kukaa na ukasimama Bei ya bia inapungua?
 
hata hakuna hasara

ndio maana wanasafirishwa kila siku

hoja hapa siyo hasara,ni kutaka kutumia wanafunzi kama kigezo cha kuvunja sheria za barabarani
Usibadilishe mada Mkuu, hoja hapa Ni Nani awasafirishe wanafunzi kwenda shuleni?.

Wapo wazazi wenye uwezo wa kunywa bia kila siku, kuendesha magari, kuhonga wanawake na kujenga majumba, lakini na wao wanataka daladala isafirishe watoto wao kwa 200
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…