Kusaga : Tulipopiga wimbo wa Mbosso tuliambiwa tujieleze kwanini tulikuwa hatupigi nyimbo za wasanii wa Wasafi. Uongozi wa WCB uulizwe

Duwh kumbe mzee baba kaoa mtoto kishua
Ila katika macho ya kawaida kabisa huu mgogoro WCB na Clouds inawezekana mwanzoni ulikua kweli ila wazee wa fursa wakaona namna ya kuongeza kipato kupitia hio conflict sasa ni kusaga clouds mama WCB wanaua upinzani kwa kupambana wao kwa wao
 
Aisee!! Kwahiyo na wewe ni nani?! B12, Adam Mchomvu, Kennedy, Seba, au?! Au nawe ni miongoni mwa wale ambao mlilishwa matango pori na Mange kwa kuambiwa Mond anamiliki 2% na kwahiyo hukutaka kusikia ukweli wa yeye kumiliki 45%?!
Mimi ni #babakasema

Sent using my oneplus 7T
 
Kwa nini toka Mwanzo walikuwa hawapigi Nyimbo za Wasanii wa Wasafi.. Angelijibu hilo ingekuwa murua kabisa vinginevyo ni wale wale tu
Mkuu, hili swali aliwahi kuulizwa na alijibu kwamba..... Hakuwahi kufaham kwamba nyimbo za Diamond hazipigwi na Clouds, hivyo alipo amuru zianze kupigwa na wakaanza na nyimbo ya Mboso ndipo uongozi wa Wasafi ulipo waandikia barua ya kujieleza kwamba kwanini Clouds inapiga nyimbo zao...
Hapa nilimuelewa Kusaga kwamba, alitaka kujitoa kwemba yeye hakushiriki kwenye dhambi ya kum maliza Diamond na Wasafi Team (kabla ya Wasafi media). Na sasa anataka kuuaminisha uma kwamba marehem ndio aliye amrisha nyimbo za Diamond zisipigwe Clouds.
Na kwasababu Ruge ni marehem na hawezi kusema tema, basi tutarajie kusikia mengi toka kwa Kusaga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu mgogoro ni ukweli ulikuwepo na upo! Na hata kama wengine walisema ni kiki tu za kuizindua Wasafi Media, lakini gogoro lilikuwepo lakini kimsingi lilikuwa ni gogoro kati ya Ruge na Diamond (lakini kiabiashara zaidi), na ndio maana wala haikushangaza Diamond kutoenda nyumbani kwenye msiba wa Ruge ingawaje hakufanya poa!! Aidha, mwanzoni nadhani hata Joe mwenyewe aliamini hili gogoro "poa tu" kama njia ya ku-boost competition kati ya media mbili ambazo ana mkono lakini kwa sasa sidhani kama bado anaamini hili gogoro ni poa tu! Na akiendelea kuamini hivyo, ni Clouds ndiyo inayoathirika zaidi kuliko Wasafi, hasa baada ya kufariki Mastermind Ruge!
 
usipanic mkuu, mmiliki wa both Clouds and Wasafi amesema yeye hajielezei popote kwa maandishi kuwa kwanini kituo chake kimoja kilikua hakichezi nyimbo za WCB full stop.
 
Mbona hawajampa airtime Qboy msafi, Harmonize au Rich Mavoko ...


Msiyoyajua ni sawa na usiku wa giza...


Au mbona hawawafanyii interview watangazaji wa clouds. Najua utakuwa umeona tatizo lilipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hujafuatilia tu. Qboy msafi wamempa Airtime mara nyingi tu. Hata juzi tu (wiki haijaisha) walimpa interview kwenye Refresh.

Wengine hawataki tu labda, mfano Harmonize aliambiwa aje kwenye festival akajikausha. Hapo hawawezi kulazimisha kama mtu atasema hataki.

Kuna watangazaji wa Clouds wanatamani lakini wanaogopa kuonekana "wasaliti". Ndio maana huwakosi kwenye comments za page za wasafi/wasanii wao.

Tusilolijua ni lipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wale mameneja uswahili mwingi

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa Uswahili wao hapo upo wapi?! Kama ni tuhuma za Clouds kuwabania wasanii ni tuhuma ambazo zipo miaka nenda rudi sasa! Au Uswahili wao ni kutaka Clouds waandike barua waeleze ni kwanini waliacha kupiga hizo nyimbo?! Kama ndivyo, wewe unaona sawa tu Clouds wawe wanaamua wenyewe wakitaka kupiga ngoma za msanii wanapiga, na wasipotaka, wanapiga pini tu bila kutoa maelezo yoyote?! Yaani wawe wanaamua tu watakavyo wao; kwamba sasa hatupigi, na sasa tunapiga!!!
 
Huoni kama ukiwa na kampuni zako mbili zinafanya kazi moja huoni kama ni njia nzuri ya biashara kuzishindanisha, kitu kinachofanywa na A kisifanywe na B. Ili watu waamini kuna shida so zote kwa pamoja zinapata kutrend kwa wakati mmoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tabia ni ngozi mkuu, uswahilini ndipo alipokulia...

Tazama namna anavyohaha hata kwenye mahusiano yake na wanawake, ni image ya kile ako nancho ndani yake
meneja wanapswa kum-shape awe profession,

sasa mameja viazi mbatata kutwa kuchambana mitandaoni sion tofauti yao na Mama yake Diaomond au Juma Lukole.
 
Jamaa ni mfanyabiashara wa kiwango cha juu, anamiliki
*clouds fm
*clouds tv
*clouds plus
*choice fm
*clouds tv RW
*WASAFI media wapo share na mke wake

Huyu jamaa ndio mengi ajaye [emoji91][emoji91]
Mengi ajaye ni mimi mkuu huyo katangulia tu
 
hamna kitu hizo sababu za EFM ulizosema hapo ni story za wanywa kahawa wa kijweni, EATV wengi hawakupeleka kazi zao kwenye tuzo na nyimbo zao zinachezwa.
kubali au kataa ukiwa na mameneja bongolala tegemea migogoro mingi zaidi.
naona unaendekeza ligi kuliko kutaka kujua....kila la heri boss
 
Hayo ni maelezo yako, sio yao wahusika. Haya ndo wengi tupo nayo kichwani ndo maana tunataka wahusika wenyewe waseme. Ninanimani tukiwasikia wenyewe tunaweza kushangaa sana.

Nani alitegemea kama Kusaga atasema WCB ndo wanakataa nyimbo zao zisipigwe hadi wewe unapata nafasi ya kulipinga?? Mi naamini kuna vingine vingi kwa pande zote
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…