Kusaga : Tulipopiga wimbo wa Mbosso tuliambiwa tujieleze kwanini tulikuwa hatupigi nyimbo za wasanii wa Wasafi. Uongozi wa WCB uulizwe

Kusaga : Tulipopiga wimbo wa Mbosso tuliambiwa tujieleze kwanini tulikuwa hatupigi nyimbo za wasanii wa Wasafi. Uongozi wa WCB uulizwe

Uliyosema yote ni kweli lakini pia tusisahau kwamba:-
1. Mke wa Kusaga ni Mwislamu! Na inasemekana Kusaga nae ni Mwislamu (alisilimu kwa ajili ya huyu mwanamke)! So, publicly, usemayo ni kweli lakini unapokuja kwenye sheria za Kiislamu, ndo na mali haviendi pamoja! Kwamba, assume ni kweli 53% ZOTE ni mali ya mke wa Kusaga personally, kwa mujibu wa Sheria za Kiislamu hiyo mali hapo Kusaga hana chake unless mke awe amekufa naye apate urithi!

2. Kwamba umiliki vivuli ni kawaida ni kweli pia lakini pia usisahau kwamba mke wa Kusaga anatoka familia bora, na ndo maana haishangazi kusikia Kusaga alisilimu kwa ajili ya huyo mwanamke! Na kwavile anatoka familia bora, inawezekana ni kweli yeye ni kivuli tu lakini pia inawezekana nae anamiliki kiasi cha hizo hisa!!
Duwh kumbe mzee baba kaoa mtoto kishua
Ila katika macho ya kawaida kabisa huu mgogoro WCB na Clouds inawezekana mwanzoni ulikua kweli ila wazee wa fursa wakaona namna ya kuongeza kipato kupitia hio conflict sasa ni kusaga clouds mama WCB wanaua upinzani kwa kupambana wao kwa wao
 
Aisee!! Kwahiyo na wewe ni nani?! B12, Adam Mchomvu, Kennedy, Seba, au?! Au nawe ni miongoni mwa wale ambao mlilishwa matango pori na Mange kwa kuambiwa Mond anamiliki 2% na kwahiyo hukutaka kusikia ukweli wa yeye kumiliki 45%?!
Mimi ni #babakasema

Sent using my oneplus 7T
 
Kwa nini toka Mwanzo walikuwa hawapigi Nyimbo za Wasanii wa Wasafi.. Angelijibu hilo ingekuwa murua kabisa vinginevyo ni wale wale tu
Mkuu, hili swali aliwahi kuulizwa na alijibu kwamba..... Hakuwahi kufaham kwamba nyimbo za Diamond hazipigwi na Clouds, hivyo alipo amuru zianze kupigwa na wakaanza na nyimbo ya Mboso ndipo uongozi wa Wasafi ulipo waandikia barua ya kujieleza kwamba kwanini Clouds inapiga nyimbo zao...
Hapa nilimuelewa Kusaga kwamba, alitaka kujitoa kwemba yeye hakushiriki kwenye dhambi ya kum maliza Diamond na Wasafi Team (kabla ya Wasafi media). Na sasa anataka kuuaminisha uma kwamba marehem ndio aliye amrisha nyimbo za Diamond zisipigwe Clouds.
Na kwasababu Ruge ni marehem na hawezi kusema tema, basi tutarajie kusikia mengi toka kwa Kusaga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duwh kumbe mzee baba kaoa mtoto kishua
Ila katika macho ya kawaida kabisa huu mgogoro WCB na Clouds inawezekana mwanzoni ulikua kweli ila wazee wa fursa wakaona namna ya kuongeza kipato kupitia hio conflict sasa ni kusaga clouds mama WCB wanaua upinzani kwa kupambana wao kwa wao
Huu mgogoro ni ukweli ulikuwepo na upo! Na hata kama wengine walisema ni kiki tu za kuizindua Wasafi Media, lakini gogoro lilikuwepo lakini kimsingi lilikuwa ni gogoro kati ya Ruge na Diamond (lakini kiabiashara zaidi), na ndio maana wala haikushangaza Diamond kutoenda nyumbani kwenye msiba wa Ruge ingawaje hakufanya poa!! Aidha, mwanzoni nadhani hata Joe mwenyewe aliamini hili gogoro "poa tu" kama njia ya ku-boost competition kati ya media mbili ambazo ana mkono lakini kwa sasa sidhani kama bado anaamini hili gogoro ni poa tu! Na akiendelea kuamini hivyo, ni Clouds ndiyo inayoathirika zaidi kuliko Wasafi, hasa baada ya kufariki Mastermind Ruge!
 
FULL STOP?! Kwani si ni Kusaga mwenyewe ndie alitaka waanze kupiga ngoma za WCB?! Hiyo Full stop hapo haiingii kwa sababu hakuna ambae alienda kumwomba! Nadhani mpo disappointed kuona mtu mnayesema ndie boss wa Diamond lakini kakaziwa kupiga nyimbo za Diamond na wasanii wengine walio chini ya label anayoongoza!! Sidhani kama unaamini Diamond alitaka zipigwe lakini akina Tale ndo wakakaza! Ukiona management ya WCB ilikaza, basi ama ni Diamond mwenyewe ndie alitaka waendelee kukaza hadi wajieleze au alibariki!!!
usipanic mkuu, mmiliki wa both Clouds and Wasafi amesema yeye hajielezei popote kwa maandishi kuwa kwanini kituo chake kimoja kilikua hakichezi nyimbo za WCB full stop.
 
Mbona hawajampa airtime Qboy msafi, Harmonize au Rich Mavoko ...


Msiyoyajua ni sawa na usiku wa giza...


Au mbona hawawafanyii interview watangazaji wa clouds. Najua utakuwa umeona tatizo lilipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hujafuatilia tu. Qboy msafi wamempa Airtime mara nyingi tu. Hata juzi tu (wiki haijaisha) walimpa interview kwenye Refresh.

Wengine hawataki tu labda, mfano Harmonize aliambiwa aje kwenye festival akajikausha. Hapo hawawezi kulazimisha kama mtu atasema hataki.

Kuna watangazaji wa Clouds wanatamani lakini wanaogopa kuonekana "wasaliti". Ndio maana huwakosi kwenye comments za page za wasafi/wasanii wao.

Tusilolijua ni lipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wale mameneja uswahili mwingi

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa Uswahili wao hapo upo wapi?! Kama ni tuhuma za Clouds kuwabania wasanii ni tuhuma ambazo zipo miaka nenda rudi sasa! Au Uswahili wao ni kutaka Clouds waandike barua waeleze ni kwanini waliacha kupiga hizo nyimbo?! Kama ndivyo, wewe unaona sawa tu Clouds wawe wanaamua wenyewe wakitaka kupiga ngoma za msanii wanapiga, na wasipotaka, wanapiga pini tu bila kutoa maelezo yoyote?! Yaani wawe wanaamua tu watakavyo wao; kwamba sasa hatupigi, na sasa tunapiga!!!
 
Wasafi Media iwe ni project ya Joe au isiwe, jamaa wanajitahidi kuwa tofauti sana kwenye hii industry.

Mfano maswali waliyomuuliza huyu boss ni yale yale ambayo yamekuwa debate mtaani.

Pia hawana noma kumpa airtime mtu yoyote hata kama anawadiss. Mfano Carry Mastory, Ney, TID (zamani) na wengine wengi. Naonaga wanapewa interview kabisa kiroho safi.

Hao Clouds sasa. Wakiwa na bifu na mtu au ukiwasema vibaya mpaka mtoto wa chekechea atajua. Mikausho mikali. Mfano hawawezi kabisa kumpa nafasi Dudubaya hata iweje kwa sababu jamaa huwa anawadiss kila siku. Angekuwa anawadiss Wasafi wangesema nae tu.

Wasafi wanajua business na kuoperate kama urban radio/tv.

Kudos!
Huoni kama ukiwa na kampuni zako mbili zinafanya kazi moja huoni kama ni njia nzuri ya biashara kuzishindanisha, kitu kinachofanywa na A kisifanywe na B. Ili watu waamini kuna shida so zote kwa pamoja zinapata kutrend kwa wakati mmoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tabia ni ngozi mkuu, uswahilini ndipo alipokulia...

Tazama namna anavyohaha hata kwenye mahusiano yake na wanawake, ni image ya kile ako nancho ndani yake
meneja wanapswa kum-shape awe profession,

sasa mameja viazi mbatata kutwa kuchambana mitandaoni sion tofauti yao na Mama yake Diaomond au Juma Lukole.
 
Jamaa ni mfanyabiashara wa kiwango cha juu, anamiliki
*clouds fm
*clouds tv
*clouds plus
*choice fm
*clouds tv RW
*WASAFI media wapo share na mke wake

Huyu jamaa ndio mengi ajaye [emoji91][emoji91]
Mengi ajaye ni mimi mkuu huyo katangulia tu
 
hamna kitu hizo sababu za EFM ulizosema hapo ni story za wanywa kahawa wa kijweni, EATV wengi hawakupeleka kazi zao kwenye tuzo na nyimbo zao zinachezwa.
kubali au kataa ukiwa na mameneja bongolala tegemea migogoro mingi zaidi.
naona unaendekeza ligi kuliko kutaka kujua....kila la heri boss
 
Hayo ni maelezo yako, sio yao wahusika. Haya ndo wengi tupo nayo kichwani ndo maana tunataka wahusika wenyewe waseme. Ninanimani tukiwasikia wenyewe tunaweza kushangaa sana.

Nani alitegemea kama Kusaga atasema WCB ndo wanakataa nyimbo zao zisipigwe hadi wewe unapata nafasi ya kulipinga?? Mi naamini kuna vingine vingi kwa pande zote
Hilo hawezi jibu.Lkn walikataa kupiga nyimbo za wasanii wengi akina Suma G,Mapacha,Lady Jay Dee,Rama Dee,Wagosi wa Kaya nk.Ila kwa WCB wameshindwa sababu walichotarajia,hakikuwa kama walivyotegemea kwa wasanii wengine waliowabania.

Nakumbuka Mchomvu siku moja anahojiwa akasema management ya CMG imesema isipige nyimbo za WCB.

Kwa hiyo jibu simple tu hata Management ya WCB imeamua nyimbo zao zisipigwe CMG,wao waliamua huko nyuma na WCB wameamua baada kutusua bila wao.Wameanza wenzao wakamaliza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom