Kusaga : Tulipopiga wimbo wa Mbosso tuliambiwa tujieleze kwanini tulikuwa hatupigi nyimbo za wasanii wa Wasafi. Uongozi wa WCB uulizwe

Kusaga : Tulipopiga wimbo wa Mbosso tuliambiwa tujieleze kwanini tulikuwa hatupigi nyimbo za wasanii wa Wasafi. Uongozi wa WCB uulizwe

Akizipatanisha hawezi kuwapata watu wasiofikiri ambao ndio wengi nchi hii.Sijui kuhusu wewe mkuu,ila ujue wenzio wako mbali sana kibiashara.
Ni sawa na kusema uwapatanishe wapenzi wa yanga na Simba ili wawe kitu kimoja,unadhani watafanyaje biashara?

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] naona umeamua kumtukana mwamba kiaina

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wana JF Wasalaam.

Leo kupitia Wasafi TV kwenye kipindi cha Bar tender alikuwa ana hojiwa mkurugenzi mkuu wa Clouds Media JOSEPH KUSAGA.

Katika mahojiano yake kati ya maswali aliyo ulizwa ni kuhusu kutopigwa nyimbo za wasanii wa WCB kwenye vyombo vyake vya Habari na Burudani.

Kusaga ameweka wazi kabisa kabisa wao kama taasisi na yeye akiwa kama kiongozi alitoa maamuzi kabisa kila wimbo wa kila msanii upigwe bila kuangalia ni nani lili mradi ni mziki mzuri na una stahili Platform.

Clouds FM kama Media walikubaliana na wakaanza kwa kupiga wimbo wa Mbosso lakini cha kushangaza waliandikiwa barua na Uongozi wa WCB wajieleze kwanini wamepiga wimbo husika na kwanini huko nyuma wamekuwa hawpigi nyimbo za wasanii wa WCB.

Hivyo, Kusaga amesema kuwa yeye hawezi kujieleza kwa Uongozi wa WCB kuwa kwanini amepiga nyimbo zao hivyo akaona ni bora waache kuliko kulazimisha kupiga nyimbo za watu ambao hawataki nyimbo zao zipigwe na Kusaga ameweka wazi kuwa waulizwe Uongozi wa Wasafi na sio wasanii wa Wasafi.

Kusaga amesema hana tatizo kabisa na wasanii wa Wasafi lakini hawawezi kulazimisha kupiga nyimbo zao kama hawataki zipigwe.

Ni kweli uongozi wa WCB umekataza nyimbo zao zisipigwe Clouds FM? Mbona Diamond amekuwa akilalamika kuwa nyimbo zake azipigwi baadhi ya radi huku wao ndio wamekataza?

Uongozi wa WCB umemficha Diamond ukweli?

Kwanini Diamond na Uongozi wake wana wasingizia Clouds Media kiasi hiki?

Diamond ana pelekwa shimoni na Babu Tale na Salam?

Nini Tatizo?
 
Back
Top Bottom