Diamond ana hisa 45% halafu unasema Diamond katoa jina, Kusaga ndo katoa mzigo?! Acheni masihara nyie watu! Halafu kiroja kingine ni hapo unaposema Kusaga ndie kaamua Wasafi miziki yao isipigwe kwenye baadhi ya radio wakati Kusaga mwenyewe wakati anahojiwa kasema wazi hana mamlaka yoyote juu ya WCB Label. Sasa how come tena awe na ubavu wa kuwapangia nyimbo zao zipige wapi na wapi zisipigwe?! Na kama aliamua zisipigwe, mbona baada ya uongozi wa WCB kugoma nyimbo zao mbona hajashinikiza ikiwa anao huo ubavu?!
The problem nyie watu bado hamtaki kukubali kwamba Diamond amepiga hatua kubwa sana, na matokeo yake ndo hayo! Kila kubwa linalofanyika, mnaamimi sio lake kwa saababu you don't believe ni SELF MADE hususani kutoka kwa mtu kama Diamond ambae hata shule yake yenyewe ndo hivyo tena!!!
Mwaka 2016, Diamond aliwahi kuhojiwa na kusema amekataa kusainiwa na Roc Nation ya Jay Z! Pitia huo uzi uone watu walivyokuwa wanamkejeli na kumwita muongo mtafuta kiki kwa maana hakuwa na ubavu wa kuwatolea nje ya Roc Nation! Na hao waliona Diamond alikuwa anatafuta kiki kwa sababu walikuwa hawataki kukubali kwamba jamaa alishapiga hatua kubwa!
Wote hao wakaja kuzibwa midomo baada ya hatimae Diamond kusainiwa na Universal! Na hata ukiangalia sababu alizotoa Diamond kwanini alikataa kusainiwa na Roc Nation, utaona alikuwa sahihi manake mkataba na Universal ulikuwa tofauti!!