Kusaga: Tunakoelekea radio nyingi zitafungwa

Kusaga: Tunakoelekea radio nyingi zitafungwa

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group anabainisha kuwa vyombo vya habari vya asili vinakabiliwa na hatari kubwa ya kufungwa kutokana na mabadiliko ya teknolojia.

Anaeleza kuwa mitandao ya kijamii imepokonya soko la matangazo, hali inayofanya redio na televisheni nyingi kushindwa hata kumudu gharama za uendeshaji. Ili kunusuru sekta hii, anapendekeza kuwa serikali itoe ruzuku au msaada maalumu kama inavyofanyika katika nchi nyingine zilizoendelea.

Tulipofika sasa kwenye upande wa traditional media, redo nyingi sana zitafungwa kabisa kabisa."

Clouds unaweza ukasema imejitahidi, hizo media nyingine naona ya huruma sana... yaani hata tu meetend zile za kawaida za kila siku wengine hata umeme hawana mara nyingine."


​
 
Podcast zinakuja kwa kasi,tena kama hivi vipindi vya michezo makelele mengi hawazungumzii mpira bali siasa za mpira. Siku maveteran wa zamani wakijitambua na kuanzisha Podcast zao zitakazo chambua mpira na kuzungumzia visa na matukio wakati wakiwa wanacheza mpira,vipindi vyote vya michezo chali.

Huwaga na watizamaga Rio Ferdinand,Gary Lineker, Ian Wright, Keane, Rooney, Micah nk huwaga wanazungumzia mpira, wanauchambua mpira,halafu wanazungumzia moment na matukio ya zamani,sio hivyo hata hizi baadhi Podcast za wanajeshi wa US wanapodcast zao kule ndipo wanazungumza vitu vyingi na reality na si haya maigizo ya CNN,BBC nk.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group anabainisha kuwa vyombo vya habari vya asili vinakabiliwa na hatari kubwa ya kufungwa kutokana na mabadiliko ya teknolojia.

Anaeleza kuwa mitandao ya kijamii imepokonya soko la matangazo, hali inayofanya redio na televisheni nyingi kushindwa hata kumudu gharama za uendeshaji. Ili kunusuru sekta hii, anapendekeza kuwa serikali itoe ruzuku au msaada maalumu kama inavyofanyika katika nchi nyingine zilizoendelea.

Tulipofika sasa kwenye upande wa traditional media, redo nyingi sana zitafungwa kabisa kabisa."

Clouds unaweza ukasema imejitahidi, hizo media nyingine naona ya huruma sana... yaani hata tu meetend zile za kawaida za kila siku wengine hata umeme hawana mara nyingine."

Mnashindwa kwenda na wakati? Kama online media ndiyo mpango wa sasa what are you waiting for? Don't be rigid, flexibility is the only option.
 
Watu wamekamata masafa mzee , lazima waone ulaji unakatika
Waingie kwenye mfumo, wakati wanaendelea na mfumo wao wa zamani waanze kuhamia mdogo mdogo kwenye social media. Akina shigongo walisoma mchezo mapema akahamia taratibu kwenye social media ikazaliwa Global Tv. Leo magazeti hayana soko tena, watu wapo kwenye mitandao ya kijamii.
 
Media haitokufa kirahisi ila itazidi kushuka ushawishi wake kama serikali itaendelea kuongeza restrictions.

Kama watu wanapata balanced meal kwenye social media. Hakuna atakaesikiliza TBC ikiwa haitoi uchambuzi makini kutoka kwa waandishi wa habari wenye ITHIBATI

Kama watu wanawapenda wachambuzi ama creatives wa social media kwa personality na ubunifu wao. Usitegemee watampenda mtangazaji kwa sababu ana ithibati

Yote kwa Yote. Radio at least zina maisha marefu zaidi ila TV zinatia huruma
 
Sababu kubwa ni uchawa.
Muda wote michezo na kusifia chura kiziwi muuaji
Hata wakipewa ruzuku haitasaidia. Kushindana na haya mabadiliko ya teknolojia haiwezekani. Wao wawekeze zaidi online maana hakuna namna kwa sasa. Hata huko Ulaya tayari MTV imefunga vituo vyake.
 
Back
Top Bottom