Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mnashindwa kwenda na wakati? Kama online media ndiyo mpango wa sasa what are you waiting for? Don't be rigid, flexibility is the only option.Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group anabainisha kuwa vyombo vya habari vya asili vinakabiliwa na hatari kubwa ya kufungwa kutokana na mabadiliko ya teknolojia.
Anaeleza kuwa mitandao ya kijamii imepokonya soko la matangazo, hali inayofanya redio na televisheni nyingi kushindwa hata kumudu gharama za uendeshaji. Ili kunusuru sekta hii, anapendekeza kuwa serikali itoe ruzuku au msaada maalumu kama inavyofanyika katika nchi nyingine zilizoendelea.
Tulipofika sasa kwenye upande wa traditional media, redo nyingi sana zitafungwa kabisa kabisa."
Clouds unaweza ukasema imejitahidi, hizo media nyingine naona ya huruma sana... yaani hata tu meetend zile za kawaida za kila siku wengine hata umeme hawana mara nyingine."
Watu wamekamata masafa mzee , lazima waone ulaji unakatikaHizo radio kwanini zisihamie kwenye teknolojia mpya, kwani lazima kutembea kwenye njia hiyohiyo?
Naunga mkono hoja hasa radio free niliiacha kusikiliza kabisa muda wote samuya samuya.Aseme ukweli na uchawa nao umechangia wasikilizaji, wasomaji na watazamaji wa hizo media nao kuzipuuza.
Nilitaka kusema hiviAseme ukweli na uchawa nao umechangia wasikilizaji, wasomaji na watazamaji wa hizo media nao kuzipuuza.
Waingie kwenye mfumo, wakati wanaendelea na mfumo wao wa zamani waanze kuhamia mdogo mdogo kwenye social media. Akina shigongo walisoma mchezo mapema akahamia taratibu kwenye social media ikazaliwa Global Tv. Leo magazeti hayana soko tena, watu wapo kwenye mitandao ya kijamii.Watu wamekamata masafa mzee , lazima waone ulaji unakatika
Hata wakipewa ruzuku haitasaidia. Kushindana na haya mabadiliko ya teknolojia haiwezekani. Wao wawekeze zaidi online maana hakuna namna kwa sasa. Hata huko Ulaya tayari MTV imefunga vituo vyake.
😂😂😂Tbc inapata kila kitu ila haina wasikilizaji.Ni mjinga pekee ambaye atashindwa kuenenda na mabadiliko yaliyopo kwa kutegemea muujiza wa kupata ruzuku kutoka kwenye serikali hii ya ccm