Kusahau kabisa ndoto unazoota usiku inasababishwa na nini?

Kusahau kabisa ndoto unazoota usiku inasababishwa na nini?

simakoku

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
587
Reaction score
675
Binafsi nina tatizo la kusahau kabisa ndoto ninazoota, pindi nikiamka. Naliita tatizo kwasababu huko nyuma nilikuwa naota na nakumbuka kila kitu na naweza kumsimulia mtu nimeota nini.

Lakini ghafla nikaanza kusahau kabisa. Hata kama nikishtuka katikati ya usiku nikijaribu kukumbuka hivi nilikuwa naota nini, yaani kumbukumbu haziji kabisa.

Huwa naota na nakumbuka kabisa kuwa nimeota, ila sasa kukumbuka nimeota nini ndio shida. Siipendi hali hii maana huwa najitahidi kweli kukumbuka lakini wapi, sasa sijui tatizo ni nini, maana najua kuna ndoto ambazo ni ujumbe fulani mtu unakuwa unapewa.
 
Hili tatizo ninalo sana

Lakini nilifuatilia nikagundua siku za nyuma nilikuwa nakumbuka sababu sikuwa na mambo mengi, jinsi umri unavyokwenda na majukumu kuongezeka uwezo wa kukumbuka mambo unapungua
 
Utakuwa na tundu kwenye ubongo ambalo kitaalam linaitwa burr hole ambalo pamoja na mambo mengine hutumika kupunguza pressure kwenye ubongo hasa pale ubongo unapokuwa unachemka! Tafuta fundi wire ring ambaye ni mtaalamu wa vichwa ili akague kama mpangilio wa fuse kichwani umekaa poa ili kukurudisha kwenye mfumo wako wa kumbukumbu kama awali!
 
Jaribu kufanya meditation

Kwa kawaida hutakiwi tu kukumbuka bali unatakiwa uende sawa na ndoto zako (sio ndoto za kitanda) yaani unavyoota unatakiwa uwe aware.

Hapo sasa utaweza kwenda sawa na ndoto yako huitaji kumsimulia mtu vitendo vitaonekana na mabadiliko pia.

Iyo ndoto ya kuwasimulia watu umeokota bulungutu la pesa alafu huzioni iyo ni ndoto ya kitanda.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata ya kugegeda unasahu, pamoja na kuona matokeo kwenye boxa. 😎
 
Usiumize kichwa chako, ndoto ni ndoto tu.. haina maana yoyote na haikusaidii chochote...

Sent using Jamii Forums mobile app
Si kweli. Kuna ndoto zingine ukweli wake uwa unadhihirika baadae kwa matukio yanayohusiana na ndoto hizo. Pia ndoto au chochote kinachosahaulika kirahisi uwa ni ile/ kile kisichokuwa na umuhimu wowote.

Hivyo ndoto yenye umuhimu si rahisi kuisahau yote sana sana hautaweza kuelezea kwa ufasaha mfululizo wa matukio yote uliyoyaona ndotoni lakini ujumbe wake wa jumla utabaki ukiukumbuka.
 
Back
Top Bottom