Kusahau kabisa ndoto unazoota usiku inasababishwa na nini?

Mi sio jinsia nayovaa boxa mkuu.
Ooohhh.....lakini pia huwa sielewi huwa kuna nguvu gani, maana kweli unaweza sahau ndoto, lakini likatokea tukio fulani ghafla ndoto yote inakuja live.
 
Nilivyokuwa mdogo niliwahi kuota nimenunuliwa viatu vipya, nilivyoamka basi nikaanza kuvitafuta nyumba nzima, na nilipovikosa nikaanza kuwadai nyumbani wanipe viatu vyangu vipya kama wameviweka mahali, ilikuwa balaa..
 
Wengi tuna shida hii lakini mimi naona ukiona unasahau ndoto ulizoota jua kuwa umri umesonga kwa hiyo ndugu hiyo ni dalili tosha ya kuwa uzee unakunyemelea!
 
Hali hii hutokea hasa umri unapokwenda juu zaidi >30. Mtu huota ndoto na kuzikumbuka anapokuwa na usingizi mzito. Hali hii hupungua na umri. Pia hali yako ya kiroho inachangia. Wakati mwingine unaweza ukasahaulishwa ndoto ya kichawi ili usichukue hatua. Kwa ujumla sio vizuri unapokuwa unaota ndoto na kusahau. Ndoto hutumiwa sana na ulimwengu wa giza na huweza kuingilia kumbukumbu yako ili usishtuke kwamba kuna kitu kinaendelea. Kabla na baada ya kuamka sali vizuri kuweka ulinzi dhidi ya mashambulio ya shetani kupitia ndoto.
 
Mkuu lala chali utakumbuka tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wengi tuna shida hii lakini mimi naona ukiona unasahau ndoto ulizoota jua kuwa umri umesonga kwa hiyo ndugu hiyo ni dalili tosha ya kuwa uzee unakunyemelea!
Kiumri mtu anaweza kuzeeka lakini roho ya mtu haizeeki, ukisahau ndoto uliyoota ujue kuna shida ya kiroho mahali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…