Kusajili dini ni kinyume cha Katiba ya nchi kifungu namba 19

Kusajili dini ni kinyume cha Katiba ya nchi kifungu namba 19

Hapo kwenye (2) kifungu kinaanza na maneno haya; "Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya Muungano,.....

Hili suala la kusajili Dini/Makanisa si ndo sheria zenyewe za Jamhuri ya Muungano? Maana naona hapo Katiba inataja kabisa kuwa bila kuathiri.

I stand to be corrected.
 
Hapo kwenye (2) kifungu kinaanza na maneno haya; "Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya Muungano,.....

Hili suala la kusajili Dini/Makanisa si ndo sheria zenyewe za Jamhuri ya Muungano? Maana naona hapo Katiba inataja kabisa kuwa bila kuathiri.

I stand to be corrected.
Sheria zingine zinabaki pale pale

Mfano mchungaji au padre jambazi kaficha bunduki yake kanisani polisi huwezi wazuia kuingia kusearch hiyo bunduki kuwa wanaingilia uhuru wa kuabudu!!!

Kuna kipindi waumini wa kiislamu walikuwa wakitwangana wao kwa wao msikitini polisi ikabidi waingie na viatu kuamua na kuwakamata watwanganaji ili kurejesha amani wasiuane.Waliingia wakiwa na viatu vyao vya kipolisi wakati msikitini watu hawaingii na viatu .Hapo huwezi sema polisi waliingilia uhuru wa kuabudu ni ruksa!!! ndio maana yake hasa ya kusema bila kuathiri shreia zingine.
 
Serikali haina mamlaka ya kusajili dini ni kinyume cha katiba ya nchi kifungu cha 19 hiki hapa nanukuu

19.-(1) Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani
na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu
kubadilisha dini au imani yake.
(2) Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya
Muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza
dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu ya binafsi, na
shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya
shughuli za mamlaka ya nchi



Mfano Hii dini serikali itataka kuisajili? au inamlenga nani Kwenye huo usajili?

Kwenye siasa ukiamua kufanya maamuzi ya kijinga makusudi, tena hadharani; utajikuta unalazimika kutetea uamuzi wako kwa nguvu; badala ya hoja.

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu Mnatuchanganya
Mara Taasisi,Mara dhehebu,
Wanasajili nini?
Dhehebu ni Kama Roman catholic,Lutheran,Sabatho nk nk
Taasisi ni kama Zipi?
Nini Kitasajiliwa naomba mtoe na Mifano tuelewe!
Cc: YEHODAYA

Usichanganyikiwe bro. Kuna pindi zingine hapa JF watu huandika vitu ambavyo hawavielewi. Wazia taasisi au dini ziwepo bila kuzisajili na kuziwekea miongozo. Hali ingekuwaje? Tuje labda vyama vya siasa navyo visisimamiwe viendeshwe bila usajili, uje makampuni, uje magari, n.k nk nk, hii nchi itakuwaje?
Wanachosisitiza ni uhuru, lkn uhuru usio na mipaka ni vurugu. Embu chukulia kwa siku moja tu kusiwe na sheria ya USALAMA barabarani. Yaani tuamke tu siku moja, anayetaka kukimbiza kwenye 50 akimbize tu, anayetaka ku overtake kwenye kona tuksa, anayetaka kupita kulia badala ya kushoto na fuleshi tu.😁😁😀 pata picha barabara itakuwaje!!!!?
 
Back
Top Bottom