Kusema hakuna mtu wa kuvaa viatu vya Urais baada ya Dkt. Magufuli ni kukosa akili

Huyu wa sasa angekuwa na akili angesota kwenye ualimu huko kijijini miaka nenda miaka rudi? Bora wale vijana waliofukuzwa UDOM kuliko huyu
 
Ndani ya ccm na hata nje ya ccm kwa kizazi hiki sioni wa kumfikia magufuli hata robo utendaji wake.
Kwa haraka haraka toka baba wa Taifa nyerere aondoke madarakani 1984 nchi yetu haikuwahi kupata mzalendo kama magufuli wengi walijali maslahi yao ila magufuli kajilipua kuvaa viatu vya nyerere

Tukimpoteza magufuli itatuchikua miaka 30 tena kumpata magufuli mpya

Ndio maana tunakuomba magufuli ukae madarakani mpaka 2034 Ili uinyoshe nchi

Nchi ilishaoza hii ilishakua shamba la bibi

Magufuli tunakuomba kaa madarakani walau hata 2034 utupeleke tuwe kama Thailand

Hizi kelele za wachache mtandaoni ni za vijana wanaotumiwa na mafisadi kukuchafua zikuumize kichwa mzee wetu

Mungu akupe nguvu katika uongozi wako
 
Sema tu Covid 19 haiko fair
 
Chama cha low IQ kimeamka..
 
Kila zama na kitabu chake, huyu magufuli wa sasa hatakua wa 2026 kuna mambo mengi yatabadilika hata kama atamzidi Idi Amin Dada kwa udikteta hatakua alivyo sasa.

kipindi hicho vijana wasomi ambao hana ndoto ya kuwasaidia kwa kuuwa sector binafsi ambayo ndiyo uti wa mgongo katika Ajira watakua wengi kiasi cha kutosha kumuangusha kwa aibu.

Viongozi wengi atakua amewafukuza kazi na watakua na hasira nae hivyo watatengeneza uasi wa chini chini na kumdhoofisha katika uongozi jeshi ambalo analipa ulaji ili kujijengea mkono wa chuma watachoka kumlinda mtu moja huku wakiona watoto wa ndugu zao wakiangaika kwa kuwaomba misaada.

Kama magufuli anataka aibu ya karne akubali huo ujinga.
 


Mkuu, ni wachache sana watakao kuelewa.

Shida ni misingi mibaya ya elimu ya kujitambua iliyowekwa na "baba wa taifa"--- Watz ni waoga na hutujitambui, elimu ilikuwa ni privilege na sio right ya mtu hivyo Watz wengi bado ni mbumbumbu kujua mambo ya nchi yao na haki zao wengi ni bendera fuata upepo.
 
Kwa haraka haraka wanao pendekeza wananguvu, lakini yawezekana muda ukasema vinginevyo. Ila tukibeza kazi yake ataongezewa muda.

Tukikubali kazi yake kuwa ni nzuri ataondoka muda ukifika. Lazima tukubali na tumshukuru vingenevyo atakuwepo. He will have nothing more to prove.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…