Kusema hakuna mtu wa kuvaa viatu vya Urais baada ya Dkt. Magufuli ni kukosa akili

Kusema hakuna mtu wa kuvaa viatu vya Urais baada ya Dkt. Magufuli ni kukosa akili

Kuna watu wataleta nyuzi za kishamba sana eti haoni mtu wa kuvaa viatu vya Urais baada ya miaka 5 au 10 ya Dr Magufuli. Sisemei Dr Magufuli hajafanya kazi , la hasha, Kajitahidi na kachapa kazi ila Tanzania ina watu mil 58 , naamini kuna watu Zaidi ya mil 1 wanaoweza kufanya vizuri kwenye kiti cha Urais Zaidi ya Dr Magufuli.

Wengi wanaomzunguzia Dr Magufuli kama mungu ni washamba Fulani ambao hawana exposure ya kutosha na elimu yao ni ya chini sana. Lakini tatizo lao kubwa ni IQ yao kuwa chini sana below the bottom line .

Tanzania kukosa viongozi wazuri ni matokeo ya Katiba mbovu na matumizi mabaya ya vyombo vya dola ambavyo vinatumika kuua Demokrasia ambayo ndio njia sahihi ya kuwaona viongozi wazuri. Wengi wanahofu hata wamekata tamaa ya siasa kwa sababu ya vitisho vya wenye mamlaka wasio jali haki za binadamu hata ndani ya chama cha CCM.

Hata Nyerere aliimbiwa nyimbo kama hizi na maadhi ya wapumbavu na wasio na akili lakini mwishoni mwenyewe Nyerere akaona hatoshi. Laiti angekubali vichwa kama kina Kambona leo Tanzania ingekua moja ya nchi zenye uchumi bora na Imara Africa Zaidi ya Nigeria na South Africa.

Ethiopia imetawaliwa na Mawaziri wakuu wawili wakatili wasio jail haki za binadamu ,wao waliamini katika maendeleo ya mkono wa chuma nao si wengine ni Hailemariam Desalegn na Meles Zenawi.

Katika vipindi vyao haki za buinadamu zilizorota sana, waandishi wa Habari wengi walifungwa na kuteswa , wananchi wengi walikimbia nchi yao , wapinzania wangi wakaishia gerezani . Pamoja na maendeleo waliyo yaleta kama barabara, Ethiopia airlines, etc mwisho chama chao kikakiri hawahitaji viongozi wakatili wanao angalia maenmdeleo bila haki za binadamu , wanahitaji demokrasia, uhuru wa kuchagua, uhuru wa kuongea na kusikilizwa etc.

Hawa wote waliimbiwa manyimbo ya kipumbavu kama wanayo imba kima kessy, msukuma, lijuakali,Sanga na wapumbavu wengine bungeni wasio jitambua kutokana na IQ zao kuwa chini sana.

Baada yah hapo chama kikamleta kijana msomi na mwelevu Abiy Ahmed ambaye ameleta neema kwa watu wa Ethiopia, maendeleo anasimamia, uchumi unaenda kwa kasi, hata kisasi na mtu, vyama vya siasa vinafanya siasa, wandishi wanaandika mambo yao kwa uhuru, walio kimbia nchi yao wamerudi,mahakama zinafanya kazi zao kwa uhuru, vyombo vya dola vinasimamia haki sawasawa bila kumwonea mtu etc.

Ni lazima watanzania tuendelee kuzipuuza sauti za hawa wachumia tumbo, wasio na akili. Tanzania inauwezo wa kutoa viongozi ambao wanaweza kubadilisha nchi hii ndani ya miaka michache, ikawa nchi nzuri, yenye uhuru, yenye uchumi imara, yenye kujali haki za binadamu, yenye demokrasia etc.

Kumbuka: Wale waliokua nondo Olevel wakiamini wao ndio wenye akili Tanzania, Siku wameenda shule kama Ilboru , Mzumbe Kibaha, wakashangaa wanashika mkia.

Pongezi sana kwa Dr Magufuli na Marais wote waliopita,
Dr Magufuli fanya kazi yako ,sepaaaaa.
Wapo wengi wenye maono na Taifa hili.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu wabariki watanzania wote Mil 58.
YES Banaaa!!!
 
Mwandishi ndiyo mashamba na limbukeni wa kutupwa!!

Ijapokuwa kuna vitu vingi vya maana katika andiko lako, Jambo moja tu ambalo linalokufanya kuonekane wewe ni mshamba na mjinga,

Nikikuuliza kwamba, Unatumia vigezo gani vya kumfananisha Magufuli ambaye ni Binadamu awe kama Mungu?

Pengine utasema ni zile sifa anazopewa za utendaji na usimamizi wake!!

Lakini Je, kuwa mtu makini na kusimamia mambo yako Kwa makini na ukasifiwa kwa umaskini wako, kunakosa gani kwako binafsi na Kwa wasifiaji?

Mimi ni mfanyabiashara, Kunakosa gani kutaka Viwango vya Mo kwamba nami siku moja ningependa kufika huko?

Au Kunakosa gani kumsifia Mo jinsi alivyomtafiti mzuuri ktk masoko na pengine kusema huwezi kumfananisha na wengine?

Na ieleweke, Mungu alituumba kila mtu awe wa tofauti na Viwango vya tofauti, na lazima hata darasani awepo mtu wa kushika no moja darasani ingawa walimu ni walewale na masomo ni yaleyale, Darasa ni lilelile, masomo ni yaleyale, walimu ni walewale, Ila kuna mwanafunzi atatoka kapa!

Kinachokusumbua ni wivu wa kike, fanya vema na wewe utapata kibali machoni pa watu, na usipende kutafsri kupendwa na kusifiwa eti ni kama kufananisha na mtu na Viwango vya Uungu!
 
Kwangu sio ujinga ni upunguani! Vijana wa tz tukatae kuongozwa na mawazo ya kizee km ya kessy!
 
Japo sijasoma hilo gazeti, ila nilitarajia kuona list ya majina angalau mawili ya wanaoweza kumpita magufuli kwa utendaji wake.

Au ungetaja hata lwa kwako.
 
"Lakini tatizo lao kubwa ni IQ yao kuwa chini sana below the bottom line" .
Wapumbavu,Hawajitambuwi,Wapo wapo tu.
 
Hii inamaanisha mambo yafuatayo:
1. CCM imeshindwa kuwatengeneza viongozi wapya ktk kipindi chote cha utawala wao kama wanavyokuwa wakijigamba; maana hata huyu wanayemsifia anasema alikuwa ana 'beep' tu, kwa maneno mengine hakuandaliwa wala siyo zao la mfumo wa chama.
2. Kati ya wanachama zaidi ya mil 12 wanaotajwa kuwa ni wa CCM hayupo mwenye akili na uwezo wala maono bora juu ya nchi hii zaidi ya Mwenyekiti wao
3. Wanaotetea hoja hiyo, hawaelewi maana ya mfumo wa Democracy; kwamba kama ndani ya chama chao hawajaona mwenye akili anayefaa kupokea kijiti basi waruhusu vyama vingine viwasimamishe wenye akili tuwapime kwa miaka mitano iliyopangwa.
4. Mwisho, hawaamini ktk taaluma, vipawa, uwezo na dhamira njema walizonazo wananchi zaidi ya mil 50 ambao wanaweza kuleta mageuzi makubwa zaidi ya haya yanayoonekana sasa, ya kiuchumi, kisiasa na kijamii.
 
Hii inamaanisha mambo yafuatayo:
1. CCM imeshindwa kuwatengeneza viongozi wapya ktk kipindi chote cha utawala wao kama wanavyokuwa wakijigamba; maana hata huyu wanayemsifia anasema alikuwa ana 'beep' tu, kwa maneno mengine hakuandaliwa wala siyo zao la mfumo wa chama.
2. Kati ya wanachama zaidi ya mil 12 wanaotajwa kuwa ni wa CCM hayupo mwenye akili na uwezo wala maono bora juu ya nchi hii zaidi ya Mwenyekiti wao
3. Wanaotetea hoja hiyo, hawaelewi maana ya mfumo wa Democracy; kwamba kama ndani ya chama chao hawajaona mwenye akili anayefaa kupokea kijiti basi waruhusu vyama vingine viwasimamishe wenye akili tuwapime kwa miaka mitano iliyopangwa.
4. Mwisho, hawaamini ktk taaluma, vipawa, uwezo na dhamira njema walizonazo wananchi zaidi ya mil 50 ambao wanaweza kuleta mageuzi makubwa zaidi ya haya yanayoonekana sasa, ya kiuchumi, kisiasa na kijamii.
watanzania tumechoshwa,kwa kifupi watanzania hawaitaji ccm Wala chadema Wala chama chochote, wanahitaji serikali ya magufulu tu.hata Kama magufuli atakuwa mgombea binafsi wananchi wataelekea huko huko.vyama tunavyochagua ndivyo vilivyotufikisha hapa kwenye umaskini huu.
 
Ukiona unamwona huyu mtu kama mungu ujue huna akili
Japo sijasoma hilo gazeti, ila nilitarajia kuona list ya majina angalau mawili ya wanaoweza kumpita magufuli kwa utendaji wake.

Au ungetaja hata lwa kwako.
 
Ndani ya ccm na hata nje ya ccm kwa kizazi hiki sioni wa kumfikia magufuli hata robo utendaji wake.
Kwa haraka haraka toka baba wa Taifa nyerere aondoke madarakani 1984 nchi yetu haikuwahi kupata mzalendo kama magufuli wengi walijali maslahi yao ila magufuli kajilipua kuvaa viatu vya nyerere

Tukimpoteza magufuli itatuchikua miaka 30 tena kumpata magufuli mpya

Ndio maana tunakuomba magufuli ukae madarakani mpaka 2034 Ili uinyoshe nchi

Nchi ilishaoza hii ilishakua shamba la bibi

Magufuli tunakuomba kaa madarakani walau hata 2034 utupeleke tuwe kama Thailand

Hizi kelele za wachache mtandaoni ni za vijana wanaotumiwa na mafisadi kukuchafua zikuumize kichwa mzee wetu

Mungu akupe nguvu katika uongozi wako
Misukule FC indicators of dictatorship is ?
 
Back
Top Bottom