Kusema kweli Ada ya kufanyia miamala imepanda mara dufu

Wanatuibia sana haya mabenki na makapuni ya simu......Ukitaka kutoa 1m inakulazimu utoe laki 2 mara 5 na hapo wanalima kati ya 900 hadi 1000 kwa kila transaction kwa hiyo hpo unalimwa Buku 5 Nzima.
Mtandao gani huo mkuu?

Ila kwa hii mitandao ya simu kwa kweli mimi naitumia basi tu sina ujanja, unatoa laki saba unakatwa 7,300? Nyingi mno...
 
Sijui wanatumia vigezo gani kupandisha hizo gharama.
Wanatuibia sana haya mabenki na makapuni ya simu......Ukitaka kutoa 1m inakulazimu utoe laki 2 mara 5 na hapo wanalima kati ya 900 hadi 1000 kwa kila transaction kwa hiyo hpo unalimwa Buku 5 Nzima.
Tusilaumu sana kampuni za simu bila kuangalia chanzo ni nini!!

Nadhani mnakumbuka kipindi kile serikali ilisema kwamba inaongeza kodi kwenye miamala ya kutuma/kutoa fedha,wadau walipiga Sana kelele kwa kudai kwamba Mzigo wote ataaubeba mwananchi maana hizo kampuni za simu ni wafanyabiashara na katu mfanyabiashara hatataka apate hasara hivyo na yeye ataongeza gharama ambapo mwisho wa siku Mzigo wote anaubeba mtumiaji wa mwisho/mteja(mwananchi)

Tukija kwenye suala la kuongezeka kwa gharama za miamala hili nalo sidhani kama kuna haja ya kufikiri Sana. Ni wazi na sote tunajua kwa sasa mapato yamepungua maana watu wengi wamefunga biashara zao,misaada imepunguzea na mingine kukatwa kabisa kutokana na sababu mbalimbali hivyo ili kufidia pengo lililoachwa serikali haina budi bali kuongeza Kodi ndo hayo mnayoyaona sasa vitambulisho mpaka kwa wapika vitumbua,waokota chupa,kampuni za simu,nk. Na hii haitaishia hapo kuna mengi yanakuja.
Yajayo....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika mkuu huku wao wakiwa kwenye misafara ya kwenda kuzindua mpaka matundu ya vyoo kwa kodi tunazolipa kwa kuteseka

CC Zero IQ
 
Kwakwel tulipo kwa sasa n shda tu kama ndo kukusanya kodi kwa nguvu wamejitahd

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila kona tunakabwa mkombozi ulibaki kwenye mabasi tu napo kumepigwa kufuli.
 
Samahani lakini , hivi wakoloni bado wapo au walishaondoka? uhuru ndani ya nchi upo hilo sina shaka , ila ni uhuru wa kufanya nini uliopo? mimi hata sielewi elewi lakini angalau ugumu wa maisha unanitia adabu sasa!
 
na sio ada tu, hata gharama za mawasilano zipo juu mno saivi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…