Kusema ukweli, wakoloni Tanzania yetu hawakuiibia kitu!


Kumbuka hata huo mfumo wa elimu ya aina hiyo ni wao walituletea, mababu zetu walikua na namna yao ya kuandaa vijana namna ya kukabiliana na majukum yao. Bado tunarudi pale pale elimu ile ilitakiwa imsaidie mhusika kuwa mtumishi mzuri kwa hao hao wakoloni. Hatusemi yote yaliyofanywa hayakuwanufaisha waafrika la hasha, mambo mengi yalikua na maslahi mapana kwao.
 
Nun
 
Mkumbushe kuwa hzo stadi za maisha kama kilimo waliwaandaa kuwatumikia ktk mashamba ya kikoloni wakiwa kama mabwana shamba. Kwa hyo kama walinufaika halikuwa lengo la mkoloni hapo ni malengo kupitiliza na kuwanufaisha indirect
 
Silabasi moja na mtihani mmoja nchi zote zilizokuwa chini ya uingereza, shule za kati tulifundishwa useremala, ujenzi, kilimo na wasichana domestic, needlework na mengineyo yanayohusu mazingira ya kwenu, sasa sijui mwingereza alifaidika nini zaidi ya porojo za wanasiasa wa hovyo, nasema wahovyo kwani jambo linapokuwa bovu kisingizio lilijengwa enzi za mkoloni halifai! Ikulu ilijengwa na mkoloni na magereza nyingi ni za enzi za mkoloni. Ukweli utabaki palepale mwingereza alituachia elimu bora na ndiyo ilimwezesha mwanafunzi wa darasa la NNE kuwa na uwezo wa kuajiriwa umesenja ofisini na wa darasa la nane ukarani ofisini; Miaka 58 ni mingi sana tumefanya nini kwenye elimu na uchumi zaidi ya kusherehekea kupokea ndege tuliyoinunua badala ya tuliyoitengeneza. Alama yetu kama viumbe wenye akili ni ipi zaidi ya kuzaa watoto.
 


Hoja kwenye huu uzi ni wizi au uporaji uliofanywa na wakoloni. Mleta uzi anasema hawakuiba au kuchukua chochote, akatolea mfano miundo mbinu na vitu walivyofanya wakoloni.

Kuanzia jibu langu la mwanzo kwenye huu uzi, nimesisitiza kwamba chochote walichofanya hawa jamaa tunaowaita wakoloni, kiliwanufaisha zaidi wao.

Walihitaji makarani na vibarua ili kazi zao ziende. Hiyo elimu iliwasaidia waafrika kuwa na uwezo wa kutumika vizuri zaidi kwenye hizo kazi zao.
 
Mkuu MABABU zetu walivyocharazwa bakora na kuuzwa utumwani kama mifugo huo sio ubaya ??? Walifanyishwa kazi kama watumwa kweny Mashamba yote ya wazungu,walibebeshwa mizigo Punda cha mtoto,ubaguzi wa rangi ulitamalaki,waliwaua wote waliokataa kutumwa nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…