Kushabikia Soka la Ulaya hakutusaidii

Kushabikia Soka la Ulaya hakutusaidii

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319
Makala hii ilichapishwa katika gazeti la Mwananchi toleo la Jumatatu, 12 Mei 2014.
Na Mphamvu Daniel, Dar es Salaam.

Ni wikiendi moja tukiwa katiba banda la kutazama Soka mtaani kwangu. Naposema kutazama mpira namaanisha huu wa Ulaya uliozoeleka hadi vijijini kuliko mpira wetu wa Kiafrika, au Butua Butua kama waanvyoita.
Timu moja inapata goli na wananchi 'washabiki' wake wanaruka kwa furaha huku wenzao waliofungwa wakinywea kwa huzuni.
Mjadala juu ya mchezo ule unaendelea mtaani, watu wanataniana na kushiriki pamoja furaha ya timu 'yao' kushinda.

Mpira ndio umekuwa ulevi wa kisasa, watu wengi hutazama Soka. Zamani kidogo hali ilikuwa tofauti, watu wachache tu, tena wanaume, waliokuwa wakipoteza muda wao maridhawa kupigizana kelele kuhusu Soka. Sasa hivi hali ni tofauti, wanawake na vijana wadogo kiumri wamekuwa wadau wakubwa wa Soka la kwenye televisheni.
Kupanuka kwa teknolojia ya habari na kukua kwa makampuni yanayoonesha ligi za Ulaya kama DSTv kumefanya hali iwe kama ilivyo.
Mpira ni mchezo maarufu duniani kote na unavutia kutazama, Brazil, ambako kunaaminika homa ya Soka iko juu wana neno Joga Bonito ambalo tafsiri yake ni 'mchezo unaovutia' kumaanisha umaridadi wa mchezo huu.

Takwimu ambazo si rasmi zinaonesha kuwa umakini katika Soka la nyumbani unapungua, au tuseme idadi ya watu ambao humakinikia Soka la ulaya inaongezeka kila kukicha. Hali hii iko Tanzania na nchi zingine za Kiafrika.

Athari hii haipo Afrika au katika Soka pekee, bali pia kwa nchi za Amerika Kusini na Karibea ambako wao ni washabiki wakubwa wa Ligi ya Baseball ya Marekani (Major League Baseball)
Jambo hili lina manufaa makubwa sana kwa uchumi wa timu na nchi husika ambao wana ligi yao. Upande wa pili ni maumivu na kuendelea kukandamizwa kiuchumi.

Athari ya moja kwa moja kiuchumi ni pale ambapo washabiki wanaponunua jezi na wakati mwingine kulipia uanachama wa timu za Ulaya. Kwa maneno rahisi ni kuwa wanatoa pesa nchini na kupeleka Ulaya, jambo ambalo si zuri kiuchumi.

Athari nyingine kubwa ni pale ambako tunawachangia fedha kupitia haki za matangazo. Mchakato wa haki za matangazo si mgeni sana machoni kwa Watanzania kwani mwanzo mwa msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara tulishuhudia kitu cha aina hii baina ya Azam Media na timu za Ligi Kuu.
Timu huwa zinalipwa na kampuni za matangazo ya televisheni, kisha wao hupata faida kwa kuwauzia watazamaji matangazo hayo. Hapa Afrika kampuni ya DSTv ndio huonesha ligi nyingi za Ulaya, na huuza huduma zake kwa bei ya juu sana (pengine kuliko kampuni yoyote hapa nchini).

Kwa nchi ambako watu wake wanaishi chini ya dola moja kuendelea kuchangia uchumi mkubwa wa vilabu vya Ulaya inasikitisha, ingawa ukweli huu hausemwi siku zote. Ni muendelezo wa ukoloni mamboleo kwani Waafrika wanatawaliwa na Soka na michezo mingine.

Watu wengi huwalaumu wachezaji wa zamani ambao hali zao za kiuchumi zimeyumba. Washabiki hao hao ndio wanaona afadhali kuchangia tiumu ya Ulaya kuliko kwenda uwanjani na kuchangia timu za ndani.
Katika hali ambapo mechi za Ulaya zinaoneshwa na kushabikiwa nchini mwetu, washabiki wa Soka hutakiwa kuchagua kati ya mechi za nyumbani au za kigeni.

Kuna kipindi ratiba ya Ligi Kuu Uganda ilikuwa inapangwa ili kukwepa kugongana na ratiba ya Ligi Kuu ya Uingereza. Hapa nchini si jambo geni kuona watu wakiingia na redio viwanjani ili kupata matokeo ya mechi za Ulaya na kinyume chake.

Katika hali ya kuelekea mapinduzi ya michezo, hatuwezi kufanikiwa kama watu wataendelea kuwa washabiki wa michezo ya Ulaya. Timu zinahitaji washabiki ili ziendelee kudumu na zipate udhamini kutoka kwa makampuni. Simba na Yanga zilipata udhamini mnono kutoka TBL sio tu kwa kuwa wana kiwango kikubwa, lakini pia kwa kuwa wana idadi kubwa ya mashabiki ambao ndipo ,soko la bidhaa lilipo.

Vyombo vya habari na wachambuzi wa michezo nao wamefuata mkumbo huu. Magazeti mengi yamejaa habari za michezo za nje kuliko ya ndani na wachambuzi hutumia misuli mingi kuelezea na kufafanua yanayohusu timu za Ulaya.
Hali hii imepelekea hata washabiki nao kutojali sana kama tunadidimia. Wapo watu ambao huumia zaidi timu zao za Ulaya zinapofungwa kuliko inapofungwa timu yetu ya Taifa.

Mauzo ya jezi pia yamehamia kwa timu za Ulaya, na sio za nyumbani. Bila kufahamu kuwa kufanya hivyo ni kuzigandamiza timu zetu wenyewe ambazo mafanikio yazo ni heshima kwetu.
Ushabiki wa Kizungu ukizidi sana ndipo madhara ya waziwazi huonekana. Nchini Kenya kwa mfano, mechi kati ya Gor Mahia na Leopards iliyochezwa Mei mwaka jana ilihudhuriwa na washabiki 7000 tu katika uwanja wa Kasarani ambao una uwezo wa kuingiza watu 60'000.

Katika ligi yetu hapa Tanzania mahudhurio sio mabaya sana kwani hata mechi ambazo hazihusishi timu kongwe za Simba na Yanga inaweza kujaza uwanja (mfano Azam vs Mbeya City, Chamazi)
ulimbukeni wa michezo ya Ulaya unaenda mbali kiasi cha watu kujinyonga kisa timu ya Ulaya (Kenya) na tukio la shabiki mmoja wa Nigeria kugonga wenzake na gari baada ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Michezo ni utambulisho wa utamaduni, na inaonekana kuwa Waafrika wameamua kutambulika kama 'wazungu weusi'. Ndio, ni rahisi kusikia mtu akijitambulisha kuwa yeye ni shabiki damu wa Barcelona na tumu 'yake' ikifungwa hana raha.

Wenzetu kwa kufahamu madhaifu yetu wanazidi kutukoleza kwa kujifanya wanatujali. Mara kadhaa tumeona ziara za makombe ya Ligi za Ulaya yakifanya ziara Afrika. Ziara hizi hazifanywi kwa mapenzi yao kwetu bali mahitaji ya kibiashara na kuzidi kututeka akili.

Masikini mtu kwao, naamini ipo siku weusi wenzangu watatambua nafasi yao katika kuoko michezo na kuamua kurudi nyumbani.

+255713049852
 
...

....Mwenye historia ya mashabiki wa soka katika Taifa letu since huko nyuma Piter Tino ,Sembuli, Jela Mtagwa watupie kidogo
 
Timu za nyumbani zinawakatisha moyo mashabiki,na siasa imeingia kwenye soka letu, kumekuwa na maneno mengi ambayo hayaleti matunda tofauti na soka la huko nje amabalo pamoja na uwekezaji bado tuaona matunda watu wanaona bora kushabikia timu za nje kuliko za ndani ambazo kimsingi haziwafurahishi wapenzi wa mpira

hata kama hakuna faida tunayopata kwa kushabikia timu hizo angalau tunapata faraja na raha ya kimchezo
 
Pia kwenye makala yako ungesema kuwa wale wachezaji wote wa nchi za Afrika wanaochezea ligi za Ulaya warudi na kuchezea ligi za nchini mwao.

Yaani akina Victor Wanyama warudi wakachezee Gor Mahia Football Club. Maana kundelelea kuchezea huko hakutusaidii.

In fact kuna mjadala kama huu unaendelea hapa: https://www.jamiiforums.com/sports/651889-kuifanya-league-ya-tanzania-a-better-product.html

Kucheza waende tu wakacheze ili walete fedha nyumbani. Mahaba yabaki kwa timu zetu za nyumbani kama vile mimi ninavyoipenda Yanga hadi kufa.
 
Mimi sitaki kuchaguliwa timu ya kushabikia. Ni kama tu leo mtu aniambie nisinunue kahawa ya nestle, badala yake ninunue africafe ya hapa hapa. Dunia ya sasa ni network. Napata kitu roho inapenda.

Wakati nikiwa shule ya msingi nilikuwa shabiki wa yanga. Nikiwa sekondari nikaanza kupoteza interest ya mpira wa bongo. Hiyo ilikuwa miaka ya mwanzo ya 80. Maisha yangu ya ughaibuni ya zaidi ya muongo mmoja yakanifanya nipende na kulielewa soka la huko. Kinachonivutia hasa ni kitu kinachoitwa sports (football) management.

Nilivyorudi Bongo, nimeona Azam wana mwelekeo wenye matumaini. Kwa hivi sasa kwa bongo nashabikia azam. Lakini timu za ughaibuni siachi.
 
Makala hii ilichapishwa katika gazeti la Mwananchi toleo la Jumatatu, 12 Mei 2014.

Tatizo la mpira wa Tanzania unavutia kuusoma kwenye magazeti lakini uwanjani magumashi kibao. Viongozi wanaoongoza mpira wababishaji tu kuanzia vyama hadi vilabu.
 
Binafsi nimepoteza interest sana na soka la Tanzania, lipo stagnant kwa miaka mingi, hamna maendeleo zaidi ya siasa na USHIRIKINA. Timu ya Taifa na vilabu vimekuwa vichwa vya mwendawazimu, viongozi wamekuwa wababaishaji sana.

Katika kushabikia kwangu mpira wa miguu hapa nchini, nimeona napoteza nguvu nyingi, uyanga na usimba vimeathiri mpira wetu sana. Uwepo wa sponsorship toka kwa azam kunaonyesha jinsi gani mpira wetu unaweza wetu unaweza kubadilika.
 
Babu zetu walijitahidi kujituma tena bila malipo ya maana lakini bado hatujafika popote,sasa wachezaji wanalipwa mamilioni lakini ndo tunazidi kudidia afadhali ya zamani..kwa sababu hizo, ndo tunatafuta timu kama LIVERPOOL ili kupata faraja..
 
Madhara ya utumwa na kutawaliwa yanajionyesha.mataifa yote yaliyotawaliwa na wazungu yana kasumba ya kushabikia vilabu vya ulaya.kaulimbukeni hako nakachukia sana.mimi nabaki na simba yangu
 
Kwenye soka tunafuata burudani, soka la bongo ni stress tupu, mipango ya kipwagu, siasa za kina rage na malinzi mpaka mpirani, wacha tulowee ulaya
 
Shabikia azam basi au mbeya city,
Wanajitahidi wana mfumo kama hao unaowapenda
 
Back
Top Bottom