Kuna kikundi cha watu kinatumia nguvu Kubwa kuiaminisha jamii kuwa Mh. Mbowe alikuwa amelewa na hiyo ndo sababu ya kuvunjika mguu.
Kwanza ifahamike kwamba katika nchi yetu kulewa siyo kosa. Lakini pia kinacho shitua zaidi ni kwamba, wanao shabikia suala hili ni wale ambao siku za hivi karibuni walionyesha kukwaruzana na Mh. Mbowe.
Cha ajabu, mmojawapo anaye jaribu kuwaaminisha watu kuwa Mh. Mbowe alilewa ni spika Ndugai. Spika Ndugai akiwa kwenye kiti cha uspika kaongea kwa uhakika wote kuwa Mbowe alilewa, lakini kwa mtu anayemjua vizuri mlevi, kudondoka kwenye ngazi lazima angeumia kisogoni.
Hivi karibuni spika Ndugai aliingia kwenye majibizano na Mh. Mbowe, kwahiyo Ndugai kuongea haya anayoongea kunatia shaka Kubwa sana. Sidhani kama ana lengo zuri. Inawezekana ni kutimiza lengo lake kumchafua Mbowe ili asirudi bungeni kama alivyo Kwisha nukuliwa kuwa Mh. Mbowe hatarudi bungeni.