Scenarios za mashambulio yote mawili ( Tuñdu Lissu na hili la Mbowe Jana) yanafanana....
Obvious, wapangaji na watekelezaji ni walewale. Eneo la shambulizi ni lilelile. Walengwa ni wa chama kilekile walichoahidi kuwa ifikapo 2020 lazima kiwe kimefutwa...
Tofauti yake ni silaha tu zilizotumika. Tundu Lissu ni SMG na AK47 na za kuulia tembo. Huyu (Mbowe) naona walitumia na nondo na mipini kuvunjia nyonga na miguu....
Ishu ya mtu kurudi kwake saa 6 usiku haiwezi kuwa ajenda ukizingatia yeye ni kiongozi Mkubwa mwenye mambo mengi ya kushughulikia...
Mimi nina uhakika, matukio haya yanaratubiwa na viongozi wakubwa ndani ya serikali na CCM kwa baraka za Ikulu...
Tusitegemee taarufa sensible and meaningful toka polisi...
Na hii haina maana kuwa polisi nao watakuwa wanahusika direct kama Jeshi la polisi...
Ni kwa sababu wanaowalipa mshahara ndiyo wahusika na ndiyo wao wataandaa (na basically imeshaandaliwa) na polisi wao wataisoma tu public, na ndipo kila mtu atakapo shangaa huu mchezo unavyochezwa....
Hawa polisi wetu uwezo wa kufanya kazi yao "professionally" wanao tena ndani ya muda mfupi sana. Tatizo wameingiliwa na siasa za wanasiasa wenye mamlaka ya kuamua hata hatima yao hawa polisi....
Hawa ni watu wa kupokea na kutii amri tu ama sema "order", hawana namna, tusiwalaumu....
Na ndiyo maana ya Lissu Jana kusema, tukimpa ridhaa ya kuingoza JMT, moja ya shida atakayoishughulikia ni kufanya mageuzi makubwa (big reforms) kwenye miundo ya majesho yetu ili kuyafanya yatekeleze wajibu independently kwa misingi ya haki, sheria na katiba...
Hivi tunategemea nini kuteua mkuu wa Majeshi ama IGP ama RPC ama OCD kanda mtiifu wa chama kilicho madarakani?
Ni majanga kama haya...!!!