Kushambuliwa kwa Mbowe: Polisi wasema wanaendelea na Uchunguzi, wapiga marufuku tukio hilo kufanywa la kisiasa. CHADEMA yamuhusisha Mchungaji Mashimo

Kushambuliwa kwa Mbowe: Polisi wasema wanaendelea na Uchunguzi, wapiga marufuku tukio hilo kufanywa la kisiasa. CHADEMA yamuhusisha Mchungaji Mashimo

wewe unayejificha kwenye keyboard kwa kusema kitu ambcho huna ushahidi nacho, siyo Muoga! hebu fanya ujasiri uende hadharani utaje huyo unayemtuhumu kwa jina lake halisi kuwa ndo kahusika ili tukuone we ni jasiri zaidi yake!
we kenge acha kutisha watu
 
" Sasa jambo lenyewe (Mbowe kuvamiwa) lina hadithi nyingi ya jinsi lilivyotokea maanake inasemekana jana mpaka saa sita usiku alikuwa mahali, inaniwia ugumu kusema chochote kwa hatua hii lakini...eeh! niseme tu kwamba msichukulie kama watu wanavyoongea, watakaosema hali halisi ni vyombo vya usalama na niwaombe vyombo hivyo vitoe taarifa mapema iwezekanavyo, waeleze ilitokea nini isiwe ni kazi yangu...wanavyozidi kuchelewa hadithi zinakuwa nyingi "-Spika Job Ndugai.

Siku zote Mwizi huwa na Kiherehere kingi tu cha Kujitetea na Unafiki uliokomaa kwa waliomshtukia au wale ambao wanataka Kumuadhibu akome.
Chakushangaza wabunge umeshawapa airtime kuzungumza against Mbowe hukohuko ambako wewe ni kiongozi
 
Kwa jinsi hali ilivyo Hakuna namna tena viongozi ambao usalama Upo mashakan kuna haja ya kuwa na walinzo binafsi
 
Huyo spika ni moja ya wapambe tu wa tukio, Muhusika mkuu mbona anajulikana.

Uzuri hapa duniani huwa hatuishi milele na hivi nyeo vya duniani huwa ni vya kupita na Mwenyezi Mungu huwa hadhihakiwi!!
 
Hakuna taarifa nimeisoma nikiumia Kama hii ya Mbowe leo, kuna jitu lioga Kama jiwe ?

Wewe ni moja ya wake zake nini? Pole sana
Kama jana ulikuwa nae kwenye pombe kisha ukamkacha badala ya kumfikisha home shauri yako,
nasikia alijipongeza sijui kwa raha au kwa kutuliza mawazo maana kamanda katangaza apitishwe eti ndo anaweza kupamnana na JPM ,

wakati anapanda ngazi kaporomoka, kulingana na kilevi akawa anaona watu wanamkanyaga, kumbe ni njozi tu.
Mpeni pole apone halaka.🤣🤣🤣
 
Kwa jinsi hali ilivyo Hakuna namna tena viongozi ambao usalama Upo mashakan kuna haja ya kuwa na walinzo binafsi
Walinzi binafsi ni wazo zuri ila kila mtu akiwa na ulinzi- huko ndiko tumefikia watanzania?

Haya mambo ni mageni sana katika nchi yetu!!
 
viongozi ambao usalama Upo mashakan kuna haja ya kuwa na walinzo binafsi

Mbowe anao walinzi binafsi siku nyingi tu, swali muhimu walikuwa wapi wakati bosi wao anashambuliwa?!
 
Chadema lazima wahakikishe Mbowe anatibiwa kwa gharama yoyote, hata kama ni kukausha account za Chama. Haiwezekani Bungeni zitolewe taarifa za eti "alianguka akitoka kulewa" mara "aliendaje kituo cha afya badala ya Hospitali" aaah, wanaongea sana hawa watu!!
Huo ni USHUHUDA kuwa matakataka yao yameshindwa kumchafua Mbowe wala kuiua CHADEMA.
Ndio maana sasa 'wagonjwa' waliobakizwa bungeni kwa kazi hiyo, wako busy kushirikiana na SPIKA dhaifu kuokoteza vineno.
We shall overcome. Amen
 
Huu mpango utakuwa umesukwa ndani ya Chadema,kutafta sympathy kwenye uchaguzi,ila wajinga utasikia wanaropoka tu.
Wewe kama siyo kiwele invata wa facebook ni kundi moja lake wanaotafuta teuzi achana na ukada kwenye maisha ya mtu
 
Mbona kwenye inshu ya Ben Saa8 hamkusema Kubenea akamatwe ilihali mlimsikia mwenyewe kwa maandishi yake, akikiri kujua mahali Ben aliko na sababu ya kujificha?
Mashimo ni Nabii na unabii hauna ushahidi katika ulimwengu wa mwili labda wote wawe kwenye ulimwengu wa Roho.
Mi sikuwepo wakati wa Ben kama ilikua hivyo kwanini hawajamkamata kubenea? ndo maana nimesema waanze na huyoo mashimo
 
Kwani Ndugai alikuwa kaombwa kutoa maelezo kwenye swala hili?
Mbona anazidi kujishusha daraja?
Hii ni kazi ya wahuni ambao wanadhani wanaihami serikali ya awamu ya tano kwa maslahi yao binafsi, kumbe wanaichafua na kuibomoa vibaya sana. Serikali hii ni ya ccm; siyo ya mtu mmoja wala kikundi cha watu. Hiki ni chama ambacho Watanzania wengi wanajua siyo cha kihuni. Ila tusubiri kuona kama ccm ya sasa imeharibikiwa kiasi hiki.
 

Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma, Gilles Muroto amesema leo alfajiri walipokea taarifa kutoka kwa Mbunge wa Viti Maaalum, akiwa na Dereva wa Mbowe, Wilhad Urassa (34) kuwa Mwenyekiti huyo wa CHADEMA wakati akipandisha ngazi kuelekea ndani kwake inadaiwa alishambuliwa na watu 3

Kamanda Muroto amesema “Inadaiwa watu hao 3 waliokuwa wamevaa jackets (makoti) walimshambulia kwa kumkanyaga na kumpiga mateke hasa mguu wake wa kulia. Kutokana na taarifa hizo majeruhi alipelekwa katika Hospitali ya Ntyuka anakopatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.”

Ameeleza, “Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi bila kuacha chochote ili kupata ukweli na usahihi wa tukio hilo. Tukio hili lisitumike kisiasa au kwa njia yoyote ya kujiongezea umaarufu kwa mtu au watu na ni marufuku kuingilia uchunguzi huo.”

Amesisitiza kuwa eneo lile lina Walinzi na Majirani watafanya uchunguzi kujua ukweli wa tukio. Pia, amewaonya Wafuasi wa CHADEMA wanaohamasishana kukutana kwani Jeshi la Polisi lipo macho na yeyote anayefanya mikusanyiko isiyo halali atashungulikiwa kweli kweli

Aidha, Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema Polisi wanapofanya Uchunguzi hawapaswi kufunga milango ya uchunguzi na kuliita hili ni tukio la kawaida kwasababu viashiria vinaonesha tukio hili lina muelekeo wa kisiasa

Mnyika amesema kati ya watu waliokuwa wanamshambulia Mbowe wapo waliosikika wakisema “Wewe unaisumbua sana Serikali, tunakushughulikia tuone kampeni utafanyaje.” Ametoa wito kwa Polisi na vyombo vya Usalama kuchunguza tukio hilo kwa mapana ili waliohusika wachukuliwe hatua

Amesema siku chache kabla ya Mbowe kushambuliwa, katika mitandao ya Kijamii kulisambaa video ya mtu anayejiita Mchungaji wa Kitaifa, Mchungaji Mashimo akisema “Kuna tukio litatokea mbele kwa Kiongozi wa Upinzani kushambuliwa” na kati ya majina aliyoyataja, jina Freeman Mbowe lilikuwepo. Ametoa wito kwa Polisi wamkamate ili aleeze hizo kauli zake.

Inasikitisha sana
 
Huyu Muroto si ndiye aliyeshindwa kueleza tukio la Sheikh hadi leo
Si huyu ambaye hajui nani alimshambulia TL
Si huyu asiyejua Camera zipo wapi

Leo anafanya uchunguzi halafu anahitimisha kuwa siyo tukio la kisiasa hata uchunguzi haujaanza!!!

Hivi kwanini hakai kimya? Kila anapoongea Kamanda Muroto, kinachofuata ni kutia shaka na kuipaka serikali matope

Pascal Mayalla JokaKuu
 
Back
Top Bottom