Scenarios za mashambulio yote mawili ( Tuñdu Lissu na hili la Mbowe Jana) yanafanana....
Obvious, wapangaji na watekelezaji ni walewale. Eneo la shambulizi ni lilelile. Walengwa ni wa chama kilekile walichoahidi kuwa ifikapo 2020 lazima kiwe kimefutwa...
Tofauti yake ni silaha tu zilizotumika. Tundu Lissu ni SMG na AK47. Huyu (Mbowe) naona walitumia nondo na mipini kuvunjia nyonga na miguu....
Ishu ya mtu kurudi kwake saa 6 usiku haiwezi kuwa ajenda ukizingatia yeye ni kiongozi mkubwa mwenye mambo mengi ya kushughulikia. Narudia tena "muda mtu kurudi nyumbani kwake" is not an issue to dabate.....
Ambacho ni hakika bila kuacha chembe yoyote ya mashaka ni kuwa , matukio haya inaratibiwa na kutekelezwa na viongozi wakubwa ndani ya serikali na CCM kwa baraka za jumba jeupe...
Kwa hiyo kama ilivyokuwa kwa Tundu Lissu, tusitegemee taarifa yoyote sensible and meaningful toka polisi hata kama watatumia karne nzima kuchunguza...
Na hii haina maana kuwa polisi nao watakuwa wanahusika direct kama Jeshi la polisi kuulinda (cover up) uhalifu huu....
Ni kwa sababu wanaowalipa mshahara ndiyo wahusika na ndiyo wao wataandaa taarifa ya uchunguzi (na basically imeshaandaliwa) na polisi wao wataisoma tu public, na hapo ndipo kila mtu atakapo shangaa huu mchezo unavyochezwa....
Hawa polisi wetu uwezo wa kufanya kazi yao "professionally" wanao tena ndani ya muda mfupi sana. Tatizo wameingiliwa na siasa za wanasiasa wenye mamlaka ambao wanaamua hata hatima yao hawa polisi kwamba awe na kazi ama afukuzwe kazi....
Hawa ni watu wa kupokea na kutii amri tu ama "order", hawana namna, nao wana familia eti. Wafanyeje. tusiwalaumu....
Na ndiyo maana ya Lissu jana ktk hotuba yake kutangaza nia ya kugombea Urais, kasema, tukimpa ridhaa ya kuiongoza Tanzania, moja ya shida atakayoishughulikia haraka ni kufanya mageuzi makubwa (big reforms) kwenye miundo ya majesho yetu yote ili kuyafanya yatekeleze wajibu wake kikamilifu na independently bila kuyahusisha na siasa kwa misingi ya haki, sheria na katiba...
Mfano, tunategemea nini kama Rais Magufuli huyu aneteua mkuu wa Majeshi ama IGP ama RPC ama OCD kada mtiifu wa chama kilicho madarakani?
Hakuna " positive" cha kutegemea bali ni taabu tu na majanga kama haya...!!!