Wakati wa Mkapa sikuwa na upeo wa kufuatilia mambo ya siasa siwezi kumuhukumu.
Kuanzia kwa Kikwete ndio nilianza kuona mchezo wa kuteka na kupiga wale walioonekana "wasumbufu" kwa serikali, Dr. Ulimboka.
Magufuli ndio akaja kuweka msingi rasmi wa haya matendo, wengi walitekwa, kutwswa, na kuuwawa wakati wa utawala wake.
Rais Samia nae hana muda mrefu madarakani lakini inaonekana muendelezo wa haya matukio unaendelea pale alipoishia mtangulizi wake, hii precedence haionekani kwisha hivi karibuni.
Chanzo cha haya inaonekana sio kiongozi, ni tatizo la kimfumo ndio maana kila kiongozi anaekuja anarithishwa ukatili wa wenzake, wengi tunaishia kuwalaumu viongozi hapa ndipo tunapokosea.
Katiba Mpya itakapopatikana ikaleta usawa kati ya raia wa nchi hii, na ikaonesha majukumu ya Rais alie madarakani utekelezaji wake na mipaka yake, na hatua gani atachukuliwa akivunja haki za kiraia wakati wa utawala wake, ndicho kitakachokuja kutunusuru na huu ukandamizaji usiokwisha.