Kushikiliwa kwa Fwema: Umoja wa wachora katuni waonya

Ni wale waliojipanga kumchafulia Rais Samia Suluhu, tuseme wanasaboteji utawala wake, na huzusha hili na lile ili lawama zote zielekezwe kwenye utawala wake.

Ni bora Rais Samia naye akawabana wale wanaozusha mambo ya ajabu ajabu ambayo hupelekea kuishusha nyota ya serikali yake maana kwenye kundi la mamba na mikenge imo.
 
Hivi unafikiri ile kauli yake ya "LAZIMA NIHESHIMIWE" aliwekewa tu kinywani?
 
Mama unachemsha, jiangalie usianguke
 
Kuna uzi ulipostiwa jana kuwa huenda tukawa na Awamu ya 7 mpaka kufikia 2025. Naona Uliondolewa hadi sasa sijui lengo au maudhui ya mleta uzi.
 
Hawawezi kufanya kitu ambacho boss wao hakipendi,ukiona yanaendelea Yale Yale ya awamu ya 5 jua boss wao wa Sasa hivi amebariki.
 
Kamati kuu nzima inakaa kujadili upumbavu kama huu badala ya kuwashughulikia wanaomuhujumu mama?

 
Wakati wa Mkapa sikuwa na upeo wa kufuatilia mambo ya siasa siwezi kumuhukumu.

Kuanzia kwa Kikwete ndio nilianza kuona mchezo wa kuteka na kupiga wale walioonekana "wasumbufu" kwa serikali, Dr. Ulimboka.

Magufuli ndio akaja kuweka msingi rasmi wa haya matendo, wengi walitekwa, kutwswa, na kuuwawa wakati wa utawala wake.

Rais Samia nae hana muda mrefu madarakani lakini inaonekana muendelezo wa haya matukio unaendelea pale alipoishia mtangulizi wake, hii precedence haionekani kwisha hivi karibuni.

Chanzo cha haya inaonekana sio kiongozi, ni tatizo la kimfumo ndio maana kila kiongozi anaekuja anarithishwa ukatili wa wenzake, wengi tunaishia kuwalaumu viongozi hapa ndipo tunapokosea.

Katiba Mpya itakapopatikana ikaleta usawa kati ya raia wa nchi hii, na ikaonesha majukumu ya Rais alie madarakani utekelezaji wake na mipaka yake, na hatua gani atachukuliwa akivunja haki za kiraia wakati wa utawala wake, ndicho kitakachokuja kutunusuru na huu ukandamizaji usiokwisha.
 
Watanzania waliowengi ni wanafiki wakubwa.
 
Kiongozi wao ni yupi naye akamatwee

USSR
Rejea maneno ya Kikwete mwana CCM mwenzio. Tena CCM kweli kweli sio nyie mnaosubiri teuzi.
Kikwete alimaanisha ' hatuwezi kutegemea polisi kutuweka Madarakani Ila Sera nzuri na utawala bora'
Lkn pia muuaji Idd Amin alikiri kabisa kwamba "you can't kill everybody"
 
Hivi unafikiri hilo jambo limefanyika kwa bahati mbaya?
 
Mlishabgilia kifo cha Dkt Magufuli. Mlisema ohh Mama anaupiga mwingi hahahhahahah

Urais ni taasisi na siyo mtu. Nadhani sasa akili zinawakaa sawa.

Huwezi kuwa unadhalilisha taasisi ya urais kiasi hicho. Na badooo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…