Kushindwa kutofautisha Neno Upare na sehemu nyingine

Kushindwa kutofautisha Neno Upare na sehemu nyingine

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2017
Posts
3,868
Reaction score
5,164
Jana kwenye msiba wa mhe marehemu Makamu wa pili wa rais, Waziri mkuu mstaafu Cleopa David Msuya nilisikia mshereheshaji wa serikali akichanganya mafaili nikagundua ni bahati mbaya hajui na wengi hawajui nikaona nitoe ufafanuzi wengi waelewe.

Neno Upare ni pana zaidi ya watu wanavyofikiri. Linajumuisha wilaya mbili Same na Mwanga watu hawa wote wanaitwa Wapare na wanaongea lugha moja inaitwa Kipare japo kuna tofauti ndogo za lafudhi lakini wanaelewana.

Kuna sehemu inaitwa Usangi anakotoka huyu marehemu. Usangi ni sehemu ambayo iko ndani ya Upare wilaya ya Mwanga na watu wa Usangi wanaongea Kipare. Kuna sehemu nyingine inaitwa Ugweno hawa wote nao ni Wapare ila kuna lugha wanayotumia inaitwa Kigweno.

Niligundua mshereheshaji alikuwa anaeleza kitu fulani nikagundua anashindwa kujua Usangi pia ni Upare sawa na ile ya kule Same.

Same nayo ni wilaya kubwa sana inakwenda hadi imepakana na Mombo, Same ndio kuna Hedaru, Makanya, Kihurio, Gonja, Kisiwani, Bendera ambapo ndio karibu sana na Mombo.

Hii ni sawa na Mbeya watu wamezoea kusema wanyakyusa lakini humo humo kuna sehemu mbali mbali kama Rungwe, Ileje na wanatumia lugha moja japo pia kuna makabila madogo ndani yake n.k.

Mtu akisema anakwenda Gonja Same Upareni kwa Wapare na Mtu wa Usangi akisema anakwenda Mwanga Upare kwa Wapare au mtu akisema nakwenda Ugweno Mwanga kwa Wapare mtu huyo atakuwa sawa kwa sehemu zote hizo.

Tofauti tu kidogo ni kwamba wilaya ya Mwanga humo ndani ndio kuna Usangi na Ugweno
Na Same ndani yake ndio kuna Hedaru, Gonja, Gonja Maore, Mwembe, Makanya, Kihurio, Bendera wilaya Same ni kubwa sana ndio maana kukawa na majimbo mawili ya uchaguzi Same mashariki na Same magharibi kwa Mwanga ni tofauti jimbo ni moja tu.

Zamani miaka ya 80 kurudi nyuma Mwanga na Same zote zilikuwa ni moja ziliitwa Wilaya ya Same ndio zikagawanywa na hata hivyo bado Same ni kubwa.

Pengine naweza Sema Wilaya ya Same ni kubwa kuliko mkoa wa Dar-Es-Salaam
 
Wapare wana utaratibu wa kuzikwa makwao kama wachaga au wenyewe popote kambi? December wanaenda kijijini?
 
Back
Top Bottom