Aisee kumbe! Nilikuwa sijui kama Same ni kubwa hivyo! Mbona nasikia wagweno hawataki kuitwa wao ni wapate?
Mkuu ngoja nikupe data za uhakika sasa
Wilaya ya Same ina kilomita za mraba 6,221
Mkoa wa DSM una kilomita za mraba 1,590
Ili Dar ipate Same inabidi dar iingie mara nne ndio itakuwa sawa na Same
Sasa twende kwenye mlinganyo mwingine
Wilaya ya Mwanga ina kilomita za mraba 1,831
Maana yake nini basi maana yake hata wilaya ya Mwanga ni kubwa kuliko mkoa wa Dar
Dar inaingia mara 1.1 kupata Mwanga kwa ukubwa
Tuendelee kwenda kazini
Mkoa wa Kilimanjaro una ukubwa wa kilomita za mraba 13,250
Ukichukua wilaya Mwanga ukajumlisha na wilaya ya Same unapata kilomita za mraba 8,052
Hii maana yake nini basi?
Hebu tuchukue ukubwa wa Kilimanjaro tutoe ukubwa Mwanga na Same yaani 13,250-8,052
Jibu unapata 5,198
Hii maana yake nini basi maana yake ni kwamba hizo kilomita za mraba 5,198 ni eneo la wilaya zingine tano za mkoa wa Kilimanjaro zilizobakia yaani Moshi mjini,Moshi vijijini,Rombo,Hai na Siha
Maana yake ni kwamba Wilaya ya Mwanga na Same peke yake inazidi wilaya tano zingine zilizobaki za Kilimanjaro.
Kiuhalisia kama tungefuata lafidhi Wapare wanafit kwa Tanga hasa Wasamba ila sababu za kijigrofia Mkoloni alikuwa na Mpango wa kutoa Uhuru kwa eneo hilo ila akaona litakuwa dogo ndio akachanganya na Same ya Wakati huo.
Nikujibu kwanini Wagweno hawapendi kuitwa Wapare.Jibu ni kwamba kiuhalisia chimbuko la Wagweno ni Uchagani waliohamia Milimani na ndio maana wana lugha yao tofauti kidogo ila mila na Wapare ni zile zile na mfalme wao zamani alikuwa anaitwa Minja.
Angalieni ramani ya Kilimanjaro