Kushtuka kutoka usingizini usiku wa manane

SteveJr99

Senior Member
Joined
May 13, 2019
Posts
137
Reaction score
291
Habari zenu wanaJF. Natumai wote ni wazima.

Mara kadhaa nimejikuta nashtuka usiku wa saa 7 au saa 8 usiku na usingizi kukata kabisa, inaweza kunichukua hata lisaa kupata usingizi tena.

Nimejaribu kuuliza hiki kitu kwa watu wa karibu wengine wanasema ni stress za maisha, wengine sina ela ntafute ela, wengine presha lakini me binafsi sina stress na kiafya hata kiuchumi niko vizuri.

Shida itakua nini sasa na kwa nini hii hali hutokea yani kwa mwezi lazima inikute mara 4 au 5 kwa wenye kujua hii hali tujuzane tafadhali.
 
nadhani umepakana na MMAKONDE hapo,au sio?
 
Kwani CHADEMA wanasemaje? Umewauliza?
 
shida yako kubwa hufanyi mazoezi au hutembei kwa miguu, fanya mazoezi utakuja kunishukuru
 
Huo ni mwanzo tu makubwa yanakuja siku utakiona live kiumbe chenyewe kinachosababisha hiyo hali
 
Mim pia ilikuw inanitokea,ila nahc kama mdau anavosema kuwa fanya0mazoezi..
 
Ni ndoto za kawaida ambazo zinatokana na harakat zetu za kutwa nzima na mawazo juu ya mambo ambayo tunahitajika kuyafanya in the future.

Incase of anything basi Sali kwa imani yako muombe Mungu unayemuamini na tatizo litaisha
 
Hiyo ndiyo mida ambayo Mwenyezi Mungu anapokea na kusikiliza shida za waja wake jijengee mazingira ya ukishtuka omba Toba na mshukuru Mungu kwa kila alichokujalia na umuombe aendelee kukujalia,au kakaa kwa kutulia kitandani fumba macho angalia Jambo gani litakuja kichwani mwako lifanyie kazi
 
Unafanya mambo mengi mchana alafu huyamalizi kwaiyo ubongo unashtuka na moyo kwenda mbio kwa hofu kwamba kazi fulani ya muhimusijaimaliza
 
Wewe hujaoa, kama ni KE basi hujaolewa .... Tuulize tulioko kwenye ndoa, unalala vizuri kabisa. Usingizi ukikata mnaamshana then mnaanza kuteta majirani na workmates Hadi mnapotelea usingizini tena! Sema nini, usikosee kuoa, utajikuta unaimba ule wimbo WA Men's National Anthem. Utafute
 
Kwa kawaida ikifika mida hiyo lazima niamke nakuja kupata usingizi saa 10.
Imenisaidia sana dhidi ya wezi na kutafakari mipango yangu
 
Hali hii inatokana kupata tendo kwa nadra pia inategemeana unalala saa ngapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…