Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE MHE. SANGA - KUSHUSHA KODI YA NGANO INAYOTOKA NJE NI KUIFANYA YA NDANI IKOSE SOKO
Mbunge wa Jimbo la Makambako Mkoani Njombe, Mhe Deo Sanga ameiomba serikali kutopunguza Kodi Kutoka 35 Mpaka 10 kwa wazalishaji wa Ngano kutoka nje ya Nchi kwani kufanya hivyo ni kutoa thamani ya Mzalishaji wa ndani na hatimaye zao lake kukosa soko.
Ni Miongoni mwa Mchango ambapo umewagusa watanzania wengi wakiwemo walengwa ambao ni Wakulima wa Ngano uliotolewa na Mbunge huyo Jun 20, 2023 Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia Bajeti ya Kuu ya Serikali ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024.
“Kupunguza Kodi ya Ngano inayotoka nje unawafanya hawa wakulima wa ndani waone hauna umuhimu" - Mhe. Deo Sanga
Kufuatia mchango wa Mbunge huyo ukamuibua Mbunge wa Makete Mhe. Festo Richard Sanga kutoa taarifa ya kuunga mkono Mchango huo kwa kuona kuwa kitendo cha kupunguza kodi ya ngano inayotoka nje italeta athari ya Ngano itakayoenda kuzalishwa na Mzalishaji wa ndani ikose soko.
“Mheshimiwa rais ametoa ngano bure kwa wakulima kwa Wilaya ya Makete iweze kulimwa na kusambazwa viwandani kwahiyo kitendo cha kushusha kodi kitaenda kufanya ngano inayoenda kulimwa na wakulima wetu ikose soko, kwahili wizara ya Fedha lazima iliangalie" - Mhe. Festo Sanga
Pamoja na Mambo mengine Mbunge Deo Sanga hakuwa kando kupaza sauti juu ya faini anayopigwa mfanyabiashara pindi anapofanya makosa kwani wengi wao hawana elimu ya kutosha hivyo kwani kufanya hivyo siyo suluhu.
"Bado wafanyabiashara hawajapata elimu faini ya Shilingi Milioni 3 bado ni kubwa siyo suluhisho tunaomba walau iwe Milioni 1 itakuwa angalau kwa mfanyabiashara ambaye ni mlipa kodi kuna vingine vinafanyika bila Mfanyabiashara kujua kama hili alilofanya ni kosa kwasababu wafanyabiashara walio wengi ni hawana elimu nia ya serikali siyo kukusanya faini" - Mhe. Deo Sanga
Amehitimisha kwa kuiomba serikai Serikali kuanza utekelezaji wa Mradi wa Leganga na Mchuchuma kuhakikisha unaanza ka wakati ili wananchi wanufaike nao.
“Fidia imeshalipwa, ombi letu ni kwamba Mradi huu ni lazima serikali muhakikishe unaanza kama ambavyo watanzania wanategemea" - Mhe. Deo Sanga