Kusitishwa Mradi wa Bagamoyo SEZ kumedhihirisha udhaifu wa Rais Magufuli kwenye Uchumi na Diplomasia

Aisee! Akili kama hizi zako hazina tofauti na zile za kina Mangungo wa kipindi kile cha utumwa
 
Tuko pamoja mpaka hapo,nakukumbusha tena mkuu,kusema kwamba kusimamia wenyewe ndio tutapata faida kidogo kuna ukakasi japo nakubaliana nawewe mirabaha nayo ina changamoto kikubwa ni majadiliano,mfano sasa hivi makusanyo ya taasisi nyingi ikiwemo bandari yanaenda hazina,mfano mda huu bandari wawe na changamoto ya vitendea kazi mlolongo wa kupata hiyo pesa ili wakanunue vifaa ili waboreshe utendaji utakuwa mrefu na pengine wasifanikiwe huku utendaji ukiendelea kuzorota wewe mwenyewe utakuwa unajua milolongo ya mambo ya serikalini ni tofauti na kwa wawekezaji.mfano mzuri ni mwendokasi wameagiza magari karibia 100 lkn bado hayajaingia barabarani pamoja na uhitaji mkubwa wa magari hayo sasahivi yote hii kwasababu taratibu gani dijui za manunuzi wabia hawakuelewana yani serikali na mwekezaji.
 
amekiri kuwa ni kweli mradi una masharti magumu, hajayasema hayo masharti. viongozi wa namna hii ni hatari kwa nchi, serikali yenye akili timamu ikakatae mradi wa trilion 23 hivi hivi? wasomi wa tanzania wana bei, wanaweza kulipwa kitu kidogo waje wapige kelele humu mitandaoni
 
kichwa maji kweli wewe unasoma kwa kuruka ruka kukimbilia dirashani kupanga foleni kwa ajili ya buku saba. Huo mradi wa bagamoyo ni uwekezaji sio kwamba nchi inatoa kila kitu toka mfukoni mwake zaid ni hao wachina ndo wanahusika kurun hiyo project
Mkuu, kichwa sio pambo! Kitumie kufikiri!
 
jamaa kahis akijenga Kikwete atafaidi sana kaamua kusitisha ili ajenge uwanja chattle mambo yanayofanywa awamu hii ni ya hovyo toka dunia iumbwe
 
Ni maamuzi ambayo watakuja kuyajutia in 10-15 years time, bandari ya Dar as a center of gravity kwa uchukuzi wa Tanzania na nchi za jirani aiwezi mudu volumes kadri uchumi wa Tanzania, Uganda,Burundi, Zambia na nchi zingine zinavyokuwa na logistic zake zitaongeza kero zaidi kwenye jiji. Kwa ivyo expansion of transportation infrastructure is bound to occur which is a future expensive undertaking.

Vitu vingine inabidi ufikirie in 20 years time sio leo tu.
 
Hujasoma na kuelewa kilichoandikwa rudia tena kusoma
 
Courtesy ni muhimu sana katika masuala ya uandishi. Ungekuwa muungwana hasa kama ungetaja jina lake hapa.
 
Sasa huu si upunguani yaani kuingiza trion of shilingi kwenye miradi ambao ni hasara eti huduma,kwamba watu wa kanda ya ziwa wana haraka sana ya kufika Dar?
Nchi hii ina watu wenye hofu na hawawezi kufikiri,,ingefaa maeneo wanayoyatilia doubt yapelekwe mezani yajadiliwe,impacts ya matrion ya bagamoyo kwenye uchumi ni faida kuliko sgr zisizo na maana,,kwani huko Singapore etc huoni free economic zone zinavyoleta faida? Mfumo wa ppp ndio model nzuri kuliko serikali kukopa na maurasimu juu
 
Tayari umehaharibu mjadala kwa kutumia maneno makali ya kashifa na dharau.
Unge pungukiwa na nini kama usingetumia neno 'upunguani'?

Ni kitu cha ajabu kumuona mwenzio punguani sababu mmetofautiana vipaumbele au misimamo.

Kila la heri kiongozi.
 
Wewe ni mvivu wa kusoma na kufikiri. Tayari hata Ndugai ameshamuelewa ZZK na anaonekana kutomuunga mkono yule mkuu katika hilo. Amka!
Nyinyi ndio wale watz wachache mnaotegemea akili za mtu kuishi.

Yaani kila mtu unataka akubaliane na huyo zitto, kwanini una imani naye kiasi hicho!!!

Kwenye hili swala mnaonyesha upumbavu kiwango sana bila kusita.
 
WasiWasi wangu ni kua ata kimradi cha SGR hakitakamilika
 
Nadhani ipo haja ya kujua masharti haya ni yapi, maana hapa maelezo yako ya jumla jumla sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…