Twende Mbele turudi Nyuma, hili ni kosa kubwa serikali ya awamu hii ya tano imefanya, Tanzania ambayo inataka kukua kiuchumi Zaidi haiwezi kuwa inaogopa ushindani, hoja ya kusema china itataifisha bandari tukishindwa kulipa ni hoja totally mfu, mfu kabisa,mawazo ya kimasikini kabisa, sisi tumetoa eneo la uwekezaji tu, mtaji unatoka china/Oman,hata kama china/oman wataendesha hiyo bandari kwa muda ya miaka kadhaa ni sawa, serikali wao watakuwa wanapata mapato, ajira zitaongezeka kwa vijana, bagamoyo ingekuwa na kuwa center ya usafirishaji wa bidhaa katika ukanda huu wa EAC nad nchi nyingi za kusini,ukisimamisha mradi huu kwa woga wako kuwa eti bandati yetu ya Dar itakufa au kukosa mizigo huwakomoi wachina, unakomoa wananchi wako, unajikomoa wewe mweyewe na serikali yako kwa kukosa mapato, unajirudisha nyuma wewe mwenyewe katika dhamira ya Tanzania ya viwanda,tuacheni kuogopa kwa kila jambo, nature ya Zambia na srilanka ni tofauti na Tanzania, kwa hili Zitto Kabwe yuko sahihi Zaidi 100%, Magufuli aangalia upya maamuzi yake, ni bora aangalie jinsi ya kukutana na Rais mwenzake wa china kwa majadiliano Zaidi.