Kusoma Postgraduate (Master/PhD) UDSM majanga

Udsm wanapjga sana pesa za mama.. kumbuka enzi za jiwe kwa pesa za ndani hapo udsm wamefanya mambo mengi sana.. wamejnga ukuta, barabara na baadhi ya majengo.. lakini leo wanakula tuu mapato ya ndani
Barabara zile zinajengwa na TANROAD kwa makubaliano zitumike na umma
 
Well unaweza kua na hoja, lakini pia nataka kukukumbusha kua tuna kitu tunaita research and innovation. Research ni more academic than innovation, ndo hapo nguvu ya hoja yako inapoingia. Coz kuinnovate kitu ambacho kina application kwenye jamii sometimes doesn't necessarily need scientific investigations nor research. Ndo maana kuna watu wengi tu wana innovate vitu na hata hawana elimu ya chuo kikuu. But ukiingia ndani zaidi to some extent, innovation inaweza kuhitaji kufanyiwa research ili kuiboresha zaidi. Ndo maana makampuni makubwa duniani yanapeleka hizo innovative ideas kwenye vyuo vikubwa ili zikafanyiwe utafiti zaidi na lengo ni kuiboresha na kuifanya salama zaidi kwa mtumiaji wa mwisho. For instance nimewahi kupitia pitia websites za vyuo mbalimbali vikubwa duniani na nikaona wanatangaza scholarships za Master's & PhD lakini unakuta kampuni kubwa za vitu mbalimbali kama magari, simu, mambo ya gesi n.k ndo wametoa sponsorships kwenye hizo ideas na wanashirikiana na chuo kwenye kila kitu. So mwanafunzi anasoma na kufundishwa na lecturers wake but on the flip side anaenda kiwandani for industrial practices. Kwa upande mwingine tena kuna research nyingi tu ambazo zimepitia kwenye scientific investigations maabara kabsa then finally zikaenda kuzaa product ambayo ina direct impact kwenye jamii. Nini nataka kusema hapa?! Issue ni kwamba huwezi kutenganisha research and innovation maana vyote vina lengo moja tu ya kutoa product ama kutatua changamoto kwenye jamii husika. So wenzetu wamefanikiwa kwasababu wameziunganisha kupitia viwanda ambavyo vinahusika na hizo ideas/ product. Sisi tunafeli kwasababu tumetenganisha research peke yake, innovation peke yake na viwanda vinapambana kivyao kuimprove products ambazo zitaweza kushindana sokoni. Ndo hapo inapokuja kuonekana Elimu yetu ya chuo kikuu haina maana coz inaishia tu kwenye makaratasi na industry haijui nini wanafanya zaidi ya kuandaa watu ambao wakifika kwenye industry mchango wao unakua mdogo sana. Nitarudi baadae!
 
Ahaa, noted.

Kumbe competency+portfolio matters alot kwenye career.

Masters na PhD sio muhimu sana labda zile kada ambazo masters ina direct impact kama medicine bila kusahau researchers.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu ni Osoro Mkubwa,naona mwanae hakazi sana kama Baba yake.
 
Kaka kila kitu kinaanza na theory kwanza kisha ndio hizo practical training mbona hizo statistical packages kama R na STATA zinatumika sana.hiyo SPSS isha pitwa na wakati na haitoi results nzuri.
 
Hahahaha [emoji38][emoji1787]
 
Kuna yule Mama Mkenda Mke wa Waziri Mkenda,yeye ukimtumia kazi leo kesho alisha kupa ukileta uzembe huwa anaenda kwa coordinatar wa Research anamwambia wakubadilishe wakutafutie supervisor mwingine.

Yupo smart na faster sana yule Mama sijui kwa sababu sio Mtanzania.
 
Wakuu nilikuwa natamani nifanye masters of taxation, hapo udsm.
Ila kwa hizi comments, mbona mnanitisha

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
Jipange maana watu wanapata sana supp na wengine wana Carry masomo hiyo masters itakubidi usome kama undergraduate. Huko kwenye research ndio majanga matupu kama program yako ni 18 months jua fika kama mpo 40 hadi huo muda ata graduate 1 au 2 wengine lazima mtachukua zaidi ya 3+yrs

Ushauri wangu kama huna muda wa kutosha kusoma na kufanya dissertation yako tafuta chuo kingine.

Wewe imagine vyuo vingine ni vigumu kusikia MTU anasoma masters halafu ame supp,Ku carry au Ku disco but UDSM at master's level watu wengi sana wana supp na Ku carry kuna baadhi ya kozi hadi nusu ya darasa.
 
Sasa kumezesha watu hizo referencing styles sijui APA, sijui Vancouver, na yenyewe ni ishu ya kujivunia? Hizo makitu unaingiza tu details za unachotaka kureference kwenye software (eg Mendley, Zotero, etc), una select referencing style unayotaka kama ni APA, kama ni Harvard, whatever you want, inakuchapia reference hapo fasta.
 
Sasa kati ya mzumbe na udsm ipi nafuu kwa level hyo hyo master

Mbna watu tunalia na mzumbe Hadi wengine tumeingia mitini ......siwezi kujianika Sana [emoji38]
Mzumbe ni nafuu zaidi na ukitaka kuhakikisha chukulia idadi ya wanafunzi wanaokwenda kuchukua hayo masomo ya master's.
Mfano kwenye masters ya uchumu katika mwaka wa masomo 1 unakuta kuna wanafunzi 30 wa wanaochukua master's ya uchumi but Mzumbe unakuta wapo 80-120 kwenye program hiyo hiyo.
 
Wewe jamaa unajua sana maana ya Masters.
 
Hapana hii sio hoja kama issue ni wingi wa wanafunzi wa masters na PhD,ni issue ambayo ipo ndani ya management ya chuo maana wanaweza wakapunguza udahili wa wanafunzi uendane na idadi ya Walimu.
1.Mimi nimefatilia sana hivizuri ,kitu nimegundua ni kuwa Wahadhiri wa UDSM 95% hawapo responsible katika kazi zao na hiyo imetokana na mazoea waliyojiwekea huko miaka ya nyuma kuwa sio lazima watu wamalize kwa wakati-kiufupi wanafanya kazi kama ambavyo Watumishi wa Umma wengi wanafanya katika Taasisi mbalimbali za Serikali.
2.% kubwa Wanafunzi wanajihangaikia wenyewe ndio maana ukiwa haupo vizuri au kama umezoe spoon feeding UDSM utaumia sana.
3.Management ni mbovu sana kuanzia wahusika wanaotakiwa wasimamie chuo mpaka kwa vice chancellor.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…