Just Distinctions
JF-Expert Member
- May 5, 2016
- 3,230
- 6,742
Katika Kikao cha Wenyeviti na watendaji wa taasisi za Umma kinachoendelea Jijini Arusha ambacho kinaongozwa na Msajili wa Hazina Ndg. Nehemia Mchechu, katika moja ya maongezi yake amekiri ana degree moja na hana mpango wa kuongeza nyingine kwa sasa.
Amezungumza hayo baada ya kuzungumzia suala la Vyuo Vikuu kutokuwa na fedha (kulia ukata) hasa vile vikongwe kama UDSM, IFM na Mzumbe wakati wana wanafunzi wengi waliowafundisha na wapo kwenye taasisi mbalimbali ambao wanaweza kusaidia kuidhinisha fedha zitakazowasaidia kwenye masuala yao kupitia CSR etc.
Akachagiza kuwa atafanya kikao na VCs ( makamu wakuu wa vyuo) ili kujadiliana kuhusu issue tofauti ila hana mpango wa kurudi darasani kuchukua degree nyingine wasije wakamkamata bure (kupata Supplementary n.k) hii moja aliyonayo inamtosha.
Ukiangalia kwa namna historia yake ya ufanyaji kazi na wasifu alionao sasa, unaona kabisa kuwa na ma-degree mengi sio sababu ya kuwa mtendaji mzuri au mwenye sifa ya kuongoza taasisi nyeti, unaweza ukawa na degree moja na bado ukaongoza taasisi nzito na nyeti na bado ukafanya vizuri, uwezo ukiongeza na uzoefu unatosha kabisa kufanya jambo.
Anyway ni hilo tu tuendelee kupambana na kulijenga Taifa letu.