Kusoma shule za umma Tanzania ni mateso ?

Kusoma shule za umma Tanzania ni mateso ?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Wanafunzi wanaoshangilia kumaliza shule kama wendawazimu wehu mpaka wanatukana hovyo inawezekana pia ni dalili ya kwamba kusoma shule za umma ni mateso na wengi wanaosoma huko hawafurahi wala hawapendi ila wanalazimishwa tu.
 
Madogo wanasoma huku wameshikiwa bunduki au unamaanisha nini? Hao wanaofanya hivyo hawataki tena kusoma washaona Zuchu mwenyewe na bwanake shule hawqna na ndio ma-role model waao wewe unafikiria kuna mtoto anaependa shule pale wanajifunza kutokana na wale wanaowashabikia ameshakwambia akili sina na dogo anaimba kabisa kwa kufurahi akili sina unafikiri ataipenda shule na akili hana unafikiri shule wanaenda wasiokua na akili?
 
Sasa mwalimu wenyewe wamevurugwa unategemea wanafunzi watakuwaje?

Shule za kata huwa ni hazina misingi I mara ya uendeshaji, ila pia mifumo zimebadilika mno, mwalimu hawako serious kama zamani.

Hawa hawa mwalimu wao pia ni Gen z na millenial wasio na maadili unategemea nini?
 
Watoto wote hawakuonesha kuwa shule za uma ni mateso ila walionesha kuwa watakuwa huru kufanya Yale ambayo umri na Sheria za elimu haziruhusu
By the way hata wazazi wao waliandika chooni na kwenye kenchi"akumbukwe sanart"unategemea watoto wasemeje
 
Back
Top Bottom