Kusoma VETA hakutakusaidia lolote kwenye nchi hii, tatizo ni mifumo wezeshi mibovu. Angalia madereva wa mabasi yanayowakuta kwa ground.

Kusoma VETA hakutakusaidia lolote kwenye nchi hii, tatizo ni mifumo wezeshi mibovu. Angalia madereva wa mabasi yanayowakuta kwa ground.

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Posts
4,805
Reaction score
17,850
Nenda kasome tu for your own benefits and risks. Ila kwa ground mambo ni tofauti sana.

Kasomee ufundi unaotaka wewe, ila the moment umefungua ka kibanda kako tu, hujaanza kuingiza hata senti 5, TRA hawa hapa.

Hata wale walioajiriwa, siku wakikuonesha salary slip zao, utawaonea huruma. Usione waajiriwa wamejichokea ukadhani ni wanaigiza, wewe hujiiulizi ni kwa nini waajiriwa wengi wanaishia kwenye mikopo mikubwa wanayoshindwa kuilipa?

Nchi hii tatizo siyo kusoma au ujuzi, tatizo ni mifumo mibovu inayowabana wale wanaopambana kutokuweza kutoboa. Ukipata ka senti 5, wanataka wachukue senti 3 wewe ubaki na 2.

 
Back
Top Bottom