Kusomea Bachelor Degree ingine

Kusomea Bachelor Degree ingine

Usiangaike kutaka kusoma degree nyingne itumie iyo bacherol yako kupata ajira kam bado haupo katika ajira wizara ya Afya inawahitaji watu kam nying kwa ajir y nutritional public awareness malnutrition moreover unaweza kujiajiri kwa kuanzisha vituo lishe otherwise uende masters degree public health au mastera ya manangement nyingine. Upo sehem sahihi kijana
na mpango wa kusoma master ya public health
 
Hello habari

Nilikua nauliza mtu ambaye ana bachelor degree moja na Advanced level alisoma CBG anaeza soma bachelor ingine ya afya mfano pharmacy , Radiotherapy, MD etc?

And je cheti cha bachelor kinaeza saidia kwenye admission kutokana na hio CBG?

Inawezekana?
Kwa anaehitaji kufanyiwa application (Maombi):

1. Maombi ya mikopo (mkopo) ya elimu ya juu 2023/2024 (heslb) uzoefu upo wa kutosha.

2. Maombi ya Vyuo vikuu na vya kati (online)

3. Joining instructions (maelekezo ya kujiunga) za vyuo vikuu na vya kati pia zinapatikana.

WhatsApp: 0620523897
 
Una uhakika nilikua nacheza 😩😩😃😃😃
Pass mark ulizopata zinaonyesha

Mkulima hupimwa kwa kilimo kikubwa analima na mwanafunzi serious hupimwa kwa marks anapata sio kwa ukubwa wa begi anabeba mgongoni au uniform za shule anavaa

Marks zako hazionyeshi kama ulipania kusoma ziko chini mno kwa fani unaomba
 
Nimesoma comment zote Mimi kwangu hakuna tunayefanana hata.
Kwangu Iko hivi...!
Ndoto yangu ilikuwa kuwa daktari na sasa nimetimiza baada ya miaka kadhaa kupita sikukata tamaa kamwe niliamini ndoto yangu siku moja itatimia na sasa imetikia.

1.Kidato cha sita nilichaguliwa PCM badala ya PCB na shule nilichaguliwa haikuwa na tahasusi ya PCB baba alifariki nikiwa kidato cha tano nikakosa wa kunipambania nihame shule yenye tahasusi ya PCB .Ikabidi nikubali kuendelea na PCM
Kibwagizo "MOYO WA MTU ULIPO NDIPO NA HAZINA YAKE ILIPO"

2.PCM nikafaulu nikachaguliwa kusoma Electronics Engineering.Nikamaliza miaka minne wakati huo ndoto ya udaktari bado Ipo !
"MOYO WA MTU ULIPO NDIPO NA HAZINA YAKE ILIPO"

3.Nikapata kazi kama mhandisi wa vifaa tiba (Medical Electronics Engineer) ,wakati naendelea kufanya kazi nakatafu chuo cha diploma in clinical medicine ,Nilisoma huku ninafanya kazi ya uhandisi haikuwa rahisi lakini nilijinyima muda na starehe nyingine zote.
"MOYO WA MTU ULIPO NDIPO NA HAZINA YAKE ILIPO"
4.Uhandisi pamoja na kuwa ulikuwa unalipa lakini sikuwahi kuufurahi ,.Baada ya kumaliza diploma ya utabibu niliacha kazi ya uhandisi na kwenda serikalini na kuajiliwa kama" CLINICAL OFFICER"
Niliacha mshahara wa TSH 1.0M na kwenda kwenye mshahara wa TSH 0.5M
Wengi walinicheka sana na ndugu wengine waliniona tahira na wakaacha kuongea na Mimi ,.Wakasahau nilivyowalilia iliwanisaidia kuhamia shule yenye PCB wanakataa
"MOYO WA MTU ULIPO NDIPO NA HAZINA YAKE ILIPO"
5.Nikiwa kazini niliomba ruhusa ya kwenda kusoma MD (5yrs) wakati huo nina mwaka mmoja kazini kama AFISA TABIBU (CLINICAL OFFICER ).Afisa utumishi akaniambia hawezi kuniruhusu kwakuwa sijatimiza vigezo ,nikaambiwa nitoe shilingi milioni 1 aniruhusu .Nikaenda banki kukopa TSH 12M nikachukua TSH 1M nikampa Afisa utumishi .TSH 10M zote nikalipa ada ya miaka 2,miaka mingine iliyobaki nitajua mbele ya safari
"MOYO WA MTU ULIPO NDIPO NA HAZINA YAKE ILIPO"

6.Kwa shida sana MD nikamaliza ,nikaenda Internship nikarudi kazini nikapewa kwanza kuwa Mganga mfawidhi wa hospitali

"MOYO WA MTU ULIPO NDIPO NA HAZINA YAKE ILIPO

7.Kwa sasa ni PhD (candidate) , Neuroanatomy
Duh inahitaji moyo sn aisee wew noma big up mkuu
 
Hello habari

Nilikua nauliza mtu ambaye ana bachelor degree moja na Advanced level alisoma CBG anaeza soma bachelor ingine ya afya mfano pharmacy , Radiotherapy, MD etc?

And je cheti cha bachelor kinaeza saidia kwenye admission kutokana na hio CBG?

Inawezekana?
Kwa bachelor kwa sasa ni ngumu, kwa muongozo wa TCU bachelor degree wanaagalia diploma na advance. Cha kufanya kagonge Msc of Public Health, au Msc Biochemistry, na zingine nyingi.
 
Hello habari

Nilikua nauliza mtu ambaye ana bachelor degree moja na Advanced level alisoma CBG anaeza soma bachelor ingine ya afya mfano pharmacy , Radiotherapy, MD etc?

And je cheti cha bachelor kinaeza saidia kwenye admission kutokana na hio CBG?

Inawezekana?
admission ya bachelor inategemea cheti cha a-level,
MD ni lazima pcb kwa guidelines za sasahivi labda bachelor environmental health science
 
Nina swali MD mwanamke anae tumia uzazi wa mpango (njiti) na hataki kutoa wakati anasumbuliwa sana na magonjwa hata painkiller hazifanyi kazi mnatumia njia zipi ?

Ajaribu kitanzi! Maana kijiti kina hormone nyingi kuliko copper ya kitanzi.
 
Hello habari

Nilikua nauliza mtu ambaye ana bachelor degree moja na Advanced level alisoma CBG anaeza soma bachelor ingine ya afya mfano pharmacy , Radiotherapy, MD etc?

And je cheti cha bachelor kinaeza saidia kwenye admission kutokana na hio CBG?

Inawezekana?
Ungekuwa ulaya chap chap.. Ila hapa nchi ya maziwa na 🍯... Michakato mirefu
 
aisee watu wasije jaribu hii kitu kabisa miaka hii .
your very lucky few who made it..
MD MIAKA HII AMNA ISSUE AISEE. AMNA viJIWE, SPECIALIST KIBAO.
IN 10 YRS MAMBO YATAKUWA OVYO. GOVERNMENT EMPLOYEMENT YOU HAVE TO WAIT FOR 3-4 YEARS. NA KWENDA KUSOMA NI MORE Years. WATU WANAELIMU KUBWA SANA MTAANI. MD SIO COURSE YA KUINVEST. masters yake tu ada ni 10 plus na heavy weight
. ENGINEERING Is the way.
Jaribu kusoma uelewe alichomaanisha, hata ingekuwa huo u MD unaissue au hauna issue yy ni kitu alikipenda moyoni mwake na alisoma kuupa moyo wake amani na utulivu kuwa imekipata kitu alichokuwa akikihitaji... ndio maana walidiriki kukopa na kuhonga ili atimize haja ya moyo wake... unaposema MD haina issue ni kwa upande wako sio kwa mwingine. Kila mtu afanye kile anachokipenda kwa uwezo wake Kila mtu na maisha yake
 
Mimi siku zote napenda kujiweka katika nafasi ya mtoa uzi. Hivyo, nikuulize unatamani kufanya hivyo kwa msukumo upi? Wa kupata malipo mazuri au kwa sababu ya passion?

Kama jibu ni kwa sababu ya passion basi utalazimika kuanzia Diploma. Kisha uingie Shahada nk.

Kama jibu ni kwa sababu ya hela na Status, piga chini mpango wako.

Anyway, karibu sana katika ulimwengu wetu.
 
Back
Top Bottom