Kusomesha mtoto mpaka ajitegemee ni 20 years. Kama huna Assets Usijiingize gharama mapema ukashindwa kufanya maendeleo mengine kama ujenzi

Kusomesha mtoto mpaka ajitegemee ni 20 years. Kama huna Assets Usijiingize gharama mapema ukashindwa kufanya maendeleo mengine kama ujenzi

MELEKAHE

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2023
Posts
2,230
Reaction score
8,337
Hizi shule za chini hakikisha anasoma ili apande darasa, na ajue hisabati na kingereza na mtafutie tuition nzuri hata kama akisoma cheap schools , ana nafasi ya kuwa vizuri kwenye elimu kama akiyajua vizuri hayo masomo mawili tu.

Usije ukajikuta kwa miaka 20 mfululizo unaingia madeni kwa watu tofauti tofauti kila mwaka kwa ajili ya kulipa school fees tu huku wewe unakula dagaa tu kwenye nyumba mbovu ya kupanga

Kama kipato chako kidogo chini ya milioni mbili kwa mwezi achana kabisa shule za gharama kwa watoto wako. Kumbuka katika Maisha Kusomesha watoto ni almost miaka 20… hapo katikati lazima ujenge, ununue properties, uwekeze katika passive income, uende holidays/retreats, uwe na gari, utimize majukumu ya familia na jamii.

Na bado Elimu useful katika maisha mostly inapatikana kwenye college nzuri/ institutions au Vyuoni, ndio maana nasisitiza wazazi wafocus kwenye uwekezaji wa ada kubwa mtoto akifika katika Elimu ya chuo au elimu ya technical skills. baada ya mtoto kuhitimu kidato cha 4 au 6.

Mtoto aliyesoma feza kuanzia primary mpaka secondary kisha chuo akaenda kusoma chuo kibovu, na kozi mbovu. anakosa advantage kwenye ushindani wa ajira ukimlinganisha na mtoto aliyesoma kayumba kisha akapata CPA. yeye anakuwa na advantage kwenye soko la ajira sababu ya hizo CPA bila kujali amesoma shule za kayumba.

Soko linatazama ulichopata mwisho wa safari kama riadha vile, halitazami kama zamani ulisoma feza
 
Wanaofanyaga kinyume na ushauri wako Akili zao Huwa ni ndogo

Maisha yenyewe mfumo wake ni kamali so yanini kujikamua mihela kibao kwaajili ya kumsomesha mtoto ktika shule za gharama wakati Maisha yako ni tia maji

Hizo pesa ni vyema utumie kuwekeza katika biashara ili hata ikitokea mtoto akasoma then kupata kazi ikawa changamoto basi Angalau utaweza kumuajiri ktika biashara yenu ya nyumbani na ikawa ni fursa kwako ya kujiingizia kipato
 
1. Elimu ya msingi na secondary inatosha
2. Elimu ya chuo bila connection inageuka kuwa mwiba kwa mhusika maana inampa matumaini hewa
3. Kupoteza miaka mingi shule ukirudi mtaani unakuta agemate wako walio acha shule wako mbali
4. Ajira nyingi za wasomi ni utumwa kuishi kwa kufunga mkanda
5. Ukigundua kipaji cha mwanao na kukiendeleza kinatoa uhakika wa maisha kuliko elimu ya chuo
 
🤣🤣🤣🤣

100 percent facts.
 
Kusomesha mwanangu shule nzuri ni ndoto yangu,nikimpeleka kayumba hata moyo wangu hauwezi kuwa na Amani!!

Upo sahihi. Ni jambo zuri kama kipato chako kinaruhusu mambo mengine yanaenda pia
 
1. Elimu ya msingi na secondary inatosha
2. Elimu ya chuo bila connection inageuka kuwa mwiba kwa mhusika maana inampa matumaini hewa
3. Kupoteza miaka mingi shule ukirudi mtaani unakuta agemate wako walio acha shule wako mbali
4. Ajira nyingi za wasomi ni utumwa kuishi kwa kufunga mkanda
5. Ukigundua kipaji cha mwanao na kukiendeleza kinatoa uhakika wa maisha kuliko elimu ya chuo
Tatizo kila Mzazi hasa hao wa 1950s, 1960s hawaamini ktk kipaji cha mtoto. Wanataka mtoto awe Doctor
 
Back
Top Bottom