KERO Responded Kusubiri Basi la Mwendokasi kituoni dk 60 - 120 ni kero kubwa na inapoteza maana ya mwendokasi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Ujumbe huu uwafikie wenye mamlaka wa kutoa maamuzi juu ya usafiri wa Mwendokasi.

Hali ilivyo sasa inatisha na kuzidi kuwa mbaya siku hadi siku kutokana na kuwa na mabasi machache yanayofanya kazi.

Hali hii inalazimu watu kukaa zaidi ya saa moja hadi mbili kusubiria magari machache hayo ambayo kuweza kuingia ndani yake ni bahati nasibu na vurugu.

Tunapendekeza Serikali kufanya maamuzi ya haraka iwezekanavyo kuingia ubia na watu binafsi wenye basi aina ya TATA-Marcopolo kusaidia kubeba abiria wa moja kwa moja wakitumia barabara za mwendokasi.

Idadi kubwa ya abiria (nimefikiwa inaweza kuwa 80%) wanatoka mwanzo hadi mwisho wa vituo kama vile Kimara - Gerezani, Kimara - Morocco, Kimara - Kivukoni.

Labda hali hiyo inaweza kupunguza msongamano wa abiria kwenye vituo katika adha ya usafiri kwa kipindi hiki wakati tukisubiri mwekezaji mpya ambaye hatujui atakuja lini.

NI VYEMA KUFANYA MAAMUZI YA BUSARA KWA HARAKA ZAIDI AMBAYO HAYAHITAJI PESA YA BAJETI YOYOTE.
BARABARA NI YA WATANZANIA, NA ITUMIKE KWA AJILI YA WATANZANIA.
1753017252932.jpg
Pia soma ~ Albert Chalamila: Mabasi 99 yataingia Agosti 15, mengine 200 yataingia Oktoba 1, 2025
 
Nanyie hmuwez kuish bila mwendokas s mnunue yenu au mpande usafir mwingn kelele za ninin kila sku
 
Poleni waTZED. Haya mambo kipindi cha uchaguzi yalikuwa yanasawazishwa, ila sasa hivi inaonekana mnadharauliwa kiasi gani
 
Ujumbe huu uwafikie wenye mamlaka wa kutoa maamuzi juu ya usafiri wa Mwendokasi.

Hali ilivyo sasa inatisha na kuzidi kuwa mbaya siku hadi siku kutokana na kuwa na mabasi machache yanayofanya kazi.

Hali hii inalazimu watu kukaa zaidi ya saa moja hadi mbili kusubiria magari machache hayo ambayo kuweza kuingia ndani yake ni bahati nasibu na vurugu.

Tunapendekeza Serikali kufanya maamuzi ya haraka iwezekanavyo kuingia ubia na watu binafsi wenye basi aina ya TATA-Marcopolo kusaidia kubeba abiria wa moja kwa moja wakitumia barabara za mwendokasi.

Idadi kubwa ya abiria (nimefikiwa inaweza kuwa 80%) wanatoka mwanzo hadi mwisho wa vituo kama vile Kimara - Gerezani, Kimara - Morocco, Kimara - Kivukoni.

Labda hali hiyo inaweza kupunguza msongamano wa abiria kwenye vituo katika adha ya usafiri kwa kipindi hiki wakati tukisubiri mwekezaji mpya ambaye hatujui atakuja lini.

NI VYEMA KUFANYA MAAMUZI YA BUSARA KWA HARAKA ZAIDI AMBAYO HAYAHITAJI PESA YA BAJETI YOYOTE.
BARABARA NI YA WATANZANIA, NA ITUMIKE KWA AJILI YA WATANZANIA.
Pia soma ~ Albert Chalamila: Mabasi 99 yataingia Agosti 15, mengine 200 yataingia Oktoba 1, 2025
Huo si mwendo kasi bali mwendo hasi wanangu. Hamjastuka siyo?
 
Back
Top Bottom