Kutafuta pesa na kuzipata ni swali la lazima kwenye mtihani wa mwanaume 😊 ukiliruka basi utafeli mtihani wote

Kutafuta pesa na kuzipata ni swali la lazima kwenye mtihani wa mwanaume 😊 ukiliruka basi utafeli mtihani wote

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
471
Reaction score
1,217
KUTAFUTA PESA: MTIHANI WA LAZIMA KWA MWANAUME.

Kwenye mtihani wa maisha ya mwanaume, kuna maswali ya hiari na la lazima, Swali la lazima ni moja tu: Kutafuta pesa na kuzipata.

Hili si swali la kuahirisha kwani ukiliruka basi umefeli mtihani wote.

Heshima nyumbani, sauti kwenye jamii, na hata amani ya nafsi mara nyingi hufungamana na uwezo wa mwanaume kumudu majukumu yake.

Jamii haitakuuliza ulisoma shule gani bali itakuuliza una maisha mazuri ki uchumi?

Lakini mtihani huu una sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ni kuitafuta. Hapo ndipo jasho, maarifa, na nidhamu vinapimwa. Sehemu ya pili ni kuipata na kuitunza. Wengi hufaulu kuitoa jasho lakini hufeli kuisimamia kwani pesa bila hekima ni kama maji kwenye kikapu.

Kwa hiyo kijana, usilale. Soma, fanya kazi, jenga ujuzi Kwa sababu kwenye karatasi ya mwanaume, ukikosa alama kwenye swali la pesa, wastani wako wote unaporomoka.

#Malenga wa Kiha
#Mwanasayansi Saul kalivubha.
 
Back
Top Bottom