Kutambulishwa ukweni na kutolewa mahari sio uhakika wa ndoa

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102

Umewahi kupeleka mahari kisha hukurudi tena na ukaachana na ndoa? Umewahi kutolewa mahari na muoaji hakurudi tena? Umewahi kushuhudia mahari imetolewa na ndoa ikafia njiani?

Kwa kuwa tunafahamu mahari ni hatua ya mwisho kabisa kuelekea ndoa kipi kinaweza kusababisha mahari kutolewa na kupokelewa na ndoa isifanyike kwa mahusiano kufa?

Pia soma:

Ushuhuda wa mdau

 
Nimewahi mimi binafsi,, nilitoa mahari, na kumvalisha pete baada ya miezi mitatu alinipigia kwa jeuri na kunitusi kisa nimepeleka mbele tarehe ya harusi hapo ndipo ukawa mwisho wa uchumba wetu, mama yake alichanganyikiwa alitaka wamuombee msamaha ila mimi sikuhitaji suluhu nae tena.
 
Mbona hilo lilikuwa jambo dogo sana! Huyo mwanamke alikuwa pasua kichwa.
 
Mwamba karata yako uliicheza vema sana hongera............
 
Safi sana, atajifunza
 
Duuuu mahari ilirudishwa au?
 
Mimi nmeshuhudia kabsa... classmate wangu (ke) alileta kadi ya mchango wa harusi home kwa ajili ya hafra ya ndoa, lakin siku chache mbeleni bwanaharusi mtarajiwa alipenyezewa habari kuwa mkewe mtarajiwa kuna mtu anammega....

Bwana harusi akapatiwa adi ushahidi wa pic,jamaa alisamehe kila kitu...wazazi wa bint walipata aibu sanaa.

Ila sema kuna mabint wanabahati zao...baada ya miezi kadhaa akatokea mwamba juzi tu ndo tumepiga mpunga wa ndoa.
 
Hawata fika mbali,,ipo siku utakuja leta ushuhuda humu
 
Heri uchumba uliovunjika kuliko ndoa ya mateso. Watu wanapigwa chini michango ishachangwa na paroko anaandaa misa, ndio iwe kutambulishwa?
 
Hata ndoa sio uhakika wa kubaki pamoja daima.....
 
Mwamba anamjua vizuri huyo binti lakini? Isije kuwa ameuziwa mbuzi kwenye gunia.
 
Yes imenitokea mimi binafsi nilitolewa mahari mwaka juzi na pete nikavalishwa. Haikuwa riziki miezi 8 baadae tukaachana na kila mtu akashika hamsini zake. Upande wa kiume hawataki kuchukua mahari zao ingawa tunafanya jitihada sana wazichukue. Kweli kabisa mahari sio ndoa wakuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…