Kutana na mzee wa miaka 64 anayependa kuvaa viatu virefu vya kike

Kutana na mzee wa miaka 64 anayependa kuvaa viatu virefu vya kike

Dawa yake ni kumpelekea watoto wa kihuni chocho wamrambe viboko vingi hadi ajoe ndo atakoma
 
Tembeeni muone mengi nchi za Papua New Guinea,Bahamas,Scotland,Bhutan n.k wanaume kuvaa ni vazi la kawaida inaitwa Kilt tartan
Utamaduni wako usiulazimishe kwa mwenzio hata wewe kuna nchi ukienda ukivaa suruali watakushangaa kidogo nenda Afghanistan na Bhutan.
Hapa kwetu wamasai wa kule mbugani bado wanavaa lubega lakini vile tumewazoea hatuwashangai lakini ni vazi la heshima sana.
Picha angalieni mfalme Charles 111 wa Wingereza kavaa Skate utasema ni shoga?.Picha ingine huyo sio mmasai ila kavaa vazi kwa kwetu ni la kimasai akienda sehemu zingine watamshangaa.
Uganda kuna shule ya sekondari imejengwa na wa Scotland wanafunzi wa kiume wanavaa skate je utasema wanafunzi ni mashoga.Halafu mtofautishe kati ya skate na kilt tatan.
Skate haina masharti ya urefu inaweza valiwa juu ya magoti lakini Kilt tartan sharti iwe ndefu.
Mbona waarabu wanavaa kikoi na msuli hamsemi.
Kabla ya kuletewa nguo na wazungu babu zetu walikuwa wanatembea kwa magome ya miti na uchi hapo mtasemaje?.
Nenda kwa Wahadzabe kidogo wanavaa ngozi za wanyama kufunika sehemu nyeti lakini wewe ukienda umevaa suti watakuona waajabu sana kijiji kizima watakuzunguka.Acheni ushamba.
Kwa Japan hili vazi linaitwa kimono.
Hawa hawa ndio wamewafundisha nyie waafrica kuvaa nguo sasa wanaweka utamaduni wao mnaona akili zimehama.
Wengi wanao comment humu hawajawahi hata kuvuka nchi za ng'ambo ndio maana ushamba umewajaa.
Kungekuwa na uwezekano wazungu waje watuambie haya nguo tulizowafundisha kuvaa na kutengeneza wote humu tungetembea uchi.
Nimeshawahi ona kwenye mkutano mmoja wa nchi zinazoendelea ulifanyika Arusha AICC mwaka 1977 wengi humu mlikuwa hamjazaliwa mimi nilikuwa chipukizi wale wa CCM Std5 alikuja raisi wa Papua New Guinea mtu mweusi kama sisi chini kavaa sketi juu kapiga koti na tai huku wana toast wine kwenye party mtasema alikuwa hamnazo?
Nafikiri kinachowashangaza wengi siyo sketi, ni viatu /high heels.

But, asante kwa kutuelezea kuhusu tamaduni tofauti tofauti duniani, nakubaliana na wewe kwamba mavazi kama magauni na kilts/skirts ni sehemu za tamaduni za jamii mbalimbali.

Kwa mark ambaye ni raia wa marekani mavazi yake siyo sehemu ya utamaduni wa nchi yake bali ni preference yake binafsi.

Mark 1.jpg

Mark 2.jpg
 
Kama waafrika, tujivunie sana tamaduni na maadili yetu, mambo yanayoendelea huko duniani kwingine yanastaajabisha.

Mark Bryan ni Injinia, mume na baba wa watoto watatu. Anapenda kuvaa viatu virefu vya kike na sketi kwa sababu vinamvutia na anaamini vinampendeza. Mkewe na watoto wake wamemkubali na hali yake kama alivyo.

Mbali na taaluma yake, Mark pia ni kocha wa mpira wa wanaume na hayuko kwenye jamii ya LGBTQIA kwa sababu maisha yake yote amekua akivutiwa kimahusiano na wanawake na si wanaume.

Unadhani nini kinaweza kusababisha hali hii?

Ungekua mtoto wake ungefanya nini?

Ukikutana naye barabarani, utamshauri au kumuambia nini?

View attachment 3240168
View attachment 3240169


View: https://youtu.be/1kKFXI52m1Q?si=oT-eEvo1aosv2tEh

View attachment 3240170
View attachment 3240171

Mnajua kupush agenda yenu!
 
Nafikiri kinachowashangaza wengi siyo sketi, ni viatu /high heels.

But, asante kwa kutuelezea kuhusu tamaduni tofauti tofauti duniani, nakubaliana na wewe kwamba mavazi kama magauni na kilts/skirts ni sehemu za tamaduni za jamii mbalimbali.

Kwa mark ambaye ni raia wa marekani mavazi yake siyo sehemu ya utamaduni wa nchi yake bali ni preference yake binafsi.

View attachment 3241062
View attachment 3241063
Kama ni Mmarekani hilo sina ubishi na wewe nakuunga mkono ila cha muhimu tu nilitaka kuonyesha wengine kuwa tamaduni za mavazi zinatofautiana sana.
 
Back
Top Bottom