Boutafrica
JF-Expert Member
- Dec 11, 2014
- 974
- 2,106
Na:A.M KITOTA
ASWHAABUL KAHF: A SCIENTIFIC APPROACH
Ni takribani karne 14 sasa tangu hali za watu wa pangoni zilipofunuliwa ndani ya Qur’an.
Na ni hivi punde tu katika kizazi hiki (mwaka 1923, 20th century) ambapo mwanamiamba wa Kijodan Rafiq Wafa Ad-Dajani alipogundua mahali ambapo panga hilo lilipokuwepo (kuwa ni eneo la Jordan lijulikanalo kama Rahib).
As we know, vijana hawa walikimbia udhalimu na ukafiri wa Mfalme Deconus na watu wake na Allah (subhaanahu wata'ala) akawahifadhi kwenye pango hilo.
Kwa kuwa idadi yao haikubainishwa wazi ndani ya Qur’an, kunakhtilafu juu ya idadi yao miongoni mwa Wanazuoni. (na Allah subhaanahu wata'ala najua zaidi).
Wengi katika Wanazuoni wanapendekeza kuwa, idadi ya vijana hao ilikuwa ni vijana saba (7) na mbwa wao akiwa ni wanane wao. Rejea Surat AL Kahf, 18:22.
Lakini, kwa mujibu wa ugunduzi huo
Makaburi manane ndiyo yalioonwa (yaliyokutwa) ndani ya pango hilo. Wakati pembeni ya mlango wa pango hilo, lilikutwa fuvu la mbwa huyo. Hali iliyoonyesha kuwa, mbwa huyo siye aliyezikwa kwenye hilo kaburi la nane.
Kama kawaida ya Qur’an, sura ambazo zimetiliwa mkazo zaidi, ndizo huwa zimebeba miujiza mingi zaidi na mikubwa mno. Miujiza hiyo ni pamoja na ile miujiza ya Kisayansi, Kiponyo (kitiba), Kihistoria n.k.
Miongoni mwa Sura hizo ni pamoja na Surat Kahf, Surat Baqarah, Surat Ikhlas, Surat Yaasin, Surat Mulk, n.k.
Specifically, miujiza ya Kisayansi ni miongoni mwa dalili zilizokadiriwa na Allah (subhaanahu wata'ala) kwenda na wakati mpaka siku ya kiama, na ndiyo maana you will see that, hakuna kitu hata kimoja kinachogunduliwa leo hii na Sayansi ya sasa kikawa hakikutajwa moja kwa moja au hakijaonyeshwa kanuni au misingi yake ndani ya Qur’an.
Tofauti na ilivyo kwenye vitabu vingine vya Dini kama:
Tanaq na Talmud - vya Wayahudi, Vedas, bhagwad Geeta na upanishad vya Wahindu, Guru Grand Sahib cha Wasikhi, Daster na Avester vya Wazoroaster, Pali na Sanskrit vya Wabudha, Biblia ya Wakristo n.k, Wanazuoni wa Kiislam wanafahamu idadi ya sura, aya, maneno mpaka herufi za kitabu chao kitakatifu kilingana na kutofautiana kwa mitindo ya qira'a toka eneo moja mpaka lingine.
Kati ya hizo aya zote za Qur’an, takribani zaidi ya aya 1160 (takribani karibuni 20% ya aya zote) zinazungumzia taaluma mbalimbali za Sayansi kama dalili na ishara za uwepo, ukubwa na utukufu wa Allah (subhaanahu wata'ala).
Kama nilivyotangulia kusema kuwa, sura zikizosisitizwa zaidi huwa ndiyo zimebeba miujiza mikubwa na mingi zaidi.
Hebu tuangalie baadhi tu ya miujiza ya Kisayansi iliyomo ndani ya Surat Al Kahf kama moja ya sura zikizosisitizwa zaidi kusomwa, hasa katika siku ya (ijumaa).
Nafasi ya panga hilo sambamba na uelekeo wa mwanga wa Jua unaoliangukia vilichunguzwa kwa umakini zaidi. Hasa eneo ambalo mwanga ulikuwa unaingilia ndani ya pango hilo.
Ilibainika kuwa, uelekeo wa kusini wa mwanga ulikuwa ni kusini magharibi. Kama mtu akisimama ndani ya pango hilo katika muda wa asubuhi, Jua linapiga kulikimbia pango kuelekea upande wa kulia na mwanga wake unapita mbele ya mtu huyo na kuonyesha kismamo chake na mpaka wake.
Jua linapokuwa kwenye kilele chake (kwa mfano mchana), hakuna mwanga unaoingia ndani ya pango hilo.
Lakini, Jua linapoelekea kuzama, wakati wa jioni, baadhi ya mwanga wake unapenya na kuingia ndani ya pango hilo kupitia kwenye uwazi wa pango hilo.
Jambo hilo la hakika lililogunduliwa linawiana ana kwa ana na maelezo ya Surat Kahf, 18:17.
Huo ni muujiza mkubwa sana kwetu sisi. Unaweza kujiuliza ilikuwaje hawa vijana wakakimbilia kwenye pango hili, lililopo eneo hilo? Na pia, waweza tena kujiuliza ilikuwaje wakaenda kujilaza katika eneo ambalo hawatapigwa na mwanga mkali wa Jua kwa kipindi chote hicho cha miaka 309?
Bila shaka, mwisho wa tafakuri yako ya kina itaangukia hapa: *ni Allah (subhaanahu wata'ala), mjuzi na mwenye hekima, ndiye aliyewakadiria kulikimbilia pango hilo na kulala sehemu hiyo ambayo haikuwa ikifikiwa na Jua kali la mchana kwa miaka yote hiyo*
Muujiza mwingine uliopo hapo ni very scientific: kama Jua lingekuwa linawapiga, ingeliwachukuwa muda mfupi sana kufa, kitokana na kapoteza maji ya mwili (au body fluid) kwa njia ya *mnururisho*
Joto lao la ndani ya miili (core body temperature) lingelipanda mara dufu kiasi cha kuchemsha kimiminika hicho cha mwili, hali ambayo ingelipelekea hali hiyo ya mnururisho na hatimaye mamilioni ya seli za miili yao, yangelipoteza maji na kusinyaa kisha seli hizo kufa kabisa hali ambayo kimsingi ingelipelekea kusimama kwa shughuli za kimetaboli za seli hizo na at the end *serious death*
Na katika aya ya 18 ya sura hiyo (Kahf), Allah (subhaanahu wata'ala) anatujuza kuwa, alikuwa akiwageuza *kulia na kushoto*
*What is the scientific wisdom of turning them kulia na kushoto?*
Kwa mujibu wa taaluma za sasa za anatomia na fiziolojia, it's obvious kuwa, wasingelikuwa wanageuzwa, kwanza, wasingelikuwa na mzunguko wa moja kwa moja wa damu.
Damu yao ingelikuwa inazunguka taratibu sana kwenye maeneo yaliyogusa chini. Hali hii ingelisababisha damu kuganda, hasa katika *peripheral areas* (maeneo ya mikononi, mguuni na kwenye ubavu uliogusa Chini). Hii ingelipelekea kutokea kwa madonda kwenye ngozi, maarufu kama *sores* au *pressure sores*
Tatizo hili lingesababishwa zaidi na kukosekana kwa mijongeo ya kiumbo (mijongeo ya viungo vya miili yao). Kwani, hii ndiyo husaidia safari ya damu kutoka kwenye moyo na kwenda sehemu mbalimbali za mwili na kutoka sehemu mbalimbali za mwili na kurudi kwenye moyo.
Tatizo lisingeishia hapo, ingelifikia hatua hata myoyo yao ingelipata matatizo makubwa sana ya mapigo. Hali hii ingelisababisha kushindwa kwa moyo kufanya kazi na hivyo, *serious death*
Huyu ndiyo Allah (subhaanahu wata'ala), mjuzi na mwenye hekima. Na kwa inavyoonekana, namna ambavyo alikuwa akiwageuza vijana hao, ni sawa na anavyotugeuzaga sisi usiku au mchana tukiwa tumelala.
Mawazo haya yanatokana na ukweli kuwa, vijana hawa walikuwa wamelala (deep sleep) katika hali ambayo, ni takribani sawa na tulalavyo sisi, isipokuwa mambo machache.
Hivyo, kama Allah (subhaanahu wata'ala) asingelikuwa anatugeuza geuza wakati wa usingizi, ni dhahiri kuwa, madhara ambayo yangeliwakuta vijana hao, yaliyoainishwa hapo juu yangelitutokea (ijapokuwa Allah subhaanahu wata'ala hashindwi kuyazuia yasitokee hata kama asingelikuwa anatugeuza)
Hii ndiyo sababu, Allah (subhaanahu wata'ala), somewhere else ndani ya Qur’an anatujuza kuwa, hata kulala kwetu pia ni ishara kwetu ya uwepo, ukubwa na utukufu wake. (Rejea Surat Ar-Room, 30:23).
Anaother scientific notion (sign) ambayo inaonekana kwa uwazi katika kisa hiki ni katika Surat Al Kahf, 18:11.
Katika aya hiyo, Allah (subhaanahu wata'ala) anatujuza kuwa, aliwaziba masikio yao. *And hence, what is anatomical and physiological implications of this?*
*Modern science can reveal this: (refer Surat Fussilat, 41:52) ambapo Allah (subhaanahu wata'ala) anasema atawaonyesha waliokufuru dalili za uwepo, ukubwa na utukufu wake ndani ya nafsi zao (miili yao):*
Kiembryolojia, itafahamika kuwa, masikio huanza kujuwa na kuendelea mapema zaidi kabla ya macho. Na kazi ya masikio huanza mapema mara tu baada ya mtoto kuzaliwa, tofauti na ilivyo kwa macho, ambayo huanza kazi baadaye. *hii ndiyo sababu, you can see, aya nyingi sana za Qur’an zitajazo ogani hizi za fahamu, masikio hutajwa kwanza, kisha ndiyo yanatajwa macho*
On the other side, masikio ndiyo kiunganishi kati ya mwanadamu na Dunia yake. Lakini pia, kifiziolojia, ndiyo ogani pekee ambayo huwa ipo hadhiri (active) muda wote, hata mtu akiwa amelala usingizi, ikilinganishwa na ogani zingine za mwili. *Huwa hayalali wala hayapotezi utayari.*
Kwa hiyo, Allah (subhaanahu wata'ala) alipowakadiria watu vijana hawa kulala kwenye pango hilo kwa miaka takribani 309, aliwaziba masikio yao, ili yasiwe dhahir (active) wakati wa usingizi huo mzigo sana. *(subhaanal llah, huyo ndiye mjuzi mwenye hekima).*
Muujiza wa mwisho ambao nimeona niu-adress ni total period of time waliokaa vijana hao humo pangoni in relation to modern astronomical point of view.
Katika Surat Al Kahf, 18:25, imeelezwa kuwa, vjana hao walikaa humo pangoni kwa muda wa miaka 300, wakazidisha miaka mingine 9.
Lets ask ourselves, ni kwa nini Allah (subhaanahu wata'ala) aseme walikaa miaka 300 na wakazidisha miaka mingine 9? Kwa nini asiseme moja kwa moja miaka 309?
Hii inatufanya tufikiri zaidi, kama aya nyingi sana za Qur’an zinavyotutaka tuwe wenye kutafakari na kufikiri kuhusu dalili mbalimbali za uwepo, ukubwa na utukufu wa Allah (subhaanahu wata'ala).
Astronomia ya sasa inaweza kudadavua jambo hili la Hakika kwa kutumia mitazamo mikubwa miwili:
Kwanza:
Miaka ya Jau 300 ni sawa ina wiana na miaka ya Mwezi 309. Misingi hii inatokana na kanuni iliyoainishwa hapa Chini:
Mwaka mmoja wa Jua ni sawa na takribani mwaka wa mwezi 1.03.
Na pili:
Mwaka mmoja wa Jua una siku 365.242199
Mwaka mmoja wa mwezi una siku 354.36705
Miaka 9 ya Jua ni sawa na 9x huo mwaka mmoja wa Jua, ambaopo tunapata 3287.179791.
Na miaka 9 ya mwezi ni sawa na 9x huo mwaka mmoja wa mwezi, ambapo tunapata 3189.30345
Hivyo, miaka 300 ya Jua imejumuisha siku 109572.6597, wakati miaka 300 ya mwezi imejumuisha siku 106310.115. Na tofauti kati ya siku hizo ni siku 3262.54.
Idadi hizi za siku zinakaribia zaidi kwenye miaka 9 ya Jua kulikoni kwenye miaka 9 ya mwezi.
Hii inamaana kuwa, vijana hao wa pangoni walikaa miaka 300 ya Jua.
Hii inamaana kwamba, walikaa miaka 300 ya mwezi kujumlisha miaka 9 ya Jua.
Hiyo miaka 300 inabakia kuwa kama ilivyo (constant), na hilo ongezeko linakuja kutokana na matokeo ya tofauti kati ya dhana ya miaka ya Jua na miaka ya mwezi. Kwa mantiki hiyo, ongezeko ni la miaka 9 ya Jua.
Hiyo ndiyo sababu Allah (subhaanahu wata'ala) hakutaja kwa pamoja kama miaka 309 badala yake akataja miaka 300 kisha wakazidisha miaka 9.
Hitimisho
Hayo ndiyo makadirio ya aliyetukuka, mwenye nguvu, mwenye ujuzi. (Surat Yaasin, 36:96).
Na makadirio hayo kwa hao vijana wa pangoni yanajumuisha:
Kuanzia mawazo waliyoyapata ya kukimbilia kwenye pango hilo, kulala upande na sehemu ya pango ambayo mwanga mkali wa Jua haupigi, huyo mbwa kuwafwata (ili kuwalinda), kuwalaza na kusimamia matendo yao yote ya kifiziolojia bila ya kula wala kunywa, tena kwa kipindi chote hicho cha muda, bila ya hata kushambuliwa na wadudu mbalimbali kama vile Microbes (fangasi, bakteria, virusi, virion, prion au baadhi ya protozoa) na wengine kama mchwa n.k.
Wasalaam.............
*Rejea zaidi kuhusu miaka ya Jua na Mwezi (solar and lunar years)*:
Mlivo. Qur’an prior to Science and Civilization. 2001. Ukurasa wa 40-60.
*Rejea zaidi kuhusu mukhtasari wa historia ya vijana hao wa pangoni*
Yusuf AL Hajj Ahmad. The Unchallengeable Miracle of the Qur’an. Ukurasa wa 94.............. *Surat Al Alaq, 96:2 na Surat Al Alaq, 15-16: Mtazamo wa Ki-embryolojia