Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 373
- 829
Ndugu Watanzania!
Juzi nilihoji iweje Mhe. Godbless Lema atekwe ndani ya Ndege taarifa zake zisijulikane? Hapa nimetumia neno hili kuwa alitekwa kwa sababu hakuna maelezo sahihi ya kuelezea ukamataji wa aina ile zaidi ya utekaji.
Akiwa katika Maria Space, Lema ameeleza jinsi alivyochukuliwa akiwa ndani ya Ndege ya ATCL pale Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Arusha wiki iliyopita.
Maelezo ya Lema ni kuwa purukushani za kumkamata wakati akiwa Ndani ya Ndege kabla hajashuka zilishuhudiwa pia na abiria na wahudumu wa Ndege (Air Hostesses). Anaeleza kuwa hakuna hata mmoja kati yao aliyejali kwani kila mmoja alikuwa anapisha kuwahi kushuka.
Tukio la Ali Mohamed Kibao kutekwa ndani ya basi la Tashriff Luxury Coach hata kesho yake kukutwa akiwa mauti kule Ununio lingewashtua abiria na wafanyakazi wa ile Ndege ya ATCL. Lakini haikuwa hivyo kwao, ilikuwa ni biashara isiyowahusu. Tulitarajia haya yangefanyika:
1. Wahudumu wa Ndege wangehoji iweje watu wamvamie mtu ndani ya Ndege bila hata ya kuwasiliana na uongozi wa Ndege?
2. Wahudumu wa Ndege wangempatia taarifa hizo Rubani Kiongozi ambaye naye angetoa kauli yake.
3. Uongozi wa Ndege ungetoa taarifa kupitia ama kwa agenti wa Lema au ingetangazwa pale mapokezi kuwa abiria huyo ameitwa kwa mahojiano na mamlaka ili kuwatoa hofu watu waliokuwa wanamsubiri.
4. Abiria wangepiga picha hata za kuiba kuwa kama ushahidi au wangevujisha picha katika mitandao ya kijamii ili umma ujue kuwa Lema amenyakuliwa akiwa ndani ya Ndege.
Lakini pamoja na taarifa kuanza kuenea kuwa Lema haonekani, hakuna hata aliyesema kuwa alikamatwa ndani ya Ndege, si abiria na wala si wahudumu wa Ndege. Wote waligeuka kuwa ni mabubu. Lakini mnafikiri kwa nini kunyakuliwa kwa Lema ndani ya Ndege kuwasumbue abiria na wahudumu wa Ndege?
1. Lema alikuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, hivyo ni mtu maarufu na isingewezekana abiria wote wale na wahudumu kutokumjua.
2. Lema ni kiongozi wa CHADEMA, chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania na hivyo haiwezekani kuwa kati ya hao abiria waliokuwa ndani ya Ndege ile hakukuwa hata na mfuasi wa CHADEMA au angalau ambaye anafuatilia siasa za upinzani au anayewafahamu viongozi au wanachama wa CHADEMA kushindwa hata kutoa taarifa kwa siri.
3. Lema anatumia sana usafiri wa Ndege, kwa hiyo ni mteja wa ATCL. Haiwezekani kuwa kati ya wale wahudumu hakuna asiyemjua. Na kwa hiyo nao ni lazima wanafahamiana na baadhi ya viongozi wa CHADEMA au hata wanachama. Basi wangevujisha zile taarifa. Hata wauguzi na wakunga katika nchi ya Misri walivujisha siri ya Farao ya kuwaua watoto wote wa kiume wa Waisraeli waliokuwa wakiwazalisha. Wakunga wakawaokoa wengi kwa siri akiwemo Musa.
Maswali ya kujuiliza ni haya:
1. Kama Lema angekutwa ameuawa katika Pori la Kisarawe, wahudumu hao abiria waliokuwa ndani ya Ndege ile wangesemaje?
2. Kama Lema atakuja kuwa Waziri Mkuu au Rais wa Tanzania, hao abiria na wahudumu wa Ndege ile watajisikiaje?
3. Hao abiria na wahudumu wa Ndege ile wao wanajiona kuwa wako salama na ndugu zao?
4. Je, wamewahi kujiuliza kama hao wengine waliopotezwa au kuuawa walichukuliwaje?
Je, ukamatwaji wa Mheshimiwa Lema ulikuwa halali? Kama ulikuwa ni ukamatwaji ule ulikuwa halali, ulihalalishwa na nini? Kama ukamatwaji ule ulikuwa haramu, iliharamishwa na nini? Je, ATCL iliunga mkono kitendo cha abiria wake kukamatwa kama ndezi ndani ya Ndege yao?
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 28 Septemba 2024