Rais wetu ndio anayetakiwa kuwa mkali kwa familia yake na kuwaeleza wanamweka mahali pabaya kama kiongozi wa nchi.Labda kama hili hawalielewi.Unless kama Urais wake ni wa Familia yake.
Wewe wasema baba awakemee watoto, wakati yeye ndiye mastermind wa maovu yote yanayotokea nchini?!
Nitatoa ushahidi mchache kuthibitisha kauli yangu. Ametekwa Ulimboka,gazeti la Mwanahalisi likatimiza wajibu wake kwa jamii na likatekeza wito mkubwa wa Polisi jamii, kutoa clues za aliyemteka Dr Ulimboka. Matokeo yake gazeti limefungiwa. mwanzo watu hawakuelewa ni nani hasa aliyeshinikiza kufungiwa gazeti hilo, jibu tulilipata Addis Ababa, wakati mkulu, alipokuwa anahudhuria kikao cha wakuu wa nchi za Afrika, alipojiapiza kuwa kamwe hatalifungulia gazeti la Mwanahalisi, kwa kuwa limechochea maaskari kuasi!
Hilo lilikuwa ni jambo la hatari mno kwa nchi, kwa Rais wa nchi kudanganya waziwazi ilimradi tu ahalalishe udhalimu wake!!
Tukio la pili ni la Mwangosi, pamoja na mkulu kuwa mtumaji mzuri sana wa salaam za rambirambi kwenye misiba mbalimbali, kwenye msiba wa Mwangosi, hakutaka kabisa kutuma salaam za rambirambi, na kuthibisha kuwa kuna namna fulani ali-collude na wahalifu, kwenye tukio hilo! Pamoja na watu na makundi mbalimbali kumtaja kamanda Kamuhanda kuwa ndiye aliyetoa amri kwa askari aliyemfyatululia bomu Mwangosi, Kamuhanda siyo tu hajafikishwa kwenye vyombo vya sheria, bali pia mteule wake Rais hajamsimamisha kazi kwa tendo lake hilo la uovu wa hali ya kutisha mno!!
Tatizo kubwa la watawala madhalimu popote Duniani, wanapoona wamezungukwa na vyombo vya mabavu vya dola wanaamini watadumu madarakani milele, lakini kitu wanachokisahau ni kuwa Historia inasema hakuna mahali popote Duniani ambapo vyombo vya dola vilishinda nguvu ya Umma wakati wote. Mifano michache barani Afrika ni Misri,Tunisia, Libya na Ivory Coast!!