Kuteswa kwa Kibanda: Ridhiwani na Nape matatani!

Kuteswa kwa Kibanda: Ridhiwani na Nape matatani!

Mungu atuhurumie tanzania yetu inazama
 
Mkuu unakumbuka baada ya makala hiyo, Vyombo vya dola vililifanya uchunguzi na kugundua kuwa ni uzushi na kwamba hakuna chuo kama hicho?
Inaelekea wewe ni mmoja wa walio ndani ya vyombo vya dola! Weka jamvini taarifa hiyo!
 
Yani hii nchi imefikia pabaya sana,
Mtoto wa Rais anajiona ni Raisi wa watoto wote wa Tz
Mtoto wa Waziri mkuu anajiona Ni waziri Mkuu wa watoto wote Tz
Mtoto wa waziri anajiona ni waziri wa watoto wote wa Tz

Watanzania kazi tunayo especially kwa Sons & daughters of Peasant!!
 
Tuko, hebu funguka zaidi hapo kwa huyu mtoto wa Rais kuhusu ukerewe
 
Nape na riz one wote walipata dv 4 unategemea wataandika nini cha maana. ila ninawasifu waliocomment wamewapa ukweli wao hapohapo!

Mh! Div 4 ? alifikache chuo kikuu sasa? lakini kajitahizi sio kama dadayake mwanasha, hivi vipi amefaulu kwlei mwaka huu?
 
Once you are a public figure you must know that everything in you is a public figure, your movement, your tongue, your wife, your children, your husband, your dog, cat, pig, all are public figure.
The only thing that you need to be is to listen before speaking, and all your belongings shall follow you.
 
mkuu facebook sio mahali pakumuadabisha, huyu mtoto, nasema waombe mungu maisha yawehivyo ccm iendele kuwa madARAKANI,lasivyo watajibia hayoyote wayatendayo sasa.
 
Huu sio udhaifu wa ccm wala viongozi wetu ila NI UDHAIFU WA SISI WANANCHI wenyewe, haiwezekani tufanywe wajinga kiasi hiki. Wakati wa ulimboka, Kova alijinadi mbele ya vyombo vya habari kuwa wamemkamata mtuhumiwa mkenya ilhali wakijua ni uongo.

Akafa Mwangosi, tume ya nchimbi wakaja na majibu ya hovyo hovyo tupo kimya tu. Ujinga huo hauwezi kufanywa na nchi nyingine. Tumewapa sisi nafasi ya kufanya yoote na kutudharau kiasi hiki.

tunaangaika kutafuta vivutio vya kuingia kwenye seven wonder wakati vituko na matukio yanayoendelea vinatosha
 
Hawa akina BASHE na RIDHWANi wana mambo yao binafsi si unajua tena Vijana? hakuna sababu yoyote ya kumhusisha Rais katika hili.
Thatha unakosea na unajua kabisa kuwa unakosea! Hawa waliomo madarakani wanapanga nani agombee urais 2015 ili aendelee kuwalinda viongozi hawa ambao wanaifisadi nchi kwa namna wanayotaka kwa kipindi hiki ambacho wapo madarakani. Kwa Kibanda kuonesha mapenzi ya dhati kwa yule mgombea mtarajiwa ambaye kwa kweli ni mwiba mchungu kwa hawa jamaa waliomo madarakani na hawa 'madogo', Bashe na Ritz1, wanafahamu fika hilo. Hivyo wanapambana, Bashe upande wa mgombea mtarajiwa ambaye kashadhalilishwa sana na utawala wa sasa na Ritz1 upande wa utawala wa sasa, ambao unapigania umweke mgombea 'puppet' kwa ajili ya usalama wao. Hili lipo wazi kwa all Great Thinkers hapa.
 
hii ndo kazi ya ccm na rais wake dhaifu kikwete........... na tutakwisha na kumalizwa na hawa mafisadi
 
Ombeni mungu awape miaka 20 tena ijayo muone mafisadi na walewa madaraka ya baba yao watakavyohangaika ktk hii dunia. Malipo ni hapa hapa labda wafe mapema. Hao wote wanafaa kunyongwa tena pale uwanja wa taifa ili fundisho la wengine.
 
mkuu Tuko fanya mpango na mimi niipate hiyo makala ya chuo cha magaidi.. kama kuna link tafadhali nijuze mkuu. salute kwako
 
Last edited by a moderator:
ccm tool box .jpgndio michezo ya ccm ya kutumia makoleo, Halafu baadae wanawahi mitandaoni kutoa matamko ya kujilinda na kukimbilia hospitali kutoa pole.NASHAURI HIYO PICHA HAPO ITUMIKE BASI KWENYE NEMBO YA CHAMA CHAO.
 
Rais wetu ndio anayetakiwa kuwa mkali kwa familia yake na kuwaeleza wanamweka mahali pabaya kama kiongozi wa nchi.Labda kama hili hawalielewi.Unless kama Urais wake ni wa Familia yake.
Wewe wasema baba awakemee watoto, wakati yeye ndiye mastermind wa maovu yote yanayotokea nchini?!

Nitatoa ushahidi mchache kuthibitisha kauli yangu. Ametekwa Ulimboka,gazeti la Mwanahalisi likatimiza wajibu wake kwa jamii na likatekeza wito mkubwa wa Polisi jamii, kutoa clues za aliyemteka Dr Ulimboka. Matokeo yake gazeti limefungiwa. mwanzo watu hawakuelewa ni nani hasa aliyeshinikiza kufungiwa gazeti hilo, jibu tulilipata Addis Ababa, wakati mkulu, alipokuwa anahudhuria kikao cha wakuu wa nchi za Afrika, alipojiapiza kuwa kamwe hatalifungulia gazeti la Mwanahalisi, kwa kuwa limechochea maaskari kuasi!

Hilo lilikuwa ni jambo la hatari mno kwa nchi, kwa Rais wa nchi kudanganya waziwazi ilimradi tu ahalalishe udhalimu wake!!

Tukio la pili ni la Mwangosi, pamoja na mkulu kuwa mtumaji mzuri sana wa salaam za rambirambi kwenye misiba mbalimbali, kwenye msiba wa Mwangosi, hakutaka kabisa kutuma salaam za rambirambi, na kuthibisha kuwa kuna namna fulani ali-collude na wahalifu, kwenye tukio hilo! Pamoja na watu na makundi mbalimbali kumtaja kamanda Kamuhanda kuwa ndiye aliyetoa amri kwa askari aliyemfyatululia bomu Mwangosi, Kamuhanda siyo tu hajafikishwa kwenye vyombo vya sheria, bali pia mteule wake Rais hajamsimamisha kazi kwa tendo lake hilo la uovu wa hali ya kutisha mno!!

Tatizo kubwa la watawala madhalimu popote Duniani, wanapoona wamezungukwa na vyombo vya mabavu vya dola wanaamini watadumu madarakani milele, lakini kitu wanachokisahau ni kuwa Historia inasema hakuna mahali popote Duniani ambapo vyombo vya dola vilishinda nguvu ya Umma wakati wote. Mifano michache barani Afrika ni Misri,Tunisia, Libya na Ivory Coast!!
 
Back
Top Bottom