Habari za mchana.
Hii nimeitoa kwenye familia moja kanda ya ziwa.
Hivi ulishawahi kuona familia fulani ina watoto wengi lakini mmoja haolewi,au haoi na akioa anaacha ndoa haidumu.
Au kama ni mwanamke anaachika ili tu arudi Kwa wazazi?
Unakuta kijana anapambana lakini hatulii,anajikuta anaacha nyumba yake na kurudi Kwa wazazi?
Au binti anazalishwa mpaka watoto wanne na wanaume tofauti lakini ndoa zake zote hazidumu?
Hebu fuatilia kisa hiki cha mwanaume wa miaka 40,akinisimulia kisa chake baada ya kusoma mikasa yangu hapa Jamii forum.............
Naitwa Moses (siyo jina halisi) nimezaliwa moja ya mkoa maarufu kanda ya ziwa,nimezaliwa mwaka 1985 katika familia ya watoto wanane,watano wakiwa wa kiume na watatu ni wa kike. Huku Mimi nikiwa ni mtoto wa mwisho kuzaliwa.
Nilibahatika kumaliza shule ya msingi mwaka 2001 ,huku nikifaulu vizuri Sana kiasi cha wazazi wangu pamoja na Kaka na dada zangu kunisaidia ili niendelee na masomo ya pili ,nilisoma hadi kidato cha nne nikashindwa kufaulu vizuri kwenda advance hivyo nikarudi nyumbani nikajiunga na moja ya Kaka zangu kwenye biashara yake ya samaki.
Kifupi nimedumu kwenye biashara hiyo miaka mingi nikiwa na Mtaji wangu,hadi kufikia hatua ya kujenga kibanda changu (nyumba) hatua ambayo iliniweka kwenye mazingira mazuri kwani niliaminiwa,nilipendwa kijijini kwetu,lakini hata wanawake walinipenda nadhani ni kwasababu ya maendeleo niliyokuwa nayo.
Na ilipofika mwaka 2012 niliweza kutangaza ndoa na moja ya mchumba wangu wa muda mrefu Aitwaye zawadi, taratibu za kuoana zilifuata na ndoa ikapata baraka Kwa wazazi wote wanne.
Zawadi ni mwanamke ambaye tulipendana sana,Kwanza tulifanana vitu vingi ikiwemo wote kuwa ni malast born,hii ni moja cha pili familia Yao nao wapo wengi kama Sisi huku wao wakiwa tisa na mwanaume ni mmoja tu ya Yule first born ,waliofuata wote ni jinsia Ke.
Lingine ni heshima na maadili ya familia ile kuanzia dada zake namna wote walivyotulia kwenye ndoa zao lakini pia namna walivyo wazuri,zawadi ni moja ya wanawake weupe na Mimi mtu mweupe mrefu ulikuwa ni ugonjwa wangu kiukweli.
anasimulia Moses.
Mimi: siyo wewe tu Mimi mwenyewe Kwa mwanamke mweupe sipindui meza na nikiwekewa mtego ni rahisi kunasa (tunapeana tano na kucheka)
Moses:Ni kweli bro lakini sisi kabila letu tumezidi,yaani tangu zamani mwanamke mweupe alipewa thamani kubwa.(Huku akicheka zaidi)
Mimi:hebu nambie maisha yalikuwaje baada ya kuoana.
Anaendelea kusimulia..................
Bro we acha tu,Kwanza maisha yalianza vizuri kama tupo kwenye beach ya kimataifa vyakula vizuri,pesa nilizochangiwa,zilitosha Mimi kukaa mwezi mzima bila kujihusisha na kazi yeyote,fungate ilikuwa fungate kweli .
Na baada ya miezi minne ya ndoa yetu mke wangu kipenzi ilionekana ana ujauzito,hili lilinifurahisha sana pamoja na yeye mwenyewe alifurahi mno muda mwingi tuliangaliana na kutabasamu,licha ya ujauzito wake bado alifanya kazi Kwa bidii pamoja na kunionesha kunijali kama mume,nilipotoka kazini alinipokea Kwa shangwe,alinipa pole alinihurumia lakini niendapo kazini hakusita kunihusia kuwa makini.
Nilivimba nilijiona mwanaume mwenye bahati kana kwamba hakuna mwanaume mwingine aliwahi kuoa.
Hata baadhi ya washikaji walinionea wivu kimtindo hakika nilikuwa mfano wa kuigwa kama mtu anayeifaidi ndoa yake.lakini baada ya muda fulani mimba ilivyokuwa kubwa mke wangu alianza kubadilika, uvivu,kunijibu akijisikia,kutokuwajibika kwenye majukumu yake ndani ya familia pamoja na hujiamini,yaani ule uoga ulimtoka aliweza nijibu atakavyo.
anaweka kituo moses
Inaendelea........👇
Sehemu ya pili.
Mimi: Mimi nadhani ni kawaida pindi wake zetu wakiwa kwenye hali hiyo.
Moses: bro ni kweli ila kwangu ni tofauti kidogo,baada ya kuona mke wangu simuelewi nikaamua kuwaeleza mmoja dada zake mmoja ambaye yeye aliolewa hapo hapo kijijini kwetu,hivyo kabla ya kumweleza yeyote niliona yeye ni msaada zaidi.nakumbuka alinijibu sawa,huku akinipa pole na kuniahidi tukutane saa za jioni baada ya kazi kesho yake.
Kweli siku insyofuata kama kawaida jioni dada wa mke wangu alikuja nyumbani Kwangu akiwa na mwanamke mwenzie akimtambulisha kama rafiki yake,tukawa watu wanne,nilieleza matatizo ya mke wangu pamoja na vituko vyake,huku wote wakinisikiliza Kwa makini,baada ya kumaliza maelezo yangu mke wangu aliulizwa ana maana gani kunifanyia Yale yote lakini alikataa akidai tupo sawa , wala hakuna shida yeyote,ni Mimi nimemtafsiri vibaya.
Baada ya hapo dada yake aliniomba nitoke nje waongee watatu,nikafanya hivyo,walitumia kama nusu saa kisha wakatoka na dada mtu akanihakikishia kuwa mambo yale hayatajirudia tena,nilifurahi kimtindo kisha wageni wakaondoka.
Usiku wa siku hiyo haukuwa vizuri ni kama nilizidisha Tatizo badala ya kulitatua,mke wangu alinuna mara kumi zaidi.
Ila nikaacha tu kesho asubuhi kulipokucha nikaenda kwenye mishe zangu, lakini baada ya kurudi jioni sikumkuta,piga simu weeee lakini haikuonesha kupokelewa japo vitu vyote vilikuwepo ila begi lake dogo sikuliona nikathibitisha katoroka,moyo ulianza kuniuma,wivu haukucheza mbali,hasira kidogo zilininyemelea lakini nilitulia nikaenda Kwa mwenyekiti wetu kumpa taarifa za kupotelewa na mke wangu.
Mwenyekiti alishauri tu kuwa ningepiga nyumbani kwetu Kwanza huenda yupo Kwa wazazi wangu,nikaambiwa hayupo ,usiku Kwa usiku nikakodi pikipiki mpaka kwao kwakuwa hapakuzi mile Saba,nilimkuta akiwa na bashasha akipiga stori na mama yake mzazi.
Nilimsalimia mama Mkwe kisha nikakaribishwa ndani,nikamkuta Baba Mkwe nikamsalimia naye huku uso wake ukiongea Jambo.
Enheee baba tumempokea mwenzio tangu asubuhi anadai mna matatizo vipi imekuwaje? aliuliza baba Mkwe.
Ni kweli tulikuwa na matatizo takribani mwezi mzima,lakini Jana nilimuita Shemeji (jina kapuni)alitusuluhisha ila nimeshangaa narudi jioni hii sioni mtu.
Nilijibu.
Baba Mkwe alimuita mke wangu na kumtaka aeleze matatizo yake.
Mke wangu hakuwa na majibu ya kueleweka zaidi ya kujiumauma tu hapo Baba Mkwe alifoka na kumtaka mke wangu arudi nyumbani Kwangu,huku akidai maelezo aliyoambiwa asubuhi yanatofautiana hata hivyo,alikuwa anasubiri maelezo ya pande zote mbili,hata hivyo kashaujua ukweli hivyo mke wangu ainuke tuondoke.
Lakini ghafla aliinuka mama Mkwe na kudai yeye hawezi kuruhusu mwanaye arudi kwangu kwasababu moja Kwa moja inaonesha hatuna maelewano hivyo akaomba mwanaye nimuache Kwanza.
Baba,Mimi ndiye niliyemnyonyesha mkeo zawadi,Mimi mwanangu namfahamu ana hasira na wewe unaonesha Una hasira hivyo kulingana na hali ya tumbo lake nisingependa arudi kwako , kwasababu huyu anahitaji uangalizi,faraja,na mambo mengine yasiyo ya maudhi sasa naomba niachie mwanangu.mama Mkwe alisema.
Baba Mkwe alishindwa kuelewa alimwangalia mkewe ,akamgeukia mwanaye akahisi kuna kitu ,ugomvi ukaanza Baba anasema mwanaye arudi Kwa mumewe ,mama anasema kama alimzaa Kwa uchungu ,hawezi ruhusu mwanaye arudi abadani.
Mimi kuona vile nikaaga nikaondoka Kwa hasira Sana nikajikuta naanza kumchukia mama Mkwe.
Nikiwa njiani nilipokea simu ya mke wangu ,lakini aliyeongea ni mama Mkwe.
Baba Kwanza usijisikie vibaya na nadhani unaijua Hali ya mkeo vizuri Sana cha kufanya wewe tulia mwanangu huyu ni mkeo,Mimi nawaona wote mna hasira hivyo wewe katulie na mwenzako akiwa sawa atarudi.aliongea mama Mkwe huku Mimi nikiwa sijatia neno.
Inaendelea......