EvilSpirit
JF-Expert Member
- Jun 15, 2017
- 13,579
- 21,407
Haya mambo ya kuendelea ya kidwanzi sana meku
Cool downHaya mambo ya kuendelea ya kidwanzi sana meku
Hadithi yenyewe ya uongo halafu unaleta mambo ya itaendeleaCool down
Sijawahi kuleta visa vya uongo we kama Una matatizo yako sema tu usilete hasira Kwa kila mtu dogoHadithi yenyewe ya uongo halafu unaleta mambo ya itaendelea
Fanya yote lakini usikosee kuoa.
Mbona fupi hivi naona umezoea kazi, mbona jana umeandika ndefu mkuu?Sehemu ya tano.
Naitwa Daniel ni mwanachama wa jamiiforum Kwa muda sasa,nafanya kazi zangu za kihandisi baada ya kustaafu Kwa hiyari mwaka 2021. Huu ni mwendelezo wa kisa hiki nilichosimuliwa na mwenyeji wangu wa kanda ya ziwa huku akiruhusu niweze kuandika nikiweza.
Sasa endelea...
Niliondoka Kwa hasira pale mgahawani huku nikipanga kufanya fujo kubwa kwenye familia ya mke wangu.
Kiukweli nilimpenda mke wangu zawadi lakini kusikia aliwahi kuolewa hii ilinifanya nijione nipo uchi kwani maringo na kuvimba kote huenda baadhi ya watu walikuwa wakinicheka tu.kuna muda usilolijua halisumbui lakini kitendo cha kuyajua haya nilihuzunika sana,nilipiga simu Kwa baadhi ya ndugu zangu nikiwaeleza tabia za mke wangu,pamoja na niliyoyasikia Kwa Fatuma.
Hakuna ndugu aliyenishauri kuachana na mke wangu,kila mtu alinieleza kuwa mwenye maamuzi ni mimi.huku kile kitendo cha kuniacha nikajikuta nawaza mambo mengi.
Kumbuka wakati hayo yote yakiendelea hakuna simu yeyote iliyoingia toka Kwa mke wangu hili liliniumiza mno nilitamani angepiga,hata angenidanganya chochote ningeridhika hakika mapenzi yanaumiza sana.
Siku iliisha huku kila nalopanga nikilipangua nakujikuta sina la hata Jambo moja lililokaa kwenye njia badala yake,nikajikuta napitiwa tu na usingizi.
**************************
Sasa Jana ndiyo ulifanya nini uliondoka na kuniachia bili , lengo lako lilikuwa nini yaani ulipanga kunidhalilisha?
Hivi ulijifanya umechanganyikiwa wewe ni wa Kwanza kuoa,Kwanza nikwambie tu sipendi na sitohitaji mazoea yeyote na wewe,Kwanza uliniita mwenyewe halafu ukaniacha na Deni,hakika wewe ni mjinga Sana, halafu umekaa kimya yaani hata huwazi Mimi nilisolve vipi ule msala?
Unadaiwa elfu 18000/-nililipa huku nikiwa sijui ulikuwa na maana gani anyway nipe hela yangu mengine nimekusamehe.
aliweka kituo Fetty akionesha alichukia mno.
Nisamehe dada , nisamehe mimi niliongea huku nikitoa wallet yangu na kuchomoa noti tatu za shilingi elfu kumi na kumkabidhi dada Fetty.
Siku nyingine ukome,na ukome na ushamba wako kwani mbona watu tumeachwa na tulikubaliana na hali na maisha ya naendelea? Eeeeh
Wewe Musa ni kijana handsome lakini pia ambaye huwezi kosa mwanamke hata ukitangaza ndoa Leo hii lakini Umechagua kujiumiza , kwasababu gani, punguzeni ushamba .aliongea Fetty huku akiondoka.
Niliingia barabarani huku simu za lawama toka Kwa washirika wangu kwenye biashara wakilaumu sana,hatimaye Nikafika kwenye kambi zetu.
Moses unazingua tena unazingua mno, siku tatu hujatokea kazini,mbaya zaidi hupigi simu,na ukipigiwa hupokei Kwa wakati.alilaumu mmoja wa washirika wangu
Siyo kutopokea tu saa nyingine hapatikani kwenye simu sijui anasumbuliwa na nini huyu ila ngojasiku adhulumiwe ndiyo atajua hicho anachokifanya kina madhara gani.wadau walizidi kulaumu.
Naomba mniwie radhi wazee,Nina matatizo kidogo kwenye familia.nilijitetea.
Wewe matatizo gani watu wasijue,msiba,ugonjwa ama nini,na unajua kabisa tuna kikundi chetu cha kusaidiana pindi mtu akipata Tatizo,sasa ni tatizo gani ambalo husemi?wewe unampenda Sana mkeo yaani unamdekeza kihindinl Sana watu wooote wanajua kuwa tangu uoe ufanisi kazini umepungua,Acha dharau kila mtu akiwa na matatizo halafu asitoe taarifa anaamua kukaa kimya itakuwaje?
walilaumu Sana,wakati huohuo simu yangu iliita ikiwa ni mke wangu kipenzi zawadi,niliiangalia Kwa muda huku nikiwa nusu ya furaha na nusu ya hasira.
Nini kitajiri usikose Sehemu inayofuata
Inaendelea........