Kutoana kafara kwenye familia, na Siri ya wazazi wetu

Kutoana kafara kwenye familia, na Siri ya wazazi wetu

Sehemu ya nane.

Moses alichukua usafiri wa pikipiki na kuondoka huku akiwa na wasiwasi kidogo kwani alihisi kashachelewa.

Baada ya kufika kituo kile kilicho mbali na nyumbani kwake, aliingia mpaka mapokezi huku akitoa ile barua ya wito na kumkabidhi afande aliyemkuta pale mapokezi.

Kwani unaitiwa nini wewe,eti jamani huyu Moses anahitajika ofisi gani.aliuliza afande mmoja.

Huyu amsubiri mkuu wa kituo ndiye mwenye shida naye.kwanza nifuate nina mahojiano na wewe (alijibu afande mwingine huku akiashiria Moses amfuate)

Karibu Moses,
Karibu Sana naitwa afande (jina kapuni)
Mkuu wa kituo ana shida na wewe na alisema ukifika nikuweke Lockup lakini Mimi ni binadamu,nimeona nikuulize maswali kadhaa.

Kwanini unafanya biashara haramu Kwa kisingizio cha samaki,yaani una biashara kivuli huku ya samaki huku Una magendo unafanya,hivi mnadhani serikali imelala eeeh.aliuliza yule afande huku akiandika vitu kwenye karatasi fulani.

Mimi nafanya biashara ya samaki,hiyo ya magendo ni ipi naomba niijue.aliuliza Moses.

Hebu ngoja Kwanza mkuu kashafika hebu njoo huku , Kwanza uongee na mkuu.

********************

Wewe ndiye Moses!
Mbona hufanani na matendo yako?
Kwanini mnafanya biashara za kijinga.aliuliza mkuu wa kituo.

Afande,ungenieleza ni biashara gani nafanya ningekuelewa zaidi na nikiri wazi Mimi sifanyi biashara haramu.

Moses wewe unanitania ,wewe na wenzio mnalima zao lililokatazwa na serikali,huku mkijua mnafanya makosa,Sisi wasiri wetu wametudokeza jana tu kuwa wewe unalima zao haramu linalochangia kuharibu vijana.aliongea Kwa mkazo mkuu wa kituo.

Nina ushahidi Moses jana nimepigiwa simu na raia mwema tena anaonesha ni Mzee ,ni mbibi mtu mzima japo sina uhakika na umri wake .

Si hilo tu mnatumia vifaa vya uvuvi haramu ,mnakiuka Sheria mnafanya Kwa Siri Sana,huku mkijua ni kinyume na Sheria,

Lakini pia Moses,kijana mwenye nguvu ambaye hata siamini ninavyokuona,unajihusisha na unyang'anyi, kujipatia pesa Kwa njia ya udanganyifu hayo yote yanatoka Kwa msiri wetu.Moses ilitakiwa uwekwe ndani ufunguliwe mashtaka lakini Mimi nimekuita ili nikuonye kwakuwa aliyenipa hizi taarifa kagoma kunipa ushirikiano.
afande aliweka kituo.

Afande ,Mimi ni raia mwema kuanzia kwenye kijiji changu,mpaka kwenye taifa langu,Mimi ni mtoto wa mkulima,na Mimi ni mkulima pia,lakini najishughulisha na biashara ya samaki ikiwa ni kuitumia fursa ya rasilimali asili tulizopewa na Mungu,nafuata Sheria na taratibu zilizowekwa na nchi,sasa afande niseme tu taarifa ulizopewa ni za uongo Mimi sijawahi kulima zao haramu, sijawahi nyang'anya au kupora.
aliongea Kwa hisia Moses huku uso wake ukionesha masikitiko.

(Huku akicheka)
Moses nakuruhusu uende,Mimi Nina zaidi ya miaka 25 nipo kwenye jeshi la polisi ,watu wenye kutia huruma kama wewe huku wakiwa ni majambazi wa kutosha nimekutana nao mara nyingi sasa wewe niletee maigizo kama sijakuweka ndani . afande alimtisha Moses.

Akiwa njiani Moses hakuhisi njaa,
Alipiga hatua za haraka huku akiwa mwenye Mawazo, mambo chungu mzima yalimkabili, ndoa yake iliyumba,yeye anabambikiwa kesi , lakini kubwa zaidi akiniuliza,ni Nani huyo Mzee aliyepiga simu polisi?
Aliwaza jinsi anavyoishi vizuri na wanakijiji,hata angekuwa anafanya biashara haramu bado wangemstahi tu

au ni Fatuma?
Fatuma hii barua ya wito kapewa na nani?
au ni Fatuma ndiye aliyenisakizia ubaya Kwa polisi?

Lakini naambiwa ni mbibi aliyepiga simu,au ni mbinu za afande kumkwepesha muhusika?

Moses alijiuliza maswali mengi huku akichukua usafiri na kurudi nyumbani,ambapo hakumkuta mkewe.

Vitu vilivyokaa shaghlabaghala ikiwemo maji yaliyomwagwa ovyo sebuleni, lakini TV,na baadhi ya vifaa vya umeme vilipasuliwa vibaya mno , aliingia chumbani na kukuta baadhi ya nyaraka zake , makaratasi ya usajili na kumbukumbu kibao zimeharibiwa vibaya.

Moses alicheka,alicheka kila alipoona vitu vilivyoharibika ,Mungu wangu nisaidie,Mungu nipe nguvu Mimi ni mkosefu ndiyo ila Kwa hili Mungu nitie nguvu ,niepushe na majaribu.
Moses aliongea peke yake,
Aliingia jikoni na kukuta vitu vingi vimeharibiwa , mwanaume machozi yalimtoka siyo kwasababu ya hasara alizozikuta,ila ni kwasababu aliziona dalili za kumpoteza mwanamke anayempenda.

Alitoka nje akiangalia huku na huko aliiona tu watu wakiwa bize na mambo yao.

Moses alijikuta ana mikosi, tena matatizo yaliyokuja na kutua Kwa pamoja,alijikaza na kurudi ndani,alichukua picha mbalimbali walizopiga yeye na Zawadi kwenye harusi yao, alijikuta anadondosha machozi, mwanaume alililia MAPENZI, Moses alimlilia Zawadi.
Moses alimpenda mno zawadi.

****************

aliingia mtaani Kwa kazi moja tu kumtafuta fatuma.alihitaji kuongea naye,baada ya kumsaka Kwa muda mrefu alimpata,.

Niambie moses niliwaza nakupataje maana Nina maongezi ya muhimu mno na wewe.Fetty aliongea.

Siyo wewe tu,hata Mimi Nina shida na wewe,hebu niambie barua uliyoleta jana ulipewa na nani? aliuliza Moses.

Mimi niliipata kutoka Kwa washirika wenzio tena alinipa Kwa kunilazimisha, aliniambia ana haraka,hata hivyo nilijua mkeo hayupo ningejua hata nisingekuja, mkeo anaongea nyie,yaani zawadi ni msumbufu mno.ila hebu tuache hayo enheee niambie Moses umeitika wito maana niliona ni wito kutoka polisi.aliongea Fetty Kwa bashasha asijue maumivu ya Moses .

Sawa nikushukuru ngoja niende,
aliaga Moses huku akiangalia saa yake na kugundua ni saa kumi na moja jioni hajapata chochote,tangu mchana wa Jana yake,kwani tangu zianze vurugu hakupata time ya kula.

Moses alipambana mwenyewe hakumpigia ndugu, jamaa wala Nani kumweleza masuala yale .aliamua kupambana.kwa kiwango alichompenda zawadi aliwaza mengi mno,alirudi ndani kuikuta hali iko vile vile (kumbe vitu angepanga nani?

Akaamua kujilipua Kwa kumpigia simu mkewe kipenzi Zawadi.

Lakini licha ya kupiga mara nyingi haikupokelewa.akatulia huku akiwaza mengi aliyosingiziwa Kwa kuonesha ana biashara haramu eti.

Simu yake iliita mpigaji alikuwa ni mkewe kipenzi Zawadi.Alicheka kidogo huku akiwa anaangalia simu ile huku akiangalia sebule ilivyoharibiwa ,simu ilikatika,ikapigwa tena,akaipokea safari hii huku akiwa mpoooole,

Hello mke wangu, mbona unanifanyia hivi?aliongea Moses mara baada ya kupokea ile simu.

Mtoto mjinga, mpumbavu mwenye laana wewe,kwanini umempiga mwanangu,yaani umempiga kuanzia Jana usiku hadi asubuhi, ulivyoridhika ukamwacha na kutokomea na kwenda zako huku ukiwa huwazi , ukaona hata akifa ni sawa tu kwakuwa haja ya moyo wako ushamaliza.

Hivi unajua ni Kwa kiasi gani nampenda mwanangu,nilimpa jina la zawadi kama ishara na shukurani Kwa Mungu Kwa kunionesha maajabu,nimemzaa nikiwa na umri mkubwa usiotarajiwa kupata mtoto,lakini kwakuwa Kwa Mungu kila Jambo linawezekana,nilishukuru kwa Zawadi aliyonipa,ambayo wewe leo umeamua kujipigia tu,sawa Kwa hili wewe kijana utanitambua Mimi ni Nani.alikuwa ni mama Mkwe wa Moses akiongea maneno makali huku Moses akiwa hajatia neno lolote .kisha simu ikakatwa upande wa pili.

Moses akashusha pumzi ndefu huku akisafisha na kukusanya vioo vya TV pamoja na meza yake vilivyoharibiwa vibaya.

Moses anampenda Sana mkewe Zawadi,kuna taarifa mbaya iko polisi ikilenga kumchafua Moses,Nani muhusika?

Itaendelea.................
 
Habari za mchana.

Hii nimeitoa kwenye familia moja kanda ya ziwa.

Hivi ulishawahi kuona familia fulani ina watoto wengi lakini mmoja haolewi,au haoi na akioa anaacha ndoa haidumu.

Au kama ni mwanamke anaachika ili tu arudi Kwa wazazi?

Unakuta kijana anapambana lakini hatulii,anajikuta anaacha nyumba yake na kurudi Kwa wazazi?

Au binti anazalishwa mpaka watoto wanne na wanaume tofauti lakini ndoa zake zote hazidumu?

Hebu fuatilia kisa hiki cha mwanaume wa miaka 40,akinisimulia kisa chake baada ya kusoma mikasa yangu hapa Jamii forum.............

Naitwa Moses (siyo jina halisi) nimezaliwa moja ya mkoa maarufu kanda ya ziwa,nimezaliwa mwaka 1985 katika familia ya watoto wanane,watano wakiwa wa kiume na watatu ni wa kike. Huku Mimi nikiwa ni mtoto wa mwisho kuzaliwa.

Nilibahatika kumaliza shule ya msingi mwaka 2001 ,huku nikifaulu vizuri Sana kiasi cha wazazi wangu pamoja na Kaka na dada zangu kunisaidia ili niendelee na masomo ya pili ,nilisoma hadi kidato cha nne nikashindwa kufaulu vizuri kwenda advance hivyo nikarudi nyumbani nikajiunga na moja ya Kaka zangu kwenye biashara yake ya samaki.

Kifupi nimedumu kwenye biashara hiyo miaka mingi nikiwa na Mtaji wangu,hadi kufikia hatua ya kujenga kibanda changu (nyumba) hatua ambayo iliniweka kwenye mazingira mazuri kwani niliaminiwa,nilipendwa kijijini kwetu,lakini hata wanawake walinipenda nadhani ni kwasababu ya maendeleo niliyokuwa nayo.

Na ilipofika mwaka 2012 niliweza kutangaza ndoa na moja ya mchumba wangu wa muda mrefu Aitwaye zawadi, taratibu za kuoana zilifuata na ndoa ikapata baraka Kwa wazazi wote wanne.

Zawadi ni mwanamke ambaye tulipendana sana,Kwanza tulifanana vitu vingi ikiwemo wote kuwa ni malast born,hii ni moja cha pili familia Yao nao wapo wengi kama Sisi huku wao wakiwa tisa na mwanaume ni mmoja tu ya Yule first born ,waliofuata wote ni jinsia Ke.

Lingine ni heshima na maadili ya familia ile kuanzia dada zake namna wote walivyotulia kwenye ndoa zao lakini pia namna walivyo wazuri,zawadi ni moja ya wanawake weupe na Mimi mtu mweupe mrefu ulikuwa ni ugonjwa wangu kiukweli.
anasimulia Moses.

Mimi: siyo wewe tu Mimi mwenyewe Kwa mwanamke mweupe sipindui meza na nikiwekewa mtego ni rahisi kunasa (tunapeana tano na kucheka)

Moses:Ni kweli bro lakini sisi kabila letu tumezidi,yaani tangu zamani mwanamke mweupe alipewa thamani kubwa.(Huku akicheka zaidi)

Mimi:hebu nambie maisha yalikuwaje baada ya kuoana.

Anaendelea kusimulia..................

Bro we acha tu,Kwanza maisha yalianza vizuri kama tupo kwenye beach ya kimataifa vyakula vizuri,pesa nilizochangiwa,zilitosha Mimi kukaa mwezi mzima bila kujihusisha na kazi yeyote,fungate ilikuwa fungate kweli .

Na baada ya miezi minne ya ndoa yetu mke wangu kipenzi ilionekana ana ujauzito,hili lilinifurahisha sana pamoja na yeye mwenyewe alifurahi mno muda mwingi tuliangaliana na kutabasamu,licha ya ujauzito wake bado alifanya kazi Kwa bidii pamoja na kunionesha kunijali kama mume,nilipotoka kazini alinipokea Kwa shangwe,alinipa pole alinihurumia lakini niendapo kazini hakusita kunihusia kuwa makini.

Nilivimba nilijiona mwanaume mwenye bahati kana kwamba hakuna mwanaume mwingine aliwahi kuoa.
Hata baadhi ya washikaji walinionea wivu kimtindo hakika nilikuwa mfano wa kuigwa kama mtu anayeifaidi ndoa yake.lakini baada ya muda fulani mimba ilivyokuwa kubwa mke wangu alianza kubadilika, uvivu,kunijibu akijisikia,kutokuwajibika kwenye majukumu yake ndani ya familia pamoja na hujiamini,yaani ule uoga ulimtoka aliweza nijibu atakavyo.
anaweka kituo moses

Inaendelea........👇

Uchawi ni siri kubwa sana
Wengi wanateseka lakini wanaowatesa ni watu wao wa ndani kabisaaa

Halafu wanawapooza kwa kuuita uchawi mizimu
 
Hii chai ya rangi inaendelea lini Jack Daniel ?
Kama ambavyo sijawahi kupenda kusoma visa vya kutunga,ndivyo ambavyo naenjoy kupost true story safari hii stori ikiwa hainihusu mimi Bali kijana Moses.kwa ruhusu yake tumekubaliana niandike huku nikizingatia code.

Hivyo ukiona ni chai usijisumbue kufuatilia,usiuhangaishe moyo na ubongo Kwa kuulisha taarifa za uongo
 
Kama ambavyo sijawahi kupenda kusoma visa vya kutunga,ndivyo ambavyo naenjoy kupost true story safari hii stori ikiwa hainihusu mimi Bali kijana Moses.kwa ruhusu yake tumekubaliana niandike huku nikizingatia code.

Hivyo ukiona ni chai usijisumbue kufuatilia,usiuhangaishe moyo na ubongo Kwa kuulisha taarifa za uongo
Muendelezo vipi mkuu?
 
Kama ambavyo sijawahi kupenda kusoma visa vya kutunga,ndivyo ambavyo naenjoy kupost true story safari hii stori ikiwa hainihusu mimi Bali kijana Moses.kwa ruhusu yake tumekubaliana niandike huku nikizingatia code.

Hivyo ukiona ni chai usijisumbue kufuatilia,usiuhangaishe moyo na ubongo Kwa kuulisha taarifa za uongo
Tatizo unachelewa kuleta muendelezo
 
Back
Top Bottom